SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Nimesikia mara nyingi maafisa mbalimbali wa polisi wakionya wahalifu kwa kusema: Atakayekamatwa kwa kosa....... atapata adhabu kali. Nikisikia hivyo huwa najiuliza: Adhabu hutolewa na jeshi la polisi au mahakama? Na kama ni mahakama, je, hakimu ana discretion katika utoaji wa adhabu kali?
Kwa uelewa wangu mdogo wa sheria najua kwamba kila kosa (jinai) lina adhabu yake kisheria. Sasa hiyo adhabu kali mapolisi wanayoizungumzia inatoka wapi?
Hebu wataalamu wa sheria naomba muujadili huu msemo upendwao sana na jeshi la polisi.