Tukio ambalo sitakaa nilisahau

Tukio ambalo sitakaa nilisahau

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Nakumbuka kipindi hicho redio ilikuwa inatangaza mpira wa simba na yanga sasa tukawa tunasikiliza, mimi nikamuuliza mzee mmoja sasa simba anacheza mpira na huyo yanga!!vipi huyo yanga hamwogopi simba!!!yule mzee akanijibu yanga ni mkali balaa anampiga simba!!

Mi nikamuuli huyo yanga kwani ni mnyama gani!! Yule mzee akanijibu kama unataka kuwaona pasua hiyo redio watatoka huko utawaona!!mimi nikamwambia unasema kweli?? Yule mzee akasema ni kweli ngoja niondoke alafu uipasue utaona mwenyewe!! Yule mzee akaondoka mimi nikaona ni kweli!!

Nikamwambia dogo apande juu ya mti dogo akapanda mimi nikaandaa ngazi nikaweka kwenye mti nikaenda kuchukua shoka la baba mvunguni mwa kitanda!

Asee hamuwezi amini niliikung'uta ile redio shoka nikakimbilia ile ngazi nikapanda juu ya mti kusubiri simba na yanga watoke,Kumbe yule mzee alinidanganya!
 
Nilikuwa ninasikiliza kipindi cha kweli na Aspro, niliangusha redio, wakati ninaiokota Julius Kilua mtangazaji alisema tumeanguka. Nilikimbia kwa mama mama mama kumbe kuna watu wanaishi kwenye redio, alinielewesha lakini ilinichukua muda sana kuelewa ile coincidence ya mimi kuinua redio na mtangazaji kujua kuwa walianguka!!
 
tehtehteh...mzee noma sana...
yaa-jpg.354121
 
Nilikuwa ninasikiliza kipindi cha kweli na Aspro, niliangusha redio, wakati ninaiokota Julius Kilua mtangazaji alisema tumeanguka. Nilikimbia kwa mama mama mama kumbe kuna watu wanaishi kwenye redio, alinielewesha lakini ilinichukua muda sana kuelewa ile coincidence ya mimi kuinua redio na mtangazaji kujua kuwa walianguka!!
😀😀😀 oblongata ilikuwa haisomi
 
Hiyo kurudisha chenji ni ni lazma mkuu maana kadri unavyo zinywa zinazidi kuwa chungu[emoji2] [emoji2] [
 
Nilikua nasikiliza Mpira,sasa mchezaji mmoja akafunga goli lakini refa akalikataa eti mchezaji alikua "Ameotea"

Nikashangaa sana na kujiuliza;

"Hivi huyu refa alijuaje kama huyu mchezaji aliota kua leo atafunga goli?"

Utoto raha sana..!!
 
Ha Ha ha ha, nakumbuka enzi hizo nilikuwa mtundu nikaunganisha speaker kwenye socket ya umeme kwa kutumia waya wa taa za mti wa Christmas nikitegemea iimbe mziki kama wa Redio. Kilichotokea sasa....!!!!
 
Duuuu mkuu umeuwa sisi tulikuwa tunafunikiaga spiker kwenye chungu dadeki surbufer imesigiziwa kitu kinachotoka hapo! Na hapo unakuta mabetri kama kumi na tatu hvi yameunganishwa[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
umri wako na unayoyaandika haviendani kabisa
 
Back
Top Bottom