MR MAJANGA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2014
- 3,444
- 10,687
Nakumbuka nilibadili njia kisa sanamu la bismini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hahahahaaaa nimecheka jf hapana chezeaNakumbuka kipindi hicho redio ilikuwa inatangaza mpira wa simba na yanga sasa tukawa tunasikiliza, mimi nikamuuliza mzee mmoja sasa simba anacheza mpira na huyo yanga!!vipi huyo yanga hamwogopi simba!!!yule mzee akanijibu yanga ni mkali balaa anampiga simba!!
Mi nikamuuli huyo yanga kwani ni mnyama gani!! Yule mzee akanijibu kama unataka kuwaona pasua hiyo redio watatoka huko utawaona!!mimi nikamwambia unasema kweli?? Yule mzee akasema ni kweli ngoja niondoke alafu uipasue utaona mwenyewe!! Yule mzee akaondoka mimi nikaona ni kweli!!
Nikamwambia dogo apande juu ya mti dogo akapanda mimi nikaandaa ngazi nikaweka kwenye mti nikaenda kuchukua shoka la baba mvunguni mwa kitanda!
Asee hamuwezi amini niliikung'uta ile redio shoka nikakimbilia ile ngazi nikapanda juu ya mti kusubiri simba na yanga watoke,Kumbe yule mzee alinidanganya!
Uwezo wako wa kunyanyua Shoka na kuvunja redio kisha kupanda ngazi na kukimbilia juu ya mti inaonyesha kabisa kiumri ulikua umeshakua sema ulichelewa tu kupata akili!Yaani mkuu nikitumia nguvu kubwa sana kukung'uta ile redio maana yule mzee akiniaminisha sana kuwa ndani mle hao wanyama wapo na nguvu nilotumia ni kubwa hata kama wangekuwepo ningechanganya ubongo zao kiwiliwili maana nilipiga kwa ngucu zangu zote!! Ebu emagine shoka ubebee juu kwa nguvu zite upige nalo redio [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Nilikua nasikiliza Mpira,sasa mchezaji mmoja akafunga goli lakini refa akalikataa eti mchezaji alikua "Ameotea"
Nikashangaa sana na kujiuliza;
"Hivi huyu refa alijuaje kama huyu mchezaji aliota kua leo atafunga goli?"
Utoto raha sana..!!
Nilikua nasikiliza Mpira,sasa mchezaji mmoja akafunga goli lakini refa akalikataa eti mchezaji alikua "Ameotea"
Nikashangaa sana na kujiuliza;
"Hivi huyu refa alijuaje kama huyu mchezaji aliota kua leo atafunga goli?"
Utoto raha sana..!!
Pamoja sana Mkuu "Mtumishi wetu"Nipo kijijini nabofya Kitecno changu necheka hadi basi.
Wenzangu wananishangaa!!
Ubarikiwe!!