Tukio gani hautolisahau mwaka 2021?

Tukio gani hautolisahau mwaka 2021?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
3,862
Reaction score
6,438
Naam
Wakuu nadhani baadhi yetu tukiwa sehemu mbali mbali za dunia au nchini tulijaribu namna moja kuvuka kutoka 21 kwenda 22.
Kila mtu akifanya kwa namna yake

Kama lengo la kichwa hapo juu ni tukio gani lilikunyoosha mpaka kufikia hatua ya kutolisahau au ni tukio gani ulikutana nalo lilikuinua kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Ukafanikiwa
Na hautolisahau


Binafsi mwezi may pale 2021 nilipata kamchongo ka party time ambayo ningevuta mkwanja flani mrefu sana ambao nlishaupangia bajeti kabisa na ratiba.

Ilikuwa green city huko lahaulla nikaazima gari ya jamaa damu damu kabisaa na alinielewa maana si mara moja kuinuana kwenye shida sasa ile kufika maeneo ya igawa pale wakati naliendea jiji la mbeya
Asalaaale!! nikaangusha chuma wakati nakwepa boda boda iliyojichanganya

Matokeo yake nikawa kwenye matibabu na kibarua kikaota nyasi baadaya kuchelewa , kilichoibuka ni kufanya matengenezo ya gari na kula hasara maradufu

Allhamdulliah shukraani kwa Mola bado napumua na nina nafasi ya kundelea kuzisaka nyingine

VIPI KWAKO ULIKUTANA NA DHAHAMA AU TUKIO LENYE NEEMA IPI???
 
Nimepitia mengi magumu na mengine mazuri tu. Good thing ni kuwa najua hakuna kitu au hali ya kudumu hapa duniani so nilipokuwa katika nyakati ngumu nilijua zitapita na nilipokuwa katika nyakati nzuri nilijitahidi kuzifurahia vilivyo maana nazo nilijua zitapita.

Bado nasonga.
 
Sitausahau huu mwaka mi nauita mwaka wa madeni nashukuru mungu sikuweza kujidhuru kuna wakati hadi nilisema kwanini nipo nilipo kwanini nisingebaki level za kuwaza kesho ndakula nini kwanini hapa nilipo sitaki nishuke nikakumbuka majamaa walivokuwa wanapambana shuleni wasishuke top 3 halafu wahuni hata hatuwazi tuna namba zetu spesho kutoka mwisho nikajisemea kumbe jamaaa waliteseka sana
 
Mimi kubwa zaidi kwangu nilikuwa na mchepuko wangu ambaye alinipenda sana hata siwezi simulia. Huyu dada wako mapacha na mwenzeke Tena wale wa kufanana hasa. Mwenzake ameolewa Sasa Kuna siku watu wasiojulikana na hawawajui hawa pacha waliniona niko na mchepuko wangu si wakaenda kwa jamaa kumwambia mkeo anatoka na mhakiki. Bwana lilitokea timbwili la asha ngedele na halijaisha ninahama nalo kwenda 2022. Yaani hawa pacha hawa acha kabisa.
 
Kwa kweli yapo mengi mabaya na mazuri ila Rais Samia kunipandisha daraja june 2021 ilinivusha ktk hali fulani ngumu, nmeamua kuikumbka hii.
 
Mimi kubwa zaidi kwangu nilikuwa na mchepuko wangu ambaye alinipenda sana hata siwezi simulia. Huyu dada wako mapacha na mwenzeke Tena wale wa kufanana hasa. Mwenzake ameolewa Sasa Kuna siku watu wasiojulikana na hawawajui hawa pacha waliniona niko na mchepuko wangu si wakaenda kwa jamaa kumwambia mkeo anatoka na mhakiki. Bwana lilitokea timbwili la asha ngedele na halijaisha ninahama nalo kwenda 2022. Yaani hawa pacha hawa acha kabisa.
[emoji1][emoji2][emoji1] nmecheka km mazuri.
 
Back
Top Bottom