Tukio gani hautolisahau mwaka 2021?

Tukio gani hautolisahau mwaka 2021?

Rafiki yake Bwana mkubwa alivo wa danganya watu ktk nyumba ya Ibada kama wasiwe na wasi wasi boss ni mzima na anawasalimia Jamani kumbe maiti ana sema na kumtuma mjumbe
 
Naam
Wakuu nadhani baadhi yetu tukiwa sehemu mbali mbali za dunia au nchini tulijaribu namna moja kuvuka kutoka 21 kwenda 22.
Kila mtu akifanya kwa namna yake

Kama lengo la kichwa hapo juu ni tukio gani lilikunyoosha mpaka kufikia hatua ya kutolisahau au ni tukio gani ulikutana nalo lilikuinua kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Ukafanikiwa
Na hautolisahau


Binafsi mwezi may pale 2021 nilipata kamchongo ka party time ambayo ningevuta mkwanja flani mrefu sana ambao nlishaupangia bajeti kabisa na ratiba.

Ilikuwa green city huko lahaulla nikaazima gari ya jamaa damu damu kabisaa na alinielewa maana si mara moja kuinuana kwenye shida sasa ile kufika maeneo ya igawa pale wakati naliendea jiji la mbeya
Asalaaale!! nikaangusha chuma wakati nakwepa boda boda iliyojichanganya

Matokeo yake nikawa kwenye matibabu na kibarua kikaota nyasi baadaya kuchelewa , kilichoibuka ni kufanya matengenezo ya gari na kula hasara maradufu

Allhamdulliah shukraani kwa Mola bado napumua na nina nafasi ya kundelea kuzisaka nyingine

VIPI KWAKO ULIKUTANA NA DHAHAMA AU TUKIO LENYE NEEMA IPI???
Kifo cha muuwaji.
 
Nimepitia kipind kigumu lakin yote kwa mapenzi ya mungu.
Baba aliondoka january, baada ya mda akafwata bibi, akafwata tena shangazi bibi na baadae akafwata baba mdogo mtoto wa babu mkubwa.
Isitoshe nilikuwa na wife naye ni mjamzito alaf sina kazi niko nabangaiza dah! Familia bado pande zote yangu na nlioachiwa inanitizama, ila hakika mungu ametupigania uhai bado upo.

When success is near the road gets tough hlo nlilitambua bado napambana.
Jah bless 2022.
 
Mimi kubwa zaidi kwangu nilikuwa na mchepuko wangu ambaye alinipenda sana hata siwezi simulia. Huyu dada wako mapacha na mwenzeke Tena wale wa kufanana hasa. Mwenzake ameolewa Sasa Kuna siku watu wasiojulikana na hawawajui hawa pacha waliniona niko na mchepuko wangu si wakaenda kwa jamaa kumwambia mkeo anatoka na mhakiki. Bwana lilitokea timbwili la asha ngedele na halijaisha ninahama nalo kwenda 2022. Yaani hawa pacha hawa acha kabisa.
😅😅😅😅🤣
 
Sitausahau huu mwaka mi nauita mwaka wa madeni nashukuru mungu sikuweza kujidhuru kuna wakati hadi nilisema kwanini nipo nilipo kwanini nisingebaki level za kuwaza kesho ndakula nini kwanini hapa nilipo sitaki nishuke nikakumbuka majamaa walivokuwa wanapambana shuleni wasishuke top 3 halafu wahuni hata hatuwazi tuna namba zetu spesho kutoka mwisho nikajisemea kumbe jamaaa waliteseka sana
Madeniiii
 
Nimepitia kipind kigumu lakin yote kwa mapenzi ya mungu.
Baba aliondoka january, baada ya mda akafwata bibi, akafwata tena shangazi bibi na baadae akafwata baba mdogo mtoto wa babu mkubwa.
Isitoshe nilikuwa na wife naye ni mjamzito alaf sina kazi niko nabangaiza dah! Familia bado pande zote yangu na nlioachiwa inanitizama, ila hakika mungu ametupigania uhai bado upo.

When success is near the road gets tough hlo nlilitambua bado napambana.
Jah bless 2022.
Kabiiisa jaah bless
 
Tukio la kufungwa kwa Kampuni niliyokuwa nafanya kazi kwa sababu ya Covid -19 na kunifanya nikae bila kazi mda mrefu nikiwa na maisha magumu ambayo sijawahi yaona. nashukuru Mungu sasa niko fresh.
Mungu yu mwema
 
Back
Top Bottom