Complicator
JF-Expert Member
- Aug 23, 2013
- 2,208
- 3,609
Arsenal Bwana, Acha tufurahie tu ubingwa…..
Nakumbuka mwaka 2012 ilikua siku ya tarehe 28/8.
Nikiwa kidato cha tano Rungwe sekondari, Tukuyu.
Hii siku ilianza kama siku zingine za kwaida tu kwa mwanafunzi, sababu ilikua jumapili basi baada ya kutoka ibadani watu tukawa na ratiba zetu za kawaida kabisa.
Kipindi hicho ushindani kati ya Man united na Arsenal ulikua umevuka mipaka hadi kuwaingia watu ndani kabisa, siyo kama sasa hivi. Kipindi hicho manchester united ya moto sana. Ya moto sana, kuna vijana wa Gen-Z hawaeezi elewa hii.
Nyie madogo…..kukutana na Man united wakati huo ilikua ni kama kukutana na jinamizi, walikua kwanza wana tabia ya kukuacha uwafunge goli moja….vile unavyoshangilia nadhani ndio ilikua inatumika kuwapa hasira.
Sasa turudi kwenye stori…..
Hii siku bhana tukapanga kutoroka usiku kwenda kiwira kutazama mechi, umbali kutoka shule mpaka kiwira ni zaidi ya kilomita 8 kwa kutembea kwa miguu halafu ni usiku. Wanaojua mazingira ya Tukuyu wanaelewa, lazima uvuke mito midogo na vilima vya kupanda na kushuka wakati wa hiyo safari…
Shida ilianza wakati tu tunatoka kuvuka fensi, Rungwe haina ukuta…ila ilikua ukikutwa tu eneo fulani unaambiwa umeruka ukuta na kesi yake ni kubwa sana, Ticha mwakatobe ndio wa nidhamu huyo.
……ile tunamaliza tu kuondoka kwanza tukaonwa na ticha Mwakatobe, ila kwa sababu ya uzito wa mechi yenyewe tukasema potelea pwete bhana, kama fimbo tushachapwa sana bhana, haoooooooo tukaondoka zetu mpaka kiwira, hapo tupo kama mtu 6 hivi.😃😃😃😃
Hawa sita mashabiki wa Arsenal tulikua wawili tu, mimi na mwanagu mmoja anaitwa Clay, Clay alikua jamaa fulani bonge ana mwili, halafu mii naishi naye sijui kumbe bhana ni “wa kishua”
Clay ndio alikua anadhamini show ya pesa na kila kitu, mimi na yeye ndio mashabiki wa Arsenal wengine wote man U. Sasa sababu ya kujiamini tumetoka tu, akavua Sare ya shule akavaa jezi ya Arsenal, kwa wakati ule kuwa na jezi ya timu ilikua ni anasa sana hasa kwa kule kijijini na mwanafunzi.
Tumefika bhana, mechi ikaanza kama zingine tu….
Yaliyotokea wote mnakumbuka😂
Sasa stori iko hapa…..
Clay kumbe toto la kishua, hajazoea bhana mbilinge mbilinge za mabanda umiza…ile kuchekwa na kukejeliwa sana akachukua personal, sijui ikawaje….mara akarusha ngumi kwa mwanakijiji. Eeeehh bhana eeh, zikaanza fujo pale.
Kumbuka wanakijiji huwaga na hasira sana na wanafunzi…shule ilikua ni ya Boys tupu. Sasa mara Clay akapigwa kata funua pale kuja shtuka yuko kalala chini haelewi, na sisi hatuna cha kufanya zaidi ya kuwaambia na kuwaomba wale raia yaishe….Wakayamaliza, ila Clay kumbe sasa stress zikarudi.
Imagine
1. umetembea kilomita 8, na hujazoea
2. Umepigwa goli 8-2 na mpinzani
3. Umepigwa ngumi na kudhalilika
4. Umevimba uso, ina maana kesho shule ndio ingekua habari inatrend, na yeye alikua ni masifa.
5. Unawaza kurudi kutembea kilomita zingine 8 na usiku, Rungwe ni baridi. Halafu wale jamaa 6 wa Man u hawajapoa bado wanahanikiza😃
8. Unawaza alishakuona Mwakatobe, kwahiyo kesho Jumatatu Assembly yumo wa kwanza anakutafuta wakati zinaimbwa nyimbo za shule😃😃😃
Clay bhana akaona “cha kufia nini” mara ghafla akasimama kwa hasira “Oyaaa mii sirudi shule, naacha shule” Siwezi haya mambo. Tunamuuliza Clay mambo ganiiiii….yeye anawaza bakora za kesho.
Jamaa kama utani, akasema tumuache kiwira…tukasema hatukuachi, akagoma…akachukua kasimu kake ka tochi akatuonyesha salio analo kama 180,000/= , Kwao ni Iringa, Gangilonga.
Akasema anachukua gari anarudi zake nyumbani, kule gari coaster hadi usiku sana zilikua zinapatikana.
Jamaa kweli bhana, aliondoka na aliacha shule siku ile ile…sijui alifikaje kwao, ila asubuhi mapema aliandika ujumbe kwa mkuu wa shule kwamba “asitafutwe” karudi nyumbani. Na alipiga simu kwao kwamba kashindwa shule anarudi.
Mii sijui hataa ilikuaje, ila tulikuja kukutana chuo DIT….2013.
Mwanangu alikufa kile kipindi cha COVID-19, sijui kwa sababu gani….Ila tayari mzee wake alikua keshampa mtaji ana kampuni ya ufundi wa umeme.
Kilichotukuta sisi shule kesho yake ni FEDHEHA…
Kwa waliosoma Boarding wanajua nini huwa kinafuatia ukikutwa na kesi ya kuruka ukuta usiku, tena kutoroka…
Aaahh ticha Mwakatobe yule bwege alikua anajua kukomalia jambo.
Leo Arsenal imekua bingwa.
Jambo gani unalikumbuka linalohusiana na fedheha kuhusu Arsenal???
😃😃😃😃😃