Siku ya kwanza kupangwa kutumikia altare (watoto watumishi kwa wakatoliki naamini wanaelewa) ilikua mwaka 2004. Nilikua na mzuka sana siku hiyo. Mida fulani usiku hivi nikakurupuka kitandani kucheki saa ukutani mshale upo kwenye 12 (saa sita usiku) mimi na wenge langu nikaileta kwenye kiswahili, nikajikoki huyo vuup nikaenda church huku home sijafunga milango wala nini nikiamini kumeshakucha (niliirudisha tu)
Nikaanza kukanyaga road, kufika mahala nikakuta dogo mmoja anakata gogo na lile giza tumeshtuana kila mtu njia yake (baadae tulikuja kujuana tukaishia kucheka tu) kufika church walinzi ndio wananitonya kua we dogo mbona sasa hivi ni saa sita usiku, nikataka kurudi home wakanizuia wakaniambia nipoe kwenye nyumba yao. Mbwa wao nae akanitilia nux, kila nikisinzia ananifokea "sikulala usiku kucha, mpaka saa 12 inafika tunapanda altareni nina bonge la usingizi, nikaishia kusinzia altareni [emoji2] na kukosea mwanzo mwisho na viongozi walikuepo basi baada ya hapo nikala mvua (adhabu) ya kutosha.