KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Kuna muda akili zetu hupatwa na wenge inakuwa Kama ufahamu umeyumba flani hivi,tunaweza sema ubongo umeyumba kwa muda!..
Ktk kumbukumbu nilishawahi mzingua father kwa wenge nililokuwa nalo..!
Ilikuwa hivi usiku nilibaki sebuleni mwenyewe nikiwa naangalia mkanda enzi bado VHS zipo,huku wengine wakitopea vyumbani na kwenda kupiga mbonji.. mwenyewe nikapata wasaa wa kujimwayamwaya na VHS ya ngumi.. Sasa mkanda ukaisha huku nikiwa na wenge la usingizi kichwani nikajiambia nikautoe then nikalale,Hilo ndo lilikuwa wazo na lilisubiri vitendo tu! Na wazo hilo lilibaki kichwani likilandalanda huku nikitopea kwenye usingizi wa pono..
Ebhana we si mzee katoka ktk mizunguko yake usiku ule akagonga mlango nikasikia kabisa,nilichofanya si kwenda kufungua mlango ni moja kwa moja nikaelekea kutoa ule mkanda maana ndo wazo lililokuwepo kichwani..😅
Sasa ubovu ile deki ilikuwa mizinguo Batani ya kutolea mkanda ilikuwa imeshakufa so nikawa nalazimisha kuutoa mkanda ili ndo nikamfungulie!
Nayeye ndo akawa anakazana kugonga alipoona mbona siji akachungulia dirishani nipo bize nahangaika na deki huku nikimuambia nakuja..😂
Akaongeza ugongaji huku akifoka zaidi maana nae alikuwa nzwiii.. he he kwani komamanga wa watu nilikuwa naelewa! Ndo kwanza Niko bize kutoa mkanda sielewi kabisa!
Ilibidi mpk mtu mwengine aamke huko ndo aje amfungulie! Sasa hapo ndo nikaipatapata nilichezeshwa mateke na mabanzi mpk nikakaa sawa.
Sikumbuki hata nilifanikiwa kuutoa ule mkanda au vipi nachokumbuka nilikula kibano tu..😂😂
Nyengine ilikuwa usiku familia tumetulia tunacheki tv Sasa na redio ilikuwa inalia kwa mbali.. mzee mzima Kama kawaida yangu nikapitiwa usingizi,nikaamshwa nikalale chumbani.. nilichokifanya niliinuka nikaenda nikazima redio nikarudi nikakaa!!😅
Ikabidi waniangalie tu wakaniacha na wenge langu..
Karibu tushee mawenge yaliyotukumba najua Kuna wengine wamekuwa na mawenge mpk yakaleta madhara!… Tufanye Kama sehemu ya kujifunza na namna ipi ya kuweza kuzuia mawenge hayo.
Karibuni.