Tukio gani mtoto wako aliwahi kukufanyia ukashindwa hata kumpiga?

Tukio gani mtoto wako aliwahi kukufanyia ukashindwa hata kumpiga?

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Watoto wana vituko sana mda mwingine unaweza piga uue mfano huyu wangu aliondoka na rimoti mpaka shuleni tafuta limot tafuta haionekani kaja toka shule kakuta watu wanatafuta rimot ndio anasema nilibeba mimi hii hapa nikamwangalia huna jinsi unamuacha

Nyingine

Nikiwa mtoto kuna siku niligoma kula mchana nilikuwa napenda kula saa tisa sasa chakula by saa sita kinakuwa tayari mama angu akaja niamsha nikale nikamwambia mimi sitaki kula akaenda chukua fimbo ile anataka kunipiga nikamwambia mbona ninyi mkiwa hamjisikii kula hakuna anae wapiga?

Mama alicheka akaacha akaondoka zake je wewe mtoto wako kakufanyia nini?
 
"Baba Ona mimi avaa chupi ya mama"

Mtoto alitamka hayo akitoka chumbani kuja sebureni ambako nilikaa mimi nikipiga story na wageni kutoka Ukweni Yaani baba Mkwe, mama Mkwe na Shemeji yangu

Hapo sijui kama mtoto keshaingia chumbani kachukua chupi ya wife na kuvaa kama kanzu😂
 
"Baba Ona mimi avaa chupi ya mama"
Mtoto alitamka hayo akitoka chumbani kuja sebureni ambako nilikaa mimi nikipiga story na wageni kutoka Ukweni Yaani baba Mkwe, mama Mkwe na Shemeji yangu
Hapo sijui kama mtoto keshaingia chumbani kachukua chupi ya wife na kuvaa kama kanzu😂
Ahhahah ase wako kiboko sana
 
Mimi na mke wangu tulikuwa tunaongea na mtoto wetu tuliyempeleka English kozi kuhusiana na umuhimu wanelimu/kusoma. Mazumgumzo yetu yalikuwa hivi.

MKE WANGU: mwanangu mimi najuta kwa nini sikusoma shule yaani natamani nirudi udogoni ili nipate kusoma. Yaani ungekuwa unajua jinsi ninavyoona wivu nimwonapo mtu anaongea kiingereza.....
MTOTO WETU: Kwa hiyo mama mtu hawezi kuongeza kiingereza bila kwenda shule?
MIMI: Atawezea wapi......
MTOTO WETU: Mbona Kila siku usiku mama anaongea kiingereza anasema " Ooh fu**k, yes, yes, ooh yes. Ooh my god.....".
Haya maneno mama kayajofunzia wapi?

Duh! nililoa mwili mzima nikabadili mada juu kwa juu kwani wazazi wangu walikuwepo.
Hawa watoto kwa kwa kuaibisha.
 
Shakur yangu daima lazima simulizi hii iletewe movie maana hata script zipo wazi haitamhangaisha director
 
Back
Top Bottom