Tukio gani ukilikumbuka unacheka tu mwenyewe?

Maisha yana matukio mengi ambayo yana muunganiko wa moja kwa moja kwenye hisia zetu, hivyo unapoyakumbuka unaweza patwa na hisia ya huzuni au furaha.

Hivyo leo tukumbuke matukio ambayo tuliwahi yashuhudia yakatuchekesha,lakini hata baada ya siku, wiki, miezi au miaka kupita bado matukio hayo hutuchekesha tunapoyakumbuka hata tunapokuwa peke yetu chumbani, njiani au chooni.

Binafsi kuna matukio mawili huwa yananichekesha sana kila ninapoyakumbuka.

TUKIO LA KWANZA
Mwaka 2018 nilikua katika harakati zangu za kununua matisheti ya buku jero, pale karume, nilipomaliza nikavuka upande wa pili, pale wanapouza mabegi begi nikawa nasubiri gari ya Mabibo niirukie nirudi home.

Sasa kuna shehe mmoja alikua amekula kanzu nyeupe safi inayong'ara kama umetoka dukani jana. Sasa kuna ile mitaro mikubwa sana ya kupitisha maji taka, na shehe akawa anataka avuke bara bara kwa haraka, bahati mbaya akasahau kuwa mavaa kanzu na inabidi aikunjie kwa juu ili aweze kukimbia vema na kuruka ile mitaro. Hivyo shehe akajaribu kuruka ule mtaro, aisee ndugu msomaji kanzu ilimchota ngwara, shehe mzima mzima kaingia mtaroni mpaka akapotelea, nilishtuka sana lakini shehe alivyotoka ndani ya mtaro akiwa mzima wa afya aisee nilijikuta nacheka kila nikikumbuka hahahhah aisee shehe alikimbilia karume sokoni kutafuta hifadhi.

TUKIO LA PILI
kipindi nipo sekondari shule ya bweni, nilikua na tabia ya kudoji bwenini tukiwa na wana kibao wenye tabia kama zangu, kikubwa tulikua tukicheza karata na kupiga soga.

Sasa ilikua lazima awepo anaepiga chabo kuangalia kama kuna mwalimu anakuja,sasa siku hiyo kumbe walimu kama wanne hivi wamezunguka njia nyingine wakitaka kutuwinda.Tumekuja kushtuka wapo karibu sana na bweni, hivyo mpiga chabo alivyotushtua, ilikua pata shika.

Kila mmoja alikimbilia alikojua, sasa mimi nikakimbilia chooni nijifanye nilikuja kujisaidia haja kubwa,mwalimu akausoma mchezo akaja hadi vyooni akawa anafungua mlango mmoja baada ya mwingine, me nikawa nishavua suruali nimekaa mkao kabisa kama najisaidia, sasa mwamba choo cha pili alisahau kuvua suruali so akawa amechuchumaa huku amechomekea.

Me nasikia tu mwalimu anafungua milango ya karibu, mara akafungua mlango ambao niko mimi akanambia "dogo maliza fasta kimbia darasani"

Nikajua tu nimepona, sasa wakati namwaga nazuga kujisafisha ticha akaenda mlango alipo jamaa, akafungua akamkuta mwana kachuchumaa. Nikawa nasikia maongezi

Ticha akamuuliza jamaa, unafanya nini? Jamaa kwa woga akajibu "najisaidia" ticha akacheka sana akauliza "dogo unajinyea au? Unajisaidiaje umechomekea?" jamaa akakosa jibu akatolewa nje akila kichapo me nikapita kama siwajui huku kicheko kimenibana sana.

Tafadhali share nawe ni tukio gani lilikuchekesha na linakuchekesha mpaka leo.
unanikumbusha nilivyokuwa advance NGUDU secondary kuna ticha wa nidhamu anaitwa KWIBO aliwahi fanya hiyo akadaka wanafunzi wengi mimi ponea yangu nilivvua nguo zote nikazitundika nje ya choo nikabaki na boxer nikazama toilet..paranja lllikapita wakatolewa wote maana walikua hawako kimkao wa kujisaidia wakabbaki wananisubiri mwama nitoke 😂 .hawakuamini natoka na bboxer yangu nikapitia shati na suruali yangu nikatembea nikawaacha wanakula fito🤣 huku ticha wa nidhamu anasema kijana wahi darasani naona ulikua na kazi nzito😂😂
 
Mambo ya math bana

Darasa letu lilikua na watukutu sana mpaka mademu walipimda unakuta wako chimbo wameji mix na masela kukwepa pindi la math, ukienda darasani unakuta watu 20 hawafi

Teacher wa math alikua peace sana alikua very charming lakini asilimia kubwa ya wanafunzi tulilichukia somo ila tulimpenda mwalimu

Sasa siku moja akaingia darasani akasema leo sifundishi nataka niwa encourage muanze kupenda maths

Teacher akamuuliza mshkaji "kwa mfano hapo scars nini kinachokufanya usipende hesabu?"

Msela akasema "wabunifu wa hesabu hawakutaka tufaulu wengi na ndio maana wakaweka vikwazo ambavyo vinapingana na uhalisia"

Mwalimu akauliza "vikwazo gani?"

Mchizi akasema "Nimefanya quiz wiki iliyopita halafu karatasi inakuja eti nimekosa zote hadi hesabu za makadirio nazo nimekosa.

Makadirio maana yake ni kukisia, kubahatisha hakuna jibu la uhakika na ndio maana yameitwa makadirio

sasa nimekadiria lakini karatasi imekuja eti nimekosa, inakuwaje hapo teacher?
 
Kwenye draft sasa nilimkuta mzee wa makamo anacheza na kijana, yule mzee alikua ni mchungaji dogo alikua understanding hakua anamtolea lugha kali

Ikafika wakati pastor amebanwa anatafuta kete ya kucheza haioni, yule kijana akamuambia mzee cheza bao yesu anaponya ndio ila sio kwenye mabao
 
Maisha yana matukio mengi ambayo yana muunganiko wa moja kwa moja kwenye hisia zetu, hivyo unapoyakumbuka unaweza patwa na hisia ya huzuni au furaha.

Hivyo leo tukumbuke matukio ambayo tuliwahi yashuhudia yakatuchekesha,lakini hata baada ya siku, wiki, miezi au miaka kupita bado matukio hayo hutuchekesha tunapoyakumbuka hata tunapokuwa peke yetu chumbani, njiani au chooni.

Binafsi kuna matukio mawili huwa yananichekesha sana kila ninapoyakumbuka.

TUKIO LA KWANZA
Mwaka 2018 nilikua katika harakati zangu za kununua matisheti ya buku jero, pale karume, nilipomaliza nikavuka upande wa pili, pale wanapouza mabegi begi nikawa nasubiri gari ya Mabibo niirukie nirudi home.

Sasa kuna shehe mmoja alikua amekula kanzu nyeupe safi inayong'ara kama umetoka dukani jana. Sasa kuna ile mitaro mikubwa sana ya kupitisha maji taka, na shehe akawa anataka avuke bara bara kwa haraka, bahati mbaya akasahau kuwa mavaa kanzu na inabidi aikunjie kwa juu ili aweze kukimbia vema na kuruka ile mitaro. Hivyo shehe akajaribu kuruka ule mtaro, aisee ndugu msomaji kanzu ilimchota ngwara, shehe mzima mzima kaingia mtaroni mpaka akapotelea, nilishtuka sana lakini shehe alivyotoka ndani ya mtaro akiwa mzima wa afya aisee nilijikuta nacheka kila nikikumbuka hahahhah aisee shehe alikimbilia karume sokoni kutafuta hifadhi.

TUKIO LA PILI
kipindi nipo sekondari shule ya bweni, nilikua na tabia ya kudoji bwenini tukiwa na wana kibao wenye tabia kama zangu, kikubwa tulikua tukicheza karata na kupiga soga.

Sasa ilikua lazima awepo anaepiga chabo kuangalia kama kuna mwalimu anakuja,sasa siku hiyo kumbe walimu kama wanne hivi wamezunguka njia nyingine wakitaka kutuwinda.Tumekuja kushtuka wapo karibu sana na bweni, hivyo mpiga chabo alivyotushtua, ilikua pata shika.

Kila mmoja alikimbilia alikojua, sasa mimi nikakimbilia chooni nijifanye nilikuja kujisaidia haja kubwa,mwalimu akausoma mchezo akaja hadi vyooni akawa anafungua mlango mmoja baada ya mwingine, me nikawa nishavua suruali nimekaa mkao kabisa kama najisaidia, sasa mwamba choo cha pili alisahau kuvua suruali so akawa amechuchumaa huku amechomekea.

Me nasikia tu mwalimu anafungua milango ya karibu, mara akafungua mlango ambao niko mimi akanambia "dogo maliza fasta kimbia darasani"

Nikajua tu nimepona, sasa wakati namwaga nazuga kujisafisha ticha akaenda mlango alipo jamaa, akafungua akamkuta mwana kachuchumaa. Nikawa nasikia maongezi

Ticha akamuuliza jamaa, unafanya nini? Jamaa kwa woga akajibu "najisaidia" ticha akacheka sana akauliza "dogo unajinyea au? Unajisaidiaje umechomekea?" jamaa akakosa jibu akatolewa nje akila kichapo me nikapita kama siwajui huku kicheko kimenibana sana.

Tafadhali share nawe ni tukio gani lilikuchekesha na linakuchekesha mpaka leo.
Hii ya mabibo!! ume!!!tupiga za mbavu dogo!! soko la Karume na route za Mabibo wapi na wapi tena basi mwaka 208 weweee dogo!! nimekaa Ilala Boma na mabibo jeshini miaka kibao!!!! soko la karume pale hakuna mtaro wa kutisha mtu muzima
 
Back
Top Bottom