Aisee safari ya shule ni kweli kuna mengi, mengine huwa tunapenda nyakati zake zijirudie na mengine hatupendi kamwe na tunashkuru kuyavuka salama!
Msanga ulnikuta mimi aisee enzi hizo nikiwa std 3, nilikuwa napenda sana kucheza mpira wa miguu, shuleni nilikuwa kila wakati nipo uwanjani nasakata kabumbu!
Basi kuna wakati mama alinunulia mpira wa gozi aisee niliupenda sana nikawa naubeba shuleni, basi siku moja ilikuwa zamu ya mwalimu mmoja mkali sana, alikuwa akisifika kwa kutembeza njiti, hivyo ukionekana nje tu ni kiboko bila discussion!
Hivyo tukawa tumebanwa sana maana nje kulikuwa kunawaka moto, so nikaamua kucheza mpira mle class, jamaa yangu akwa mbele ya ubao na mimi nyuma ya darasa, enzi hizo hakukuwa na msongamano mkubwa sana wa wanafunzi , darasa lilikuwa na mikondo A na B , na ndani ya chumba kulikuwa mistari mitatu ya dawati hivyo tukawa tunapigiliana mpira kupitia ile space ya mstari na mstari wa dawati.
Aisee tukanogewa na mchezo tukajisahau kama wiki hiyo ni zamu ya yule ticha mkali wa mboko, basi ticha akashtukiza na kukuta tuko bize na kupiliana mpira, jamaa anapiga nadaka na kisha na mimi nampigia!
Basi huyo ticha akatudaka akaagiza viboko, monitor akaleta viboko vitano vilikuwa mijeredi ya uhakika! Basi yule ticha akamuanza yule jamaa yangu, alikuwa kila akipiga kiboko kinakatika kipande kinaruka mpaka batini!
Aisee kilipofika kiboko cha tano nikaona jamaa analia kama mtoto huku ticha akiagiza fimbo nyingine kwa ajili yangu, nilipojiakagua mwilini nikagundua siku hiyo ndani ya kaptula ya shule nilivaa bukta yangu flani nyepesi sana hivyo nikahisi hapa ntakufa!
Basi ticha akaelekea mlangoni kumta yule monitor awahishe viboko, aisee kuona hivyo haraka nikakwea dirisha, kisha nikavuta mafuta, akatuma jamaa wa std 7 wanifukuzie kunikamata, nilitoka mshale nikakata vichoro viwili, nikatokea mtaa mwingine nilishawauza! Huyooo mpaka home!
Kufika home nikamwambia mama naumwa alafu mwalimu anataka kunichapa viboko 10, Duu, kesho yake tukaenda shule na mama yule ticha ile kumuona mama akapoza, alichongea sana kwa mama lakini mama alijitahidi kukabiliana nae na kunitetea, basi akamuomba anipunguzie adhabu, akanishusha njiti 4, msanga ukawa umekwisha! Aisee zile siku mbili sintakuja kuzisahau! Mungu amrehemu Mwalimu wangu huyo, kwasasa ni Marehemu!