Mwanakulipata
JF-Expert Member
- Jul 17, 2018
- 714
- 1,193
Hii yangu nahisi ndo kiboko
Kipindi tupo form 4 mwanzo sana pale tulikuwa tukiletewa test hizi wasichana walikuwa wanatunyoosha sana sisi wavulana tukaanza kudharaulika darasani tukawa tunaitwa science B hii kitu ilituuma sana
Sisi wavulana Tukaongea na Monitor tukaandika barua tuwe tunabaki shule mpaka saa 2 usiku, ikumbukwe shule ilikuwa ni ya day...basi mkuu wa shule alikuwa anatuamini akatukubalia ila sharti lilikuwa ni wavulana only ndio tutakuwa tunabaki tukasema sio kesi
Kazi ikaanza rasmi piga misuriii weee tukaanza kuvuka mipaka..tukawa tunapika mpaka ubwabwa shule[emoji23][emoji23] tunachanga tunanunua mchele wale wanaokaa karibu wanaleta sufuria tunapika wali na maharage tukishakula tunafua nguo tunalala kabisa hapo hapo mpaka asubuhi...ikifika saa 10 tunavaa uniform tunaenda nje ya shule kutembea tembea ili tusishtukiwe
Sasa ijumaa kuamkia jumamos kabla mtihani wa mock wengi hatukwenda kulala shule walienda watu watatu tu...walivyofika wakasoma mpaka saa 7 usiku wakavizia mlinzi kaenda kwake ...wenyewe wakaenda kwenye madirisha ya chemistry laboratory wakaanza kukomba zile test tube zilizokaa meza ya kwanza kabisa pale dirishani...wakakusanya meza kama tatu hivi wanajaza kwenye mabegi yale makubwa nia yao wakauze kariakoo
Mlinzi akawaona na anawafaham vizuri...basi bhna akawaambia mbona mnataka kunifukuzisha kazi...kesho yake asubuhi tukaitwa wavulana wotee tuliokuwa tunalalaga pale shule mlinzi akatusema sanaa...mwisho akasema andikeni barua ya kukubali kama mmekutwa na vifaa vya shule ama laasivyo nitapeleka hii kesi kwa mwalimu mkuu jumatatu asubuhi...akaendelea kusema hii barua itakuwa kama makubaliano kati yangu na nyie..siku ijitokea mmeiba tena napeleka kwa mwalimu pamoja na hizi barua ila hii kesi ya leo nimewasamehe nyie andikeni barua
Hapa mlinzi alituchezea akili ukizingatia tulishapanick...tukaandika barua tukizani yatakuwa yameisha...jumatatu asubuh tupo kwenye mtihani wa Civics wa mock tunaona mlinzi amebeba yale mabegi na barua zipo mkononi anaelekea kwa headmistress...nilichanganyikiwa hata kuandika essay nilishindwa...(tulifeli hiyo mock kama kuku..wavulana wote chaliii)
Nikawaangalia wenzangu nikaona wapo kwenye sura za unyonge sana, mtihani ulivyoisha tukaitwa pale tukafungiwa darasa moja...anatoka mmoja mmoja kwenda kuhojiwa kwenye jopo la walimu..tokea saa 4 mpaka saa 8 tulivyomaliza kuhojiwa tukapelekwa kufanya mtihani wa pili wa geography
Shule nzima ilitujua aisee kesi ilikuwa nzito kila sehem tunaitwa wezi..yaani tulivyomaliza mtihani headmistress akiingia darasani anatuchoropoa wavulana anatutoa nje ni mwendo wa viboko tutaje wapi vifaa vilikuwa vinapelekwa..haipiti wiki bila kupigwa viboko...ila walikuja kukutwa na hatia ni wale waliokamatwa ile siku na wengine wawili...wakaambiwa warudi nyumbani kama wakitaka kurudi shule kuendelea kusoma waje na hela ya vifaa vilivyovunjika tokea mwaka uanze...walipigiwa mahesabu kila mtu aende na laki 4...
Wanangu nimewakumbuka sanaaa...[emoji119]