Dadakidoti
JF-Expert Member
- Jul 26, 2024
- 399
- 1,409
Poleni na majukumu ya hapa na pale. Nisiwachoshe kama mada inavyosema ni tukio gani ulifanya kwenye utoto wako hata familia yako haijui mpaka leo.
Mimi naanza nakumbuka kipindi nipo darasa la tano nilikuwa nasoma mkoa X kati ya wale Watoto ambao tulikuwa na akili nilikuwa mmoja wapo nilikuwa kati ya wale top 3 kwa akili za darasani. Hali ambayo ilikuwa inapelekea walimu wengi kunipenda sana. Sasa nakumbuka mwalimu mmoja Y alikuwa anatufundisha somo la Maarifa ya jamii alikuwa na tabia ya kutupa vitabu na jioni tunavikusanya na kuvirudisha ofisini. Sasa yule mwalimu alikuwa hawapi mamonita vitabu alikuwa ananipa mimi jukumu la kugawa vitabu kwa wenzangu na jioni kuvikusanya kuvirudisha ofisini.
Sasa siku moja mud awa kurudi nyumbani ulipokaribia nikakusanya vitabu kama kawaida nikaviweka kwenye meza ya mwalimu mbele ya darasa mara nikasikia wenzangu wanaruka Kamba kwa nje sasa mwenzenu hakuna mchezo nilikuwa naupenda kama kuruka Kamba baaada ya kuwasikia sinikaruka kupitia dirishani kuruka Kamba mchezo ukaninogea nikasahau jukumu la kupeleka vitabu kwa mwalimu kengele ilipogongwa ya kwenda mstarini ili turuhusiwe kurudi nyumbani ndo nikakumbuka kuwa vitabu sijapeleka. Sasa mwenzenu nirudi darasani sijakuta kitabu hata kimoja. Nikawauliza wenzangu kila mmoja anasema hajui. Nikawaza namwambiaje mwalimu na alikuwa mkali sana nikaamua kuuchuna.
Kesho yake asubuhi nyumbani tulikuwa tupo ndugu watatu wote tunasoma shule moja make tulikuwa tunakaa na babu na bibi basi nikaanza kujizungusha ili wenzangu waondoke nisiongozane nao. Huku nina mamba yangu kichwani walivyoona najizungusha wakaamua kuniacha. Nilivyohakikisha wameondoka nami nikatoka zangu nikapitia kwa mganga na miambili yangu ya kula shule nikampelekea mganga ili aniangalizie walioiba vitabu na wavirudishe
Nilivyofika kwa mganga nikamweleza kila kitu. Akazunguka nyuma ya nyumba yake akaleta majani akasema nifumbe macho nikafumba yale majani yakageuka karatasi akanambia ile karatasi nisiikunjue mpaka nafika shule wala nisiangalie nyumba pia nisiongee na mtu yeyote tena niende kwa kukimbia mpaka shuleni na ile karatasi nimpe mwalimu husika imeandikwa majina ya walioiba vitabu.
Jamaa nilitoka pale speed mia ila nilivyokaribia kufika shuleni ikabidi nivunje masharti ya mganga niligeuka nyuma nione kama kuna mtu nilivyoona hakuna anaeniona nikafungua ile karatasi nilishangaa nilichokutwa kimeandikwa mle.
Nanukuu “Sisi waze wa Kijiji tumeambiwa na huyu mtoto X Jina Langu kuwa jana alijisahau akaenda kucheza wenzake wakamwibia vitabu. Ameogopa kukwambia akaja kutwambia sisi hivyo tunamwombea msamaha. Wazee wa Kijiji. Nilisonya hela yangu kachukua, kanidanganya kuwa yameandikwa majina wezi kumbe ameandika uongo. Nikawaza nikimpa mwalimu akanituma wazazi nitasema ni wazee gani wamekaa kikao? Na babu atajua kuwa nimeenda kwa mganga wakati toka nipo pale sijawahi ona aende kwa mganga nikaichana ile karatasi nikaenda shule.
Sasa msiulize nini kilinikuta baada ya mwalimu kujua kuwa vitabu nimepoteza kwa uzembe ila sikuthubutu kumpa ile barua feki ya mgaga wala sikusema nyumbani kama nilienda kwa mganga ilikuwa siri yangu hata mama angu hajui kama niliwahi kwenda kwa mganga. Waganga waongo jamani kha! Miambili yangu inaniumaga mpaka leo.