Tulia Ackson unaamini Raisi wa nchi yetu hastahili kunyooshwa kidole, ona hii clip ya kilichotokea huko Uingereza kwenye Jumba la Waziri Mkuu uone jinsi dola ilivyojitenga na siasa na wanasiasa hata pale Waziri Mkuu anapopigwa kwa kukejeliwa na wananchi wa kawaida (sio Bunge wala wabunge).
Your browser is not able to display this video.
Hapo ni London nje ya Geti la 10 Downing Street kwa Waziri Mkuu. Wananchi wameamua kunfanyia PARTY nje kwa kumkejeli kuwa kavunja SHERIA kwa kufanya party wakati wa Corona. Hakuna aliyepigwa wala kukamatwa na Polisi. Jaribu Tanzania utapigwa kipigo cha MBWA.
Niki-copy na ku-paste hiyo video,inaleta kile kinachojulikana kama "hot linking
", kitu ambacho hapa JF hakiruhusiwi(hii kitu huwa sielewi logic yake kwanini wanazuia).
Ngoja nikusaidie Salary Slip, video yenyewe hii hapa...
Your browser is not able to display this video.
Wabunge wanamjadili Mkuu wao wa Serikali alivyo mjinga naye yupo anasikiliza! Kwa hapa kwetu siku hiyo hata FFU wangetinga ndani ya hilo bunge!
(Bahati mbaya, kwa sababu ya lugha, chawa hawataambulia kitu hapa!)
Na hapa wananchi wameamua kukusanyika nje ya jumba anakoishi na kumvurumishia kejeli na dharau bila bughdha yoyote ile...hiyo ndiyo siasa! Hebu angalieni...
Your browser is not able to display this video.
Ingekuwa hapa siku hiyo sijui wananchi wangapi wangepoteza maisha mikononi mwa polisi hawa wetu wenye kiu ya damu za Watanzania wanaoonesha tu hisia zao za kutokubaliana na hawa miunguwatu wetu!
Shukrani sana mkuu. Hawa wenzetu ndio maana wanaendelea.Kwao kuwa kiongozi sio kuwa Mungu mtu bali ni mtumishi wa watu tofauti kabisa na sisi.
Huku kina Lissu wakiwaeleza ukweli watawala, wanaonekana kama wahaini ,wakati kwenye hilo Bunge la Uingereza, Waziri Mkuu anapondwa utadhani ni mtu wa kawaida tu.
Tubadilike watanzania , viongozi sio malaika na waambiwe ukweli hata kama ni mchungu ndio tutasonga mbele.
Tulia Ackson unaemaini Raisi wa nchi yetu hastahili kunyooshwa kidole, ona hii clip ya kilichotokea huko Uingereza kwenye Jumba la Waziri Mkuu uone jinsi dola ilivyojitenga na siasa na wanasiasa hata pale Waziri Mkuu anapopigwa kwa kukejeliwa na wananchi wa kawaida(sio Bunge wala wabunge)...
Watu wazima hujenga hoja na sio matusi!! Kila mtu sura hupewa na Mungu , sasa kama wewe sura Yako ni nzuri ni nzuri kwa hao wanaokupenda na kwa wengine wewe sura yako ni mbayaaaaaaaa!! " Beauty is in the eyes of the beholder!!"
Very poor excuse
Yani mpaka mzungu anakuwa na uwezo wa kutushawishi mabaya sisi wenyewe akili tunakuwa tumeweka wapi? Kwani hatuna uwezo wa kutambua baya na zuri?
Blacks hatujitambui ndo maana hata matatizo yetu ya msingi bado tunaamini tumesababishiwa .
+1
Yani tupo kama boda boda , akipata ajali hata kama aligonga mti , atasema mti ulimchomekea!!!
Matatizo unaona kabisa ni la kuyatatua wenyewe , bado tunamsingizia mzungu,
Tulia Ackson unaemaini Raisi wa nchi yetu hastahili kunyooshwa kidole, ona hii clip ya kilichotokea huko Uingereza kwenye Jumba la Waziri Mkuu uone jinsi dola ilivyojitenga na siasa na wanasiasa hata pale Waziri Mkuu anapopigwa kwa kukejeliwa na wananchi wa kawaida(sio Bunge wala wabunge).
By Fatma Karume aka Shangazi kupitia twitter:
Hapa ni London nje ya Geti la 10 Downing Street kwa Waziri Mkuu. Wananchi wameamua kunfanyia PARTY nje kwa kumkejeli kuwa kavunja SHERIA kwa kufanya party wakati wa Corona. Hakuna aliyepigwa wala kukamatwa na Polisi. Jaribu Tanzania utapigwa kipigo cha MBWA.