Tukio la Aucho kumpiga Ajib mwamuzi alionekana tangu mwanzo anafuata maekekezo

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Your browser is not able to display this video.
Tangu mchezo umeanza mwamuzi alionekana kupanic na kujaribu kuwatisha wachezaji wa Coastal.

Binafsi niliwaeleza wadau kuwa hii mechi ingemsababishia mwamuzi kuadhibiwa na yeye alionekana kuwa tayari kwa lolote mradi Yanga wapate pointi 3.

Kama wasingefunga goli lile, ilikuwa imeandaliwa penalty na mchezaji angalau mmoja wa Coastal kupewa kadi nyekundu.

Wengi tulijua tukio la Aucho lilistahili kuadhibiwa kwa kadi nyekundu, hatothubutu kuitoa kwa kuwa ameshalambishwa asali
 
Hahahaa daa ila mashabiki wa Simba tuna moyo kumbe zile tano zilikua chache walitakiwa watuchape 7 ili tukose nguvu kabisa ya kuja humu yetu yametushinda tumekula 5 ghafla tumehamia coastal nako maumivu tiende wapi sisi sasa.
 
na nyie tuliwapa Pesa ngapi Budaaa
Mnajua wachezaji mliowarubuni mliwapa ngapi. Soka lilikuwa dk 45 za kipindi cha kwanza, kipindi cha pili yalikuwa maigizo.
 
Mnajua wachezaji mliowarubuni mliwapa ngapi.
Soka lilikuwa dk 45 za kipindi cha kwanza,kipindi cha pili yalikuwa maigizo

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app

Usiache kumeza dawa tu manake kile kipigo cha goli 5 bado kimekuchanganya kabisa wewe meza dawa upumzike.

Uzuri ile gemu Yanga walimhonga Mo kabisa [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Mmekosa uvumilivu wa kimichezo kabisa... Yani Tano tu mnaweweseka wiki nzima. Mlikuwa mnakufa nane kima nyie
 
Coastal union wana bahati kutokupata kadi nyekundu,

Kile kitendo cha refa kufuta kadi ya njano ya kwanza ya mchezaji wa coastal na kumuonesha njano nyingine alimpendelea mno maana ile ilikuwa yellow card ya pili na ni red card direct.
 
Mngecheza soka achaneni na hujuma katika soka.
Ninyi si chama cha siasa

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Mlipopigwa kono la nyani mlifanyiwa hujuma gani,yaani ushindwe wewe na timu yako kumfunga Yanga ndio uje kutegemea Coastal Union awape furaha kwa kumfunga Yanga? Tabuleeeee Laaaaaaaaaa
 
Acheni Upuuzi
 
Hivi UMEANGALIA MPIRA KWELI au unaandika kishabiki tu.
 
Asante Kwa Uzi lakini umejaa ushabiki usio na faida Kwa soka letu.
Kuanzia Leo mfuatilie Mwandembwa halafu Rudi upya utoe ulichogundua.
Katika kanuni za uamzi kuna kitu kinaitwa "time management". Huyu Kila Mechi hili suala katika marks 10 huwa anapata 3. Mwandembwa ni Mtu asiyezingatia mwenendo mwema wa Mwamuzi Kwa kusoma nature ya mchezo kabla ya kuanza kuuchezesha. Mechi ya Jana Tangu maneno ya Kocha FIKIRI kwenye mkutano na waandishi wa habari, Hadi mahojiano na Mtangazaji kabla ya mechi alieleza Wazi yeye anaingiza timu Kwa tahadhari maana anamheshimu Mpinzani wake. Ni Wazi Coast waliingia na concept ya kupoteza Muda Tangu dakika ya Kwanza. Chukua tukio la faulo ya kipindi cha Kwanza kuelekea Coastàl iliyozusha rabsha Musonda akaangushwa. Chanzo cha tukio ni Mwamuzi mwenyewe kukosa time management. Faulo haiwezi kuandaliwa na kupigwa baada ya dakika 4. Tangu mpira umetengwa mpaka fujo zinatokea zilipita dakika 4. Kama upishi basi Mwandembwa anapika Maharage kwenye jiko la mkaa(Waamuzi wanauelewa msemo huu).
Tukio la Aucho ni straight red card uko sahihi, lakini lilikuwa na Kadi ya njano Kwa Ajibu. Kitendo alichokifanya dhahiri ni upotezaji Muda wa makusudi na kutaka kumprovoke mwenzake naye akaingia mtegoni. Na kama Aucho asingefanya vile Ajibu bado asingechukuliwa hatua yoyote maana Hilo halikuwa tukio la Kwanza kupoteza Muda makusudi.
Beki Tatu wa Coastàl mpira ukitoka anapandisha Sox, anarekebisha kamba za viatu, anarekebisha shinguard, anaomba mpira mwingine ndo anarusha lakini katoka bila hata onyo.
Tatalila za Mwandembwa zinaongezeka kwenye tukio la Kadi ya njano Kwa beki wa Coastal badala ya mhusika halisi Triple "G". Kadi ya dakika ya 11 imekwenda kufutwa dakika ya 41???
Tukubaliane tatizo la waamuzi bado ni kubwa Sana narudia ni kubwa mno maana hata vitu vidogo kama hivi waamuzi wengi wanaogopa Wachezaji.
 
Ndugu, nadhani siku nyingine ukiwa unaandika upende kushirikisha ubongo maana sidhani narudia sidhani kama AUCHO ni chizi aamue kumpiga kiwiko mchezaji mwenzake...

Anza kuongelea kitendo alichofanya AJIBUU then ndio tujadili tendo la Mchezaji wa Pili.

Nb. SIPENDI UGOMVI MICHEZONI, INAPENDEZA KAMA BOLI LIKITEMBEA KWA UWEZO WA TIMU PINZANI NA SIO JANJA JANJA NA UHUNI WA KISHAMBA UWANJANI. UKIWA MAKINI NA UKIWEKA USHABIKI MBALI UTAGUNDUA JANA KUNA TIMU ILICHEZA MPIRA WA KISHAMBA UWANJANI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…