Tukio la kibanda cha mlinzi kujengwa kwa milioni 11, ni ishara kwamba viongozi wa wilaya na mkoa wamezembea au walijua

Wanakaa tu ofisini na kuchat wassap na kuulizia miradi yao.

Nani anajali??
 
Ndio tatizo la kuwa na viongozi wapenda kiki , hapo ilitakiwa wafanye uchunguzi wa fasta na wale wote waliobainika katika wizi wahukumiwe kwa mujibu wa sheria...kama faini au plea bargain au kifungo au vyote kwa pamoja.
 
Nimewahi ndiyo. Unadhanu kujenga jengo la serikali ni kama kujenga kibanda chako cha mlinzi?
Mkuu pale kilipo chuo kwanza ni Shemu ambayo hata ikijenga msingi kozi tatu kibanda hakianguki wastani kibanda kile hakizidi matofali 800 halafu kokoto tani 7 yaani kuanzia msingi hadi lenta mifuko 8cement yaani kwa kifupi wamepiga
 
Hiyo kazi inafanywa bure? Huyo mkandarasi halipi kodi? Hataki faida?
Mkuu pale kilipo chuo kwanza ni Shemu ambayo hata ikijenga msingi kozi tatu kibanda hakianguki wastani kibanda kile hakizidi matofali 800 halafu kokoto tani 7 yaani kuanzia msingi hadi lenta mifuko 8cement yaani kwa kifupi wamepiga
 
Mkandarasi amejitahidi sana. Kwa kile kibanda inazidi mil 11. Ukumbuke hapo kwenye mil 11 kuna kama 1.6mil ya VAT.

Watu wanapelekeshwa tu kama kasuku. Lakini kile kibanda kitazidi hiyo bei ya mil 11. Tuache ushabiki
Hiyo 1.6 ml. ya VAT imetokana na shilingi ngapi?
Nadhani itakua umefanya hesabu pamoja na hela iliyoibiwa
 
Mkurugenzi ahojiwe mana ujenzi huo yeye anaujuwa,mhandisi anajuwa na kama kuna kamati nayo ihojiwe.
 
Kuna haja ya kufuatilia kwa kina haya masuala ya vibanda vya Veta na sio kuwalaumu tu. Mwaka jana mwenge ulikataa kuzindua mradi wa chuo cha VETA wilaya ya Nyasa kwa sababu hiyo hiyo ya kibanda cha mlinzi kilijengwa kwa kiasi cha TZS 12 M.

Na leo tena gharama ni TZS 11 M. Nadhani kutakua na sababu za msingi vema kufanya ufuatiliaji na kuhoji wahusika na si kufanya siasa.

Mkandarasi apeleke BOQ iangaliwe kama inaakisi uhalisia wa gharama za ujenzi.

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…