Hii ni kwa wale ambao wameshiba kwa itikadi kali za kikristo na kiislamu, kiasi cha kupuuzilia kabisa uhalisia wa dini za jadi za kiafrika.
https://en.m.wikipedia.org/wiki/Mugo_wa_Kibiru Someni mmfahamu nabii Mugo Wa Kibiru aliyetabiri ujio wa mzungu Kenya miaka mingi kabla ya mkoloni kufika pwani ya Afrika mashariki. Alitabiri pia kwamba mti wa Mugumo ambao ulikuwa Thika utakapoanguka mzungu atafurushwa Kenya. Mkoloni alipanick na kuogopa utabiri huo kiasi cha kuujengea mti huo 'support' ya chuma kote kote, ili usianguke lakini haikuzuia kitu. Mti huo wa Mugumo ulipigwa na radi ukanyauka hadi ukaanguka miezi kadhaa kabla ya Kenya kupata uhuru. Sio hadithi za vijiweni hizi, kumbukumbu hii ipo kwenye vitabu vya historia ya taifa la Kenya.