Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
10,677
Reaction score
11,768
Naandika habari hii nikiwa na kumbukumbu ya kuwakumbuka marafiki zangu dogo Chiko, Wamisujo, pamoja na Topha.
Hii ilikua 2015, leo ni zaidi ya miaka 5 imepita tangu washkaji zangu hao watangulie kuzimu.

Utashangaa kwanini leo nimekaa nikawakumbuka machizi boti wangu hawa.

Leo Asbuhi nimekutana na mshikaji flani hivi ambaye tulipotea takriban miaka 5 iliyo pita, huyu mshikaji tulikuwa wote NAIROTO, tulipoteana kutokana na masahibu ninayo taka nikueleze hapo baadae.

Tulipo kutana leo kila mtu alikua akimshangaa mwenzie. Mimi ndie nilie kuwa wakwanza kumuita jina lake, alipo itika tulikumbatiana na kila mmoja kutaka kujua mwenzeke ilikua wapi baada ya tukio lile.

Kwa upande wangu nilijua mshikaji alisha kufa kwenye tukio lile.

****************************************************************************************
Nakumbuka ilikua 2015 kipindi Nanhupo madini (Ruby) yanatoka kinoma. Nakumbuka ndio mbuyuni ingali mbichi watu kila siku ni mwendo wa Dollar tu.

Mara mzungu akaongeza ulinzi porini (kukabiliana na wachimbaji) police wakawa wengi, kila askali ana mbwa, watu wakawa wanapigwa Risasi wengine wanang'atwa na mbawa.

Wachimbaji uoga ukatuingia, kila mtu akawa amepagawa, ukizingatia wengi wetu tumetoka Tanzania.

Mungu si John wala Kasim, akaonyesha makudula yake.....
Tukasiki kuna kijiji kinaitwa nairoto kuna dhahabu inatoka kwa wingi.

Kama kawaida ya wachimbaji (kuhama hama) safari zikaanza za kwenda Nairoto.

Nitarudi muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom