Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Safari iliendelea huku kila mmoja sasa anamuogopa mwenzie, kila mtu anaamini kile ni kipindu pindu.

Baada ya mwendo mrefu Wamisunjo akaanza kukosa nguvu ya kutembea.
Tumbo lilianza kumuuma na kila baada ya hatua kadhaa jamaa alikua akituomba tumngoje akajisaidie.
Baada ya mwendo mrefu Wamisunjo alishindwa kutembea nakutuambia ambia tumuache yeye hawezi kutembea.

Kwakua kila mtu alikua na uoga wa kuambukizwa, hakuna alie thubutu kumbeba, tulimuacha hapo na sisi kuendelea na safari.

Tulifika kijijini usiku kama saa 6 usiku.
Kijiji kulikua kumejaa huzuni tupu.
Nakumbuka kuna brother mmoja wa kinyakyusa (jina nimelisahau) nyumbani kwake kulikua na maiti kibao (kitu kama 19 hivi) zilikua zime tandazwa barazani.

Nyingi ya maiti hizo zilikua za watoto wa Mbeya.
Hawa walikua wanamiliki vingwendu (mashine za kusachia dhahabu)

Tulikaa pale kijijini kama week hivi, mwenye bahati ya kuwaona ndugu zao waliwaona wasio na bahati ndio basi tena

Kwa upande wangu nilipotezana na wengi, wengine walikufa, wengine ndio kama huyu mshikaji nilie kutana nae leo asbuh.

Yani ni miaka 5 ndio kwanza nakuta nae leo, mshikaji alikua kwenye misele hii hii yakwangu sema sehem nyingine.

Ndani ya week ile wengine walirudi walikotoka, wengine tuliendelea kubaki kwa kukosa nauli.

Mala zikaanza story za chini chini kutoka kwa wanakijiji wapale (nairoto)

****************************************************************************************
Wachimbaji wa mwanzoni kabisa baada ya kugundua dhahabu kwenye korongo lile, walienda mpaka kwa mwenye (chifu) wa kijiji kile na kumueleza azma yao ya kuchimba.

Chifu akawakubalia, ila kwa masharti ya kutovuta bange, sigara, pombe, wanawake wawapo polini.

Wachimbaji walikubali japo walijua kua masharti hayo kwa mchimbaji ni magumu na hayawezekani tu.

Jamaa wale walichimbaa na kila siku dhahabu ndio zilikua zikohowa tu.

Dhahabu zilitoka ile mbaya mpaka sisi wa mbali mlio ukatufikia.

Kama desturi ya mchimbaji, bila vileo (bombe, sigara, bange, wanawake) haendi.
Ikabidi washauriane kwenda kuomba kwa Mwenye, waruhusiwe kuishi maisha yao.

Walivyo fika kwa mwenye, Mwenye akakataa.
Akawaambia mizimu ya huko haitaki vitu hivyo, kwahiyo yeye haruhusu ila kama wanataka kutumia vitu hivyo ni hiari yao.

Wachimbaji walivyo rudi polini wakaanza kutumia vitu vyote.

Sigara, bange, gongo ndio vitu vya mwanzo kuingia.
Lakini kadili siku zilivyo kua zina songa ndio laana ikawa inaongeza polini.

Wanawake wakawa wengi, biashara ya ngono ikawa rasmi polini.

Polini kukawa mjini na kijijini kukageuka mstuni.
Ilifikia hatua mtu wa kijijini anakuja kutumia polini.

Baduka yakafunguliwa, bar zikawa zimezagaa.
Polini lakini mziki unagongwa utadhani uko lidas.
Mabanda ya video kama kawa.
Kiufupi poli liligeuka uwanja wa laana kwa muda mfupi tu.

Mpaka nafika mimi pale polini nilikuta kila kitu cha mjini kiko kule.

Nakuja kidogo.
 
Nisahihishe jambo moja, maranyingi huwa sipendi kuandika kutokana na kazi zangu.

Mimi sio muajiliwa, mimi ni mchimbaji, kwa hiyo maisha yangu ni yakushea na washkaji.

Some time naweza nikawa naandika jambo mala anatokea mtu (rafiki) anaanza kuniongelesha, kwa hiyo inanibidi niache kuandika nimalizane nae kwanza.

Kwahiyo munisameh kwa hilo.


************************************************************************,,*************

Kwenye safari ile nakumbuka niliongozana na mdogo wangu (Mtanzania mwenzangu pia kabila letu ni moja ) Dogo Chiko.

Tulitoka Nanhupo kuelekea nairoto kwenye dhahabu.

Tulifika Nairoto kijijini kisha pakesho yake tukaelekea polini (machimbo)

Kwanza pale kijijini tulikutana na umati wa watu usipime.

Kila mtu akiwa na shauku ya kufika polini.

Kesho yake palipo pambazuka kila mtu alikua tayari kwa safari ya kuelekea polini, me na chama langu (dogo Chiko ) tuliukanyaga kwa mguu kutokana na kutokua na nauli ya piki piki.

Nauli kwa mtu mmoja kutoka pale kijijini kwenda polini ilikua 500 quinhento miticais sawa na 25000 ishirini na tano shilling.

Tuliukanyaga mwendo wa masaa 12 kwa mguu, nakumbuka tuliingia matandani kama mida ya saa moja usiku hivi.

Lakini kwa mgodini (japo ni polini) tulikuta kama tuko mtaa wa kongo.

Watu ni wengi mno, vijana wa kiume na wakike, mabibi na mababu, mpaka watoto wa miaka 7.

Kila aina ya laana ilikua inapatikana huku, Vifo (kuuana) ubakaji, kutiana vilema yani ni kama kupakaa mafuta tu.

Pombe gani unayo itaka utaikosa, Heineken,Savana, breezer na mapombe kibao ya gharama.

Malaya kutoka kila pembe ya Africa.
Wamalawi, Watanzania, na wenyewe Mocambique.

Kiufupi huu ulikua uwanjani wa madhambi.

Nakumbuka nilifanya kazi kama week mbili tu, mala ghafla ukaibuka ugonjwa wa ajabu matandani pale.

Watu walikua wakibadilika rangi na kuharisha mwisho kifo.

Yani unaweza kukaa na mshikaji mala ghafla akaanza kubadika rangi ya macho yake, akienda kujisaidia akirudi (wengine walikua hawarudi) unamuona mwili wote ume badilika rangi kawa wanjanoo, hapo amalizi saa munamkimbia.

Halii hii ilitamba siku mbili tu, siku ya tatu matanda yote nyeupe.

Watu wote tulikimbia kurudi kijijini, sasa balaaa lilikua njiani.
Watu wengi walifia njiani, tulio tusua ni wachache sana.

Nakumbuka msafara wetu (wakurudi kijijini) ulikua na watu 8, kati ya hao wawili tuliwaacha njiani, (walifia njiani).

Moja kati ya watu hao ni Rafiki yangu kipenzi (mdogo wangu) Dogo Chiko, na mshikaji alieitwa Wamisunjo (Mateas)

Nakumbuka tulikiamsha kutoka matandani pale mida ya saa4 asbuh, tulitembea umbali mrefu, mdogo wangu Chiko akatuambia tumngoje anaenda kukata gogo (kunya)

Tulimngoja, tulikaa chini mwenye sigara aliwasha, mwenye bange lake alilipua, mwenye maji alikunywa.

Muda ulipita mara Chiko akarudi, na safari kuendelea.
Lakini kila tulipo muangalia usoni, macho yote yame badilika rangi nakua yanjano.

Tukampa maji na safari ikaendelea.

Hatukufika mbali sana, Chiko akaomba tumsubiri anakwenda tena kujisaidia.

Tilipu hii tulimngoja bila dogo kurudi, ikabidi mshikaji mmoja amfuate.
Alipo fika kule alimkuta chiko kesha kufa.
Jamaa akatuita tuje kumcheki, nikiwa mingoni mwao nilimkuta dogo amesha kauka pale alipo kaa.

Kwakua tangu tuna toka matandani tulishaambiana kua ugonjwa huu ni kipindu pindu, hivyo ukifa hakuna mtu alie thubutu kukushika.

Kwahiyo Dogo Chiko tulimuacha hapo na sisi kuendelea na safari.

Nitarudi muda si mrefu.

Horror story
 
Back
Top Bottom