Baada ya kubembelezwa saaaana huko DM kwa kutumiwa hadi wadada kuniahidi tunu basi nimebadili mawazo sasa nitasimulia habari ya safari yetu ya kutafuta mali (RUPIA) humo msitu wa NYUMBANITU
(achaneni na utani wa hapo juu) sasa twende taratibu,matukio mengi nitafupisha tu kufanya story kueleweka
Kwa wasiojua...Nyumbanitu iko Njombe wilaya ya wanging’ombe kuna mahala panaitwa Mdandu huko,ni msitu wenye habari za kutisha sana wenyeji wa huko hakuna sehemu wanapaheshimu kama hapo
Huu msitu cha kwanza uko na wanyama wasio wa kawaida kabisa na wanapatikana huko tu,kuna kuku fulani weusi tiii na midomo myekundu,hawa wanaishi humo na hakuna anayewahudumia kwa chakula wala matunzo...pia kuna ng’ombe n.k wote hawa ni kwa ajili ya matambiko ya makabila mbalimbali ya mkoa wa Njombe,zamani ikiwa wilaya ya Iringa,,haswa wabena na wakinga.
Kuna ukoo kule unaitwa wa akina Mkongwa,hawa ndio wamiliki halisi wa huo msitu na inasemekana wao wakifa huwa wanageuka kuwa nyoka na wanaishi huko kwenye huo msitu...kwa waliofika kutalii kuna wazee wako nje huwa wanatoa maelekezo ya namna ya kuingia humo na mila za humo,kama una roho nyepesi unaweza ishia tu kufika mlangoni ukarudi zako ulikotoka...unapigwa mkwara mlangoni na moja kati ya issue unapaswa kujipanga ni kwamba kama mwanamke usiende ukiwa kwenye HEDHI sababu mizimu humo ikisikia tu harufu ya damu wote mlioongozana na huyo mnapotea na hamuwezi onekana hadi wazee wa mila wafanye yao...
achana na hayo...
kilichotutia tamaa sisi kuhusu humo ndani ni story za uwepo wa RUPIA za mjerumani bwanaaa...na hakika zipo na zilikuepo,tulichogundua wale wazungu washenzi sana,hii ya kujenga hofu watu wasiende humo kwa kujiamini ndio imefanikiwa kuziacha mali zao salama mule msituni...wazungu akili nyingi sana,humo wamepandikiza uchawi mkali sana na unalindwa na hao wazee wa mila bila wao kujua wanalinda mali za watu....
ilikua 2001 mwezi wa 12 sasa tukiwa na jamaa zangu tukapanga mkakati wa kuingia mule bila kufata sheria zao za kichawi...maana ukifata protocal kuna maeneo huruhusiwi kufika na ndio inasemekana yana mali
kuna mapango makubwa inasemekana yakitumika wakati wa vita...kwa story tulizopata ni kwamba hizi mali zimefichwa kwenye masanduku makubwa yananing’inia kwenye mapango/mahandaki yaliyoko ndani kabisaaaa wanakosemaga ndio anakaa mzee mwenye msitu,ingawa kikweli huko sababu ya giza na kutisha basi kumekua makazi salama ya nyoka wakubwa wa kila aina na hao kuku wa kichawi ndio chakula chao...
tukiwa tumejipanga,plan ilikua ni kazi ya usiku mmoja tu tunamaliza tunarudi na mali na utajiri wetu...kulikua na habari kwamba soko ya rupia ni uhakika...
nikirudi naanzia sasa kwenye safari yenyewe kuingia msituni nyumbanitu
..........