Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Mkuu kwanza asante kwa kushare nasi pia kwenye hiyo story. 3. Pole kwa ulemavu kukatwa mguu. 3. kweli wanaume tunapitia mengiiii sana I see.

Usiwaone akina Ginimbi wanakufa kwenye miaka 34 akiwa kwenye kilele cha ukwasi,ukadhani ni kawaida. Wote akina Ivan. Yote hayo ni sehemu ya mapambano ya wanaume kumfukuza mdudu umasikini,tuko radhi kuhatarisha maisha yetu.

=>Swali moja mkuu. Kama umesema wale wazee wanatumika na wazungu kulinda zile mali,kwa uchawi. Kwa nini msiwatumie hao wazee kuwalainisha kwa njia yoyote,mpaka wakakubali kufanya yao,kutambika ili kufokoa hizo mali mkuu?

Mwisho hiki unachohadithia nimekisikia hata huko Mbeya maeneo ya Tukuyu eneo moja linaitwa kisiwa. Hilo eneo ni mlimani lakini maji yamejitengeneza kama bwawa kubwa juu kwenye kilima. Yale maji yana kina kirefu,japo watalii wanaogolea hata wageni wa ndani lakini kwa ya wazee walinzi wa kile kisiwa. Kuna watu nasikia wamewahi kufia hapo,wengine ni wazungu. Nasikia kwa chini kabisa kwenye hayo maji kuna mali wazungu walizihifadhi kwenye masanduku makubwa wakati wanaondoka.
hii imebak kuwa myth.mana nilishasikia huko kuna mlango una lok chin ya maji sasa duh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile kuangalia tunapopandia kwenye kitanda kwa macho yangu tena kukiwa na giza nikamwona mtu amevaa kanzu nyeupe akiwa na mandevu kibao akifunua neti like naye apande kitandani...
Aisee kelele nilizopiga hazikuwa na mfano

Dah, ni bongo tu majini yanafunua neti ili yapande kitandani[emoji23][emoji23][emoji23]. Ndio kama ile ya kwenye bongo movie jini kuangalia kushoto na kulia kabla ya kuvuka barabara
 
Nipe maujanja ya glycerine

Nipe maujanja ya glycerine
kinachofanyika ni kuchanganya mercury na hicho kilainishi dhahabu hainasi kama inavyotakiwa na unashangaa kiwango ni fixed hata kama mmekamatisha watu wenye udongo tofauti...
utashangaa wote mnanasa point moja moja tu....af mwenzenu kamanda aliekuja na mercury yake mfukoni anaondoka na yai la mbuni..
 
hahahahaahaa daah nimecheka sana we jamaa et umetumiwa hadi wadada...
Baada ya kubembelezwa saaaana huko DM kwa kutumiwa hadi wadada kuniahidi tunu basi nimebadili mawazo sasa nitasimulia habari ya safari yetu ya kutafuta mali (RUPIA) humo msitu wa NYUMBANITU

(achaneni na utani wa hapo juu) sasa twende taratibu,matukio mengi nitafupisha tu kufanya story kueleweka

Kwa wasiojua...Nyumbanitu iko Njombe wilaya ya wanging’ombe kuna mahala panaitwa Mdandu huko,ni msitu wenye habari za kutisha sana wenyeji wa huko hakuna sehemu wanapaheshimu kama hapo

Huu msitu cha kwanza uko na wanyama wasio wa kawaida kabisa na wanapatikana huko tu,kuna kuku fulani weusi tiii na midomo myekundu,hawa wanaishi humo na hakuna anayewahudumia kwa chakula wala matunzo...pia kuna ng’ombe n.k wote hawa ni kwa ajili ya matambiko ya makabila mbalimbali ya mkoa wa Njombe,zamani ikiwa wilaya ya Iringa,,haswa wabena na wakinga.

Kuna ukoo kule unaitwa wa akina Mkongwa,hawa ndio wamiliki halisi wa huo msitu na inasemekana wao wakifa huwa wanageuka kuwa nyoka na wanaishi huko kwenye huo msitu...kwa waliofika kutalii kuna wazee wako nje huwa wanatoa maelekezo ya namna ya kuingia humo na mila za humo,kama una roho nyepesi unaweza ishia tu kufika mlangoni ukarudi zako ulikotoka...unapigwa mkwara mlangoni na moja kati ya issue unapaswa kujipanga ni kwamba kama mwanamke usiende ukiwa kwenye HEDHI sababu mizimu humo ikisikia tu harufu ya damu wote mlioongozana na huyo mnapotea na hamuwezi onekana hadi wazee wa mila wafanye yao...

achana na hayo...

kilichotutia tamaa sisi kuhusu humo ndani ni story za uwepo wa RUPIA za mjerumani bwanaaa...na hakika zipo na zilikuepo,tulichogundua wale wazungu washenzi sana,hii ya kujenga hofu watu wasiende humo kwa kujiamini ndio imefanikiwa kuziacha mali zao salama mule msituni...wazungu akili nyingi sana,humo wamepandikiza uchawi mkali sana na unalindwa na hao wazee wa mila bila wao kujua wanalinda mali za watu....

ilikua 2001 mwezi wa 12 sasa tukiwa na jamaa zangu tukapanga mkakati wa kuingia mule bila kufata sheria zao za kichawi...maana ukifata protocal kuna maeneo huruhusiwi kufika na ndio inasemekana yana mali

kuna mapango makubwa inasemekana yakitumika wakati wa vita...kwa story tulizopata ni kwamba hizi mali zimefichwa kwenye masanduku makubwa yananing’inia kwenye mapango/mahandaki yaliyoko ndani kabisaaaa wanakosemaga ndio anakaa mzee mwenye msitu,ingawa kikweli huko sababu ya giza na kutisha basi kumekua makazi salama ya nyoka wakubwa wa kila aina na hao kuku wa kichawi ndio chakula chao...

tukiwa tumejipanga,plan ilikua ni kazi ya usiku mmoja tu tunamaliza tunarudi na mali na utajiri wetu...kulikua na habari kwamba soko ya rupia ni uhakika...

nikirudi naanzia sasa kwenye safari yenyewe kuingia msituni nyumbanitu

..........
 
Back
Top Bottom