Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

nitakua naandika kwa vituo tuvumiliane...nilishawahi andika thread ndefu saaana kipindi fulani simu ikazimaga ghafla kila kitu kikapotea

plan yetu kuingia mwezi wa 12 ilikua sababu ile ni miezi ya kula mavuno kwa wakazi wa Njombe wanajua huu ni msimu wa mvua na watu wengi ndio huwa wanaenda kutambika huko malori kwa magari ya kifahari...hata hao kuku huwa wengi na habari ni kwamba hata mali ndio inakua nyingi,inasemekana huwa inakuja mali na kupotea na ishara ni hao kuku kuwa wengi na kupungua

tulikua watano,1.mimi ,2.mobu (marehemu) ,huyu alikua mkinga alikua ana mishe za kupasua mbao kwa msumeno wa mkono shimoni(waliokaa njombe wanajua hii style ya kupasua mbao) 3.usungilo (marehemu) naye alikua na mishe za kupasua mbao,kwao ni bulongwa makete huko 4.mangi(alitoka mzima) huyu tulifanikiwa kutoka naye ila baada ya kutoka alikaa kama wiki moja akaanza onesha dalili za kuwa kichaa,na akawa kichaa kweli akaondokaga pale njombe hadi leo sijui habari zake (mungu amrehemu huko aliko) 5.mwaikambo (marehemu) jamaa wa mbeya alikua naye kaja kuhangaika na maisha tu Njombe.

Nirudi kwangu mimi kwanza kidogo,by then mimi nilikua mwajiriwa kiwanda cha chai,ajira siyo ya kitaalamu lakini kipato cha kuweza kuwanyanyasa hao jamaa zangu wote kiuchumi...wanangu sana,tunakutana kijiweni tunawa washkaji haswaa...kwenye hii safari mimi ndio nilikua master planer,sababu labda ya kuwa na kauli...mangi ndio alikua kama mwenye maono yote na alikua na njaa sana na hii mali...kwahiyo kupona kwangu mimi ilikua sababu sikua mstari wa mbele kuingia ndani kabisa ya pango kwenye hayo masanduku..

usiku tar 22/12 tukiwa na kila kitu cha kuingia kufungua masanduku tukaenda mdandu...fika tukiwa tushapiga mitungi yetu wanangu wako mbele mbele tukaingilia upande mwingine kabisa wa msitu ambako hata hakuna watu...hakuna kibaya hapo,tunakata majani kwa mapanga na miti midogo kupata njia...tumetembea zaidi ya masaa mawili msituni ili kuja unganisha na njia ya kule wanakoingilia watalii...na sababu tayari tulikua ndani hatukuonekana na wale wazee kule nje pamoja na walinzi wa msitu


wazee...mule ndani ni giza totoro,tochi zetu za mawe zile za kuitwa KURUNZI.,,,betri tatu tatu,tukafika tukaipata ile sasa njia ya ndani kabisa kwenda mapangoni...humu mchana kunatisha saanaaa,sasa imagine usiku inakuaje,hakuna story hapo na kama ni kuitana ni kwa sauti za chini sana,hofu ilikua kubwa na mvua sasa ikawa imeanza kupiga...baridi ni kali sana msituni

tumeendaaaa tukafika sasa kwenye mlango wa pango hapo ndio visa vilipoanzia...kule ndani usiku wanyama ndio wanakua active sababu ya ratiba labda za utalii so usiku pango ndio zinakua na fujo...tukaanza liingia pango bila uoga,mwendo kama wa dakika 30 hivi...huko ni kusikia tu sauti za wadudu na wanyama wadogo..tukamaliza hiyo zone ya zile pango za kitalii sasa tukawa kwenye mwisho ambako watu huwaga hawaruhusiwi kusogea zaidi ya hapo kwa imani kwamba watapotea hawatorudi.

na ndio habari ya vifo vya ndugu zangu watatu,kichaa cha mangi na ulemavu wangu inaanzia hapa...

ulemavu wangu wala usiwape wazo...ni kwamba niliumwa na nyoka huko nikafanikiwa kwa kudra za mungu tu kuokolewa kwa kukatwa mguu wa kushoto..

nitarudi..
Wahiwahi tuna hamu mkuu
 
Mkuu hiyo stori sio mbaya nawe ukishare nasi tukapata ya kujifunza zaidi coz zote zinahusu utafutaji katika swala zima la uchimbaji wa madini ya dhahabu. Naamini kuwa uchimbaji wa madini ya dhahabu unaendana na majini coz mdogo wangu aliokota pete ya dhahabu ina kidani chekundu juu yake baada ya dada wa kiarabu kufungua pochi yake ili atoe nauli na ile pete ikadondoka kwenye siti akiwa anaongea na konda huku akichokonoa chokonoa pochi yake. Dogo baada ya kuichukua alishuka kituo kinachofuata na break ya kwanza kwa bro wake ambaye ni mimi...
Sijui nami niseme nitaendelea Kama mkuu Kitoabu ?😂😂
Basi bhana, baada ya kunieleza nikatoka nae mpaka kwa sonara wa kihindi. Yule sonara baada ya kumuonesha tu alipandisha mashetani, eh alipoanza kupiga kelele kwa maneno ya kiarabu na kutimua mbio na watu wengine wote waliokuwepo pale jumlisha na sisi wote mbio huku nimeishikilia mkononi.
Tukakaa sehemu na mdogo wangu nikimhoji maswali huku nami nikianza kuiogopa ile pete. To cut the story short tukaenda kwa sonara mwingine Kariakoo naye ni muhindi ofisi yake ikiwa inanuka ubani tupu, alipoiangalia akatuuliza mmeipata wapi huku akitukazia macho. Hapa nikaona yasijeyakatokea yaleyale ya kule Ila imani yakupata pesa ilikuwa imenijaa nikamkazia kwa kumdanganya kuwa mama ametupa tuje kuiuza kwasababu anaumwa. Akatuangaliaa Sana huku akiiangalia Ile pete, bila kuipima wala nini akasema nawapa laki 5 na elfu alobaini. Aisee sikutegemea, mi nilijua tutauza laki ikizidi sana laki moja na nusu, Sasa kusema laki tano nikakubali fastaa...
Mkuu mimi nipo 50-50 niliookota pete 1 karibu na dukani lakini wakati nawaza kwenda kuuza kesho,nikasahau...jioni yake mwenye pete kaja. Akauliza nikamyumbisha kidogo nione. Lakini aliniambia hiyo pete huwa haipotei hata akiachaga kwenye gari hua anaipataga tu.
Akasisitiza nimpe tu mana mara ya mwisho alikua hapo nikampatia ile pete akasema hakuwa na wasi was sababu kashaidondosha mara zaidi ya 10 na hua anaipata. Niliogopa sana na sikuamini tena sio kila dhahabu inamfaa kila mtu nyingine zimechanjiwa
 
🤣🤣
Ungewahi kufanya hii biashara usingeuliza swali kama hilo...
Mimi ni Mdau wa hii biashara unaweza kutengeneza hata 600M na bd zikaisha ukatumia 300M Mia tatu nyingine ikaliwa ma shimo tena ..
Aiseeh hii kazi ni ngumu mno
 
Mike hali yako?

Pole sana mkuu,je kilichomtokea huko KJ Ni nini?!!
Jamaa alivyotoroka kambini wenzake kanikumbusha nilivyotoroka jeshini usiku Wa SAA saba na nusu nikipitia maporini yenye wanyama Wa kila aina ila nashukuru Mungu alikuwa upande Wangu nilitoboa nikafika home salama Sikh ya pili yake.
 
Back
Top Bottom