Tukio la Lissu hadi Lissu ahojiwe, tukio la Mbowe upelelezi tayari, lini Mbowe kahojiwa?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Tarehe 9 mwezi huu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mh. Mbowe alishambuliwa na kuvunjwa mguu na watu wasiojulikana, ni takriban siku 3 tu tayari polisi wamefanya uchunguzi na kuja na matokeo.

Lissu alishambuliwa tarehe11/9/2017 hadi leo karibu miaka mitatu 3, polisi wanadai wameshindwa kuendelea na upelelezi kwa vile hawajamhoji Lissu na dereva wake.

Kama wameweza kwa Mbowe bila kumhoji inashindikana nini kuendelea na upelelezi tukio la kushambuliwa Lissu hadi wamsubiri yeye na dereva wake.
 
Yani washambuliaji wa Mbowe walichagua goti tu wakambonda tap basi wakaondoka,
Inaonekana Mbowe aliwatengea kabisa mguu kwamba bondeni hapa!

Huu uhuni uwe unaishia huko chadema, msilete huku mtaani kuna watu wana akili.
 
Kutokana na taarifa ya jesh ni kuwa hakuna uthibitisho wa mtu mwingine yeyote wa kuwa Mh Mbowe alishambuliwa zaidi ya "Mbowe mwenyewe na dereva wake."
Je wamewahoji, kama hawajawahoji na kumpima mhusika kwanini wana conclude alikuwa amelewa.
 
Si mlisema polisi wanacheleweshaga uchunguzi??
Haya sasa wamewahi
Sawa wamewahi lkn kuwe na logic basi ili watu wauone ukweli, hata kama wameamua kudanganya basi watu wapate shida kuuona uongo.
 
Logic za nini??
Mtu kautwika mtindi akateleza halafu anataka kiki za VoA
 
Kutokana na taarifa ya jesh ni kuwa hakuna uthibitisho wa mtu mwingine yeyote wa kuwa Mh Mbowe alishambuliwa zaidi ya "Mbowe mwenyewe na dereva wake."

Ingelikuwa hivi ajali zinazouwa watu wote bila shuhuda uchumguzi usingefanyika

Sometime mnakuwa wapumbavu mliopitiliza.
 
Kumtetea Mwenyekiti Bado sana
Kiki yake Imebuma
Alitaka kugeuza Upuuzi wake kuwa mtaji wa siasa hovyo kabisa
Nani kamtetea, tunahoji utendaji kazi wa jeshi la polisi, mhusika mkuu alihojiwa au wamekuja na majibu yao waliyopanga?
 
Tarehe 9 mwezi huu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mh. Mbowe alishambuliwa na kuvunjwa mguu na watu wasiojulikana, ni takriban siku 3 tu tayari polisi wamefanya uchunguzi na kuja na matokeo.

Lissu alishambuliwa tarehe11/9/2017 hadi leo karibu miaka mitatu 3, polisi wanadai wameshindwa kuendelea na upelelezi kwa vile hawajamhoji Lissu na dereva wake.

Kama wameweza kwa Mbowe bila kumhoji inashindikana nini kuendelea na upelelezi tukio la kushambuliwa Lissu hadi wamsubiri yeye na dereva wake.

Wakati msemaji wa police anasema walipomhoji mbowe hospitalini akasema wakati anapigwa alipiga kerere kuomba msaada wewe ulikuwa unasikilizia matako au hukuwa na mda wa kusikiliza?

Kama hukusikia narudia kama alivyosema msemaji wa police,
Mbowe baada ya kuhojiwa alisema, alitoka kwa joyce mukya na kwenda kwake, wakati anapanda ngazi akashambuliwa na watu wasiojulikana, akapiga kerere kuomba msaada, kisha dereva wake akaja kumchukuwa na kumpeleka kwa joyce mukya , na baadae wakaenda hospitali,

wakiwa huko hospitalini ndo wakapiga sim police, na police walipofika hospitali wakamhoji ila alikukwa kalewa chakali kipombe
Sasa hapo unauliza maswali gani tena bwashee?
 
Kasome tena taarifa ya polisi, hakuna sehemu Mbowe kahojiwa na polisi, polisi wamehoji mashuhuda tu, hizo quoted quotes ni za msemaji wa polisi siyo za Mbowe.
 
Kutokana na taarifa ya jesh ni kuwa hakuna uthibitisho wa mtu mwingine yeyote wa kuwa Mh Mbowe alishambuliwa zaidi ya "Mbowe mwenyewe na dereva wake."
Mkuu nifafanulie ulichoandika maana mie sijaelewa kabisa
 
Taarifa ya madaktari ilionyesha alikua kalewa tena chakarii
Nani kakuambia kuwa mtu aliyepanga kukushambulia hata tekeleza nia yake kwa kuwa amekukuta umelewa?je ulevi pia siku hizi unaweza kumvunja mtu mguu? I thought kazi ya upelelezi ililenga kutuambia majeraha ya Mbowe yalisababishwa na nini.Anyway hii ndo Tanzania ya Magufuli
 
Back
Top Bottom