Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Nakwambia hivi, kusafirisha mwili wa mtu mmoja tu kutoka Marekani kuja Tanzania ni mshahara wa afisa mkubwa tu wa serikali ya Tanzania mwaka mzima.

We are talking about something around $15,000.Maiti ya mtu mmoja tu.

Sasa hapo ukisema usafirishe mtu mmoja kwa mwezi, useme wengine watajisafirisha wenyewe, that is $180,000

Na hapo mzozo tayari, watasema kwa nini huyu kasafirishwa na serikali, huyu kanyimwa fursa hiyo.

Hiyo kwa Marekani tu.

Unajua GDP Per Capita ya Mtanzania ni kiasi gani?

Sasa hapo serikali kwa kuwa ina limited resources inapata uamuzi.

Fedha hizo isafirishe maiti za raia au ilipe mishahara ya wafanyakazi?

Hapo serikali ikiamua ilipe mishahara ya wafanyakazi siwezi kuilaumu.

Na ndicho kinachotokea.
 
Balozi za Tanzania kwa kweli night useless kabisa. Najua tupo wengi tu ambao ni wahanga was kitelekezwa na Balozi zetu kule nje.

Halafu kibaya hakuna chochote tunaweza fanya kuhusu hili.
 
Majukumu ya Balozi si kusafirisha Maiti zinazoenda nchini kwake bwana mdogo.
Walio like post yako wote najua sio wasafiri. Na nadhani hata hapa Dar hawajawahi fiki kabisa.

Hujui unaongelea nini mkuu.
 
Kimsingi balozi za bongo hazinaga faida kwa watu wake,ukienda migration kutafuta passport unaonewa wivu sasa ndio watakuwa hao waliobebwa na Serikali tofauti na wewe ambae umekomaa na.kusafiri mwenyewe?

Pole kwa msiba
 
Ni bure kwenye midomo ya majizi ccm lakini hospital pesa kama kawaida
 
Balozi za Tanzania kwa kweli night useless kabisa. Najua tupo wengi tu ambao ni wahanga was kitelekezwa na Balozi zetu kule nje.

Halafu kibaya hakuna chochote tunaweza fanya kuhusu hili.


Mbona mnaeleweshwa humu sio kazi ya Balozi kukusaidia hela au mahitaji yeyote yatakayo gharimu hela na bado hamuelewi?

Mnawalaumu watu wasiohusika kabisa Kwa matatizo yenu
 
Kwanza chief pole sana kwa msiba.

Hivi kwani nchi za nje huwa hawaruhusu kuzika nchini mwao mtu ambaye si wa kwao ? Kama wanaruhusu kuna maana gani au faida gani ya kusafirisha maiti ? Kama hawaruhusu hii itakuwa dharura.

Maana sijawahi kuona faida ya kusafirisha maiti tena ukizingatia sisi dini yetu hairuhusu jambo hili,sababu ardhi yote ni ya Allah.
 
Walio like post yako wote najua sio wasafiri. Na nadhani hata hapa Dar hawajawahi fiki kabisa.

Hujui unaongelea nini mkuu.
Ubalozi unaweza kuwajibika ku coordinate mambo, lakini gharama za kurudisha mwili Tanzania ni jukumu la familia.

Unless mtu ni mfanyakazi wa serikali.

Serikali ina mambo mengi jamani haya mengine mjipange wenyewe, acheni ushamba na ujima wa kutegemea serikali kila kitu.

Kuna bima za wasafiri, kuna bima za maisha, kuna mifuko ya dharula ya familia, kuna benefits za waajiri, jifunzeni kuzitumia hizi si kila kitu mnataka serikali ibebe mzigo.

Serikali yenyewe balozi zikipewa hela kidogo tu mnalalamika wizi.

Ndiyo mnataka ziongezewe hela za kusafirisha maiti mpate kulalamika mabalozi wanaiba hela?

Hapo kila familia iuchukue mzigo wake yenyewe tu.
 
Wafanyakazi wa serikali wanakatwa PAYE ambayo hiyo inatumika kuandaa tena mishahara ijayo na serikali inaongeza fedha kidogo kutoka vyanzo vingine, ni kama wafanyakazi wanalipwa mishahara kutoka katika mishahara yao wenyewe.

Mapato ya migodini, bandarini nk haya ndio matumizi yake yakiwa wazi na kusimamiwa kwa umakini, yanaweza kufanya miradi ya maendeleo na bajeti nyingine kama hizo za kibalozi. Watu wametoa mifano ya ununuzi wa ndege 11 kwa cash, maana yake tatizo sio fedha bali tatizo ni vipaumbele na maamuzi tu ya nchi, pamoja na usimamizi wa fedha yenyewe ya umma.

Ni jambo linawezekana kabisa, na sio kuwa tunalia lia bali tunasema inawezekana kwa kuwa fedha ni zetu kutoka kwetu, sema hazina usimamizi mzuri, na ndio maana tunapendekeza zitumike kwenye mambo kama haya.

Kuwezekana kwake kupo hivi, Mwendazake alipenda ndege na madaraja akajenga kwa cash ikawezekana. Chukulia mfano mtoa mada angekuwa Rais leo, angefanya anavyovipenda, huenda cha kwanza angeweka bajeti ya dharula balozini na mambo yangeenda.
 
Nje ya mada,niliingia ubalozi wa Burundi Dar kajengo kakishkaji kama barbershop, sema kuna manzi mmoja anaitwa Stella ana takooooooo huyoooo.
 
Kwanza nikupe pole kwa msiba na kashkash zote mlizopitia lakini ule unaitwa wa Tanzania sio Tanganyika kwa hyo ule ubalozi unapaswa uwatreat watanzania wote equally including Zanzibar. sasa hili la kwamba hawajaplay part yao sina uhakika ngoja waje wataalam watujuze
 
Kimsingi balozi za bongo hazinaga faida kwa watu wake,ukienda migration kutafuta passport unaonewa wivu sasa ndio watakuwa hao waliobebwa na Serikali tofauti na wewe ambae umekomaa na.kusafiri mwenyewe?

Pole kwa msiba
Mkuu, naamini jina lako hapa JF la "Opportunity Cost" hujalichagua kwa bahati mbaya.

Bila shaka unaelewa concept ya "Opportunity Cost" katika uchumi.

Tuseme wewe ndiye unapanga bajeti ya serikali.

Umepewa $15,000.

Una uchaguzi wa kutoa hizo hela ziende ubalozini kusafirisha maiti, au umlipe mshahara ofisa mmoja wa serikali anayefanya kazi nyingi sana za ubalozi, ikiwamo ya kusaidia kusafirisha maiti zirudi Tanzania.

Ukimlipa mshahara huyo afisa, anaweza kufanya maarifa mengine tu vikundi vya wasamaria wema na jumuiya za Watanzania nchi za nje zikasaidia kusafirisha maiti.

Ukiweka bajeti ya kusafirisha maiti hiyo $15,000, unakosa hata afisa wa kusaini hizo hela zitoke.

Hapo utaamua vipi?

Nafikiri unaelewa concepts za finite resources na opportunity cost katika uchumi.

Hiyo hela utaamua iende wapi?
 
Muhaya anayekufa Dar naye akitaka kurudishwa kwao Kanyigo akazikwe huko kwa nauli ya ndege ya kulipiwa na serikali utakubali?

Maana na yeye ni raia na anaweza kusema Dar si kwao.

Kwa nini umpendelee Mtanzania aliye nje halafu aliyefia Dar anayetaka kuzikwa kijijini kwao umnyanyapae wakati na yeye analipa kodi?
 
Hakuna bure sajo sijui anaishi wapi! Lazima siyo Bongo, anaangalia hotuba za wasanii wetu YouTube.
Hata hayo ya kupeleka watoto India kulikuwa na misaada ya watu mule.

Everyday is Saturday............................... [emoji41]
Kwa kupenda dezo hivi bila kufikiria kanuni za kiuchumi Watanzania tutabaki kulalamika sana tu.

Hatutavuka lindi la umasikini.

Kwa kupenda kujilemaza.

Hapa kuna watu wanaweza kudai serikali ichimbe kaburi imzike ndugu yao.

Ndiyo muendelezo wa kimantiki wa hii hoja.

Kumzika mtu si kufukia udongo kwenye kaburi tu. Hata kumsafirisha ni kumzika.

Sasa ndugu wanajikosesha baraka za kusema fulani ndugu yetu tumemgharamia kumsafirisha mpaka tumemzika.

Wanataka azikwe na serikali kimsingi.

Ni jambo la fedheha sana.
 
Mbona mnaeleweshwa humu sio kazi ya Balozi kukusaidia hela au mahitaji yeyote yatakayo gharimu hela na bado hamuelewi?

Mnawalaumu watu wasiohusika kabisa Kwa matatizo yenu
Watu hawana nuance.

Ndiyo maana ni rahisi kukuta mtu analaumu serikali kila siku.

Lazima ujiulize, hiyo serikali inakosea tu?

Mimi nailaumu serikali ya Tanzania kwa kuunda taifa la watu wajinga wengi na watu walio tegemezi sana.

Nailaumu serikali kwa kutoweka mazingira mazuri ya watu kuwa na ajira na kipato.

Mpaka wanakuwa tegemezi sana kwa serikali.

Lakini siilaumu serikali kwa kukataa kusafirisha maiti za Watanzania wanaokufa nje.

Ningeweza kuilaumu serikali kama Mtanzania kuzikwa Tanzania kunamfanya mtu huyo aweze kufufuka.

Kwamba akizikwa Ethiopia si kwao, anakufa kimoja, lakini akizikwa Tanzania anakufa wiki mbili halafu anafufuka.

Hapo ningeilaumu sana serikali kwa kumkosesha mtu nafasi ya kufufuka baada ya wiki mbili.
 


Mimi huwa nasoma thread za watu wanaolilia ajira za serikali humu nabaki nashangaa sana..

Watu kama wameaminishwa lazima waajiriwe na serikali....hii mentality ya hatari mno mno..

Badala ya kijana kuwaza kufanya Jambo tofauti la kuweza hata kuajiri wengine ..unakuta Yuko bize kutembea na bahasha na kulalamika serikali haiajiri...
 
Sasa watu kama hao wakikutana na mtu kama mimi niliyejiapiza kamwe sitafanya kazi serikali ya Tanzania, naweza kuelewa kwa nini inakuwa shida kuelewana.
 
Walirudishwa bila huruma kwa gharama za nan???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…