Marekani wana sera za kibaguzi mkuu hasa Afrika baada ya watu wengi kupata uraia wao wakaweka baadhi ya kanuni za kutotoa misaada kwenye balozi zao zaidi ya waliopoteza passport nilipokua Hong Kong mmarekani mmoja aliruka nyoka aliishiwa kila kitu alienda ubalozini kwao wakampa hela ya siku tano sikushangaa kwa sababu miaka ya 2000 nilipokua nabeba box Cape Town alikuwepo mmarekani mmoja nae full nyoka akipata mshahara wake hapo debeers na analala long street au camps bay nje na gari yake ikaonekana ni hatari sana ubalozi ndio ulilazimisha yule jamaa arudi kwa kukata tiketi na kila kitu ingawaje alikuja kulipwa stahiki zake na debeers akiwa USA hapo ni Cape Stad tuu mkuu mimi nilibahatika kuanza mambo ya safari na kazi nje miaka ya nyuma nikiwa na umri mdogo nimeona wamerekani wakiwasaidia raia wao sio kwa kusikia ..
Mara nyingi inakuwa ni michongo ya jitihada binafsi za wafanyakazi wa ubalozi wanasaidia watu.
Hata Bongo Andy alivyokuwa anasafiri kabla hajatulia alikuwa anaharibu sana South hapo anakimbilia ubalozini, watu wanamfanyia heshima jina la baba wa Taifa wanampa nauli ya kurudi Bongo.Lakini si kitu kilichopo officially.
Baharia usawa huu kutegemea serikali michosho, serikali zenyewe bajeti ndogo, uende kusafirisha maiti ya mtu mmoja kutoka unyamwezini $15,000. Huo mshahara wa ofisa mkubwa sana wa serikali kwa mwaka mzima Tanzania.
Watu wanunue bima tu, serikali ya Tanzania mimi nailaumu kwa kufuga umasikini unaofanya watu waitegemee sana.
Serikali inatakiwa kuangalia mifumo, watu wapate ajira, wakipatwa na msiba kuchangishana hizi $100 mpaka $1,000 isiwe tabu sana.
Watu wangekuwa na uwezo huo hata usingesikia wanailaumu serikali kushindwa kurudisha maiti Bongo.
Lakini kwa sasa serikali imefanya umasikini kama jadi Tanzania, na imetengeneza wananchi tegemezi sana.
Kuna demu mmoja mnyamwezi alikuwa ananipa story alikuwa anatalii kuzunguka sehemu mbalimbali, akaishiwa hela Cairo.
Kitu cha kwanza alichofanya alimpigia simu Mama yake, kwao wako safi. Mama yake alikuwa New Jersey akamtumia hela.
Yani hakuwa hata na wazo la kwenda ubalozini, aliona mambo kama hayo unayamaliza kifamilia tu.
Lakini ndiyo hivyo, nchi yake ilishaweka uchumi mzuri, familia yake ilikuwa na kipato.
Alikuwa ana option ya kumaliza mambo kifamilia.
Sisi upande huo pangu pakavu tia mchuzi, serikali haijaweka mifumo mizuri, watu hawana ajira, lazima watu waililie serikali kuanzia mambo ya serikali kweli mpaka mtu akishindwa kupenga makamasi atailaumu serikali.