Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Huyu Mtanzania alikuwa safarini peke yake, Ethiopia haikuwa destination yake , alishushwa kwa dharura ya kuumwa ghafla na umauti ukamfika huko.Sisi hatuna familia wala jamaa kule.
Kama balozi yupo ,unadhani nanai awajibike kutowa msaada?
kama hawalipi gharama zote , hata kuchangia sehemu ya Gharama ubalozi hauwezi ?
Ili tujue Zanzibar mnatebmngwa badi tupe mfano wa MTU wa bars aliefia nje ya nchi halafu serikali ikawajibika kutoa nauli na kila kitu,

Msipende sana kulalamika kama watoto kwa mama wa kambo,

Sio lazima Serikali iwajibike kwani yenyewe ndio imehusika na kifo?
 
Kama huna figures hayo malalamiko mengine ni ulalamishi ambao hauko katika msingi makini.

Kama kuna Watanzania 100 tu kwa mwaka wanafariki Marekani nchi moja tu, kitu ambacho si kigumu kwa sababu mimi katika group moja tu napata msiba kama mmoja kila mwezi, na mimi sipati misiba yote, na ikiwa kusafirisha mwili mmoja wastani ni kama $15,000, hapo tayari unaongelea $1,500,000 kwa watu 100.

Dola milioni moja na nusu.Kusafirisha maiti tu.

Hiyo bajeti ya kusafirisha wanaofariki Marekani tu, hujagusa nchi nyingine, hujagusa kodi ya ofisi ya ubalozi, hujagusa kodi ya nyumba ya balozi, hujagusa mishahara ya wafanyakazi, hujagusa kusaidia wanaoumwa.

Sawa Mkuu ila rate ya vifo hivyo 100 vinatisha mkuu yaani hapo ina maana kila baada ya siku nne Mtz m1 anafariki USA....Kama ndio hivyo basi panatisha....Kwenye community kupoteza mtu m1 kila baada ya siku 4 ni hatari.

Ni sawa na vyuoni mkianza mwaka wa kwanza hadi mnamaliza wanaweza wakafariki watu wawili au watatu ndani ya miaka hiyo minne au mitano ya kozi hadi mnamaliza.
 
Asikwambie mtu wazanzibar wana hutu sana ,ukiona mzanzibar ana roho mbaya basi huyo mzanzibar wa magomeni au ilala.

Wabara wana umimi sana ,sasa serikali inashindwa vipi kugharamikia tukio kama hilo? JMT hawana funds za dharura?
Wana utu ilihali mlishasema Serikali yenu iliwahi kuwagharamia wanafunzi wenu,
Ikawaacha wa bara wakarudi makwao huo ndio muungano? Au utu?
 
Wengi watashangazwa na na mada ya hapo juu.

Taratibu fuatilia

Tare 21/04/2021 siku ya juma tano, Dada yangu Fatma Said alifariki dunia Nchini Ethiopia akitokea Dubai kuja Zanzibar (Tanzania).
Akiwa ndani ya ndege 'Fly Dubai' aliumwa ghafla na kuilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura nchini Ethiopia ikiwa nio kiwanja cha karibu kwa walipokuwa.

Tukio hili la kumshusha pale ni sehemu ya taibu za ndege inapotiokea dharura. Mgonwa alipelekwa Hospitali na Kufarikiduni muda mchache baada ya kufika hospitali.

Yamkini serikali ya Ethiopia iliarifu ofisi ya Kibalozi ya TANZANIA kwa hatua stahiki.

Wana familia nao tulipopata habari tuliwasiliana na Balozi ili kujua hatua gani zifanywe ili Mwili wa marehemu urejeshwe Nyumbani kwa mazishi. Balozi wa Tanzania alianza kutudanganya na kutupiga danadana eti akidai kuwa hana FUND za kugharamia matukio ya aina hii.

Hatimae ilitubidi wanafamilia tulipishwe Gharama za Hospitali, Kusafirisha mwili na kila kilichohusu kusafirishwa kwa mwili husika.

Mwili ulifika jana tarehe 27/04/2021 kwa ndege ya Cargo ya Ethiopia Air Line.

Nilianza kujiuliza NINI FAIDA YA KUWA NA BALOZI NCHINI ETHIOPIA? Lakini mara nikakumbuka kuwa kama Zanzibar ingelikuwa na Ubalozi wake kule tungelipata matokeo tofauti?

Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Nimeyasema haya nikiwa na Uchungu mkubwa wa kuona kuwa MUUNGANO WETU umekuwa kikwazo kwa raia wa Zanzibar .HILI NALO NI MOJA YA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO kwenye mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. We are not treted equaly.

Namuoba Waziri wa mambo ya nje Ahusike na tukio hili la Ethiopia kwani Ubalozi wa TZ haukusaidia lolote kifedha katika jambo hi la Marehemu.

Isije ikatumwa Invoice ya kuonesha kuwa Ubalozi ulitumia fedha,itakuwa ni Upigaji wa fedha za serikali.

Nawakilisha.
Nani kamtuma Marehemu Dubai? Kila Msafiri lazima ujikatie bima, hilo unalijua wewe yakhe? Acha kupenda vya bure, wajibika binafsi
 
Sawa Mkuu ila rate ya vifo hivyo 100 vinatisha mkuu yaani hapo ina maana kila baada ya siku nne Mtz m1 anafariki USA....Kama ndio hivyo basi panatisha....Kwenye community kupoteza mtu m1 kila baada ya siku 4 ni hatari.

Ni sawa na vyuoni mkianza mwaka wa kwanza hadi mnamaliza wanaweza wakafariki watu wawili au watatu ndani ya miaka hiyo minne au mitano ya kozi hadi mnamaliza.
Kipindi hiki cha Covid pandemic watu wamefariki sana, na mpaka ule ubishi wa kutaka kusafirisha maiti kila msiba naona unaanza kuisha, tunaanza kuzika watu huku Marekani naona.

Hiyo namba hata ukiigawanya mara nne kusema nimeiweka juu sana, iwe mtu anafariki kila wiki mbili, bado ni mzigo mzito sana kwa ubalozi wetu, ndiyo maana Wanyamwezi tunajiongeza kuchangiana na kukumbushana kukata bima za maisha tu.

Ukienda Ubalozi wa Tanzania US kuomba msaada wa kurudishiwa maiti nyumbani na ubalozi watakuuliza wewe umetoka sehemu gani Marekani na huko hakuna jumuiya ya Watanzania unaojuana nao wakuchangie?

Ubalozi kuingia gharama hizi si kitu practical, utataka balozi ziuze majengo kwa kutaka kusafirisha maiti kuzirudisha Bongo.

Tunapotaka serikali itusaidie tuwe na moyo wa kufikiria wengine pia, hela za serikali zina kazi nyingi sana.

Kuna wanafunzi wanasomeshwa na hela za serikali, kuna mishahara watu wanalipwa na serikali, kuna madawa yananunuliwa na serikali.

Msifikiri ni vitu rahisi tu.Balozi zenyewe zimechacha jamani siyo kwamba nchi yetu ina bajeti za kutosha kuhudumia kila mtu na shangazi yake.

Haya mambo mengine tujiongeze, tukibweteka sana tutataka mpaka mahari kwenye kuoa tulipiwe na serikali.
 
Si suala la kutowezekana.

Kuna nchi zina uwezo mkubwa lakini hazirudishi maiti za raia wao nyumbani, unless wawe wafanyakazi wa serikali kama wanajeshi.

Kwa sababu raia inawabidi wawe na "personal responsibility".

Ukianza kupeleka hela za kurudisha raia ubalozini ndiyo mwanzo wa kuleta mzozo wa pesa kuliwa, kama zimeliwa kweli au kwa figisu tu za kusingiziana.

Ndiyo maana wenzetu wananunua bima, wanasoma small prints za tiketi, wanajiwekea akiba za dharula.

Sisi tunataka kila kitu ifanye serikali, hatuna personal responsibility.

Marekani ni nchi yenye utajiri mkubwa sana. Lakini ukiacha wafanyakazi wa serikali kama wanajeshi, raia wa kawaida akifariki nje ni jukumu la familia kusafirisha mwili. Si jukumu la serikali.

Serikali ilishaweka mifumo huko.Ilishaweka mifumo ya bima, ilishaweka mifumo ya atu kuwa na ajira na biashara.

Kwa kweli Wamarekani wengi ukiwambia mwili usafirishwe na serikali wanaweza kuona ni jambo la aibu.Mwili usafirishwe na serikali kwani huyu mtu hana ndugu? Yani wanaona hata kama huduma ya serikali ipo, hawaiamini, wanaona wao ndio wanaweza kupanga vizuri kumrudisha ndugu yao. Wtapanga kwa mapenzi ya ndugu, ndugu yao kurudishwa na serikali ni kama kazikwa na serikali, bila mapenzi ya ndugu.

Sasa sisi wengi tunapenda dezo.

Mimi nitailaumuserikali kwa kutoweka misingi ya uchumi mzuri.Wtu wamepigika, mpaka familia zinashindwa kujipanga kumrudisha ndugu yao.

Hapo nitailaumu serikali sana tu.

Lakini, kwenye gharama za kurudisha maiti, ni jambo la aibu maiti ya mtu ambayesi mfanyakazi a serikali kurudishwa na serikali. Pia ni jambo ambalo serikali yetu haiwezi kumudu.

Tujifunze kujitegemea, kukata bima, kuweka akiba, kuwa na emergency funds, sio kuishia kuitegemea serikali tu.
SA ni nchi ambayo haina sera za kimasikini kama hiyo ya sijui nchi tajiri hazifanyi hivyo wao wanafanya...sio tuu maiti hata akiwa mzima kapata matatizo sehemu anasaidiwa sisi umasikini upo kwenye damu kwa hiyo ni ngumu kufanya vitu kama hivi na ubinafsi pia unachangia ...
 
Nilikwenda ubalozi wa Marekani wa zamani kabla haujapigwa bomu. Pale ubalozini waliweka bango kwa raia wa Marekani kwamba ubalozi huu hautoi msaada wa hela kwa watu wenye matatizo ya hela.

Inaonekana kuna raia wengi wa Marekani walikuwa wanaishiwa hela wanaenda kuomba hela ubalozini kwao, mpaka ubalozi ukaamua kuweka bango mlangoni kama raia wa Marekani kaishiwa hela hata asijisumbue kuomba msaada wa hela ubalozini.

Sasa Marekani ni nchi masikini?
 
Marekani wana sera za kibaguzi mkuu hasa Afrika baada ya watu wengi kupata uraia wao wakaweka baadhi ya kanuni za kutotoa misaada kwenye balozi zao zaidi ya waliopoteza passport nilipokua Hong Kong mmarekani mmoja aliruka nyoka aliishiwa kila kitu alienda ubalozini kwao wakampa hela ya siku tano sikushangaa kwa sababu miaka ya 2000 nilipokua nabeba box Cape Town alikuwepo mmarekani mmoja nae full nyoka akipata mshahara wake hapo debeers na analala long street au camps bay nje na gari yake ikaonekana ni hatari sana ubalozi ndio ulilazimisha yule jamaa arudi kwa kukata tiketi na kila kitu ingawaje alikuja kulipwa stahiki zake na debeers akiwa USA hapo ni Cape Stad tuu mkuu mimi nilibahatika kuanza mambo ya safari na kazi nje miaka ya nyuma nikiwa na umri mdogo nimeona wamerekani wakiwasaidia raia wao sio kwa kusikia ..
 
Sijawahi kusikia ubalozi wa Tanzania ukisafirisha maiti ya mtanzania, iwe U.S. iwe U.K. iwe India iwe China iwe Japan, na wanakufa Watanganyika kwa Wazanzibar, nachojua ndugu, jamaa na marafiki na wenye mapenzi mema hujichanga na kugharamikia.
Sijui labda awe marehemu ni mtumishi wa serikali aliyetumwa kazi kiserikali huko ughaibuni afie huko, ndiyo serikali litachukua jukumu hili.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Marekani wana sera za kibaguzi mkuu hasa Afrika baada ya watu wengi kupata uraia wao wakaweka baadhi ya kanuni za kutotoa misaada kwenye balozi zao zaidi ya waliopoteza passport nilipokua Hong Kong mmarekani mmoja aliruka nyoka aliishiwa kila kitu alienda ubalozini kwao wakampa hela ya siku tano sikushangaa kwa sababu miaka ya 2000 nilipokua nabeba box Cape Town alikuwepo mmarekani mmoja nae full nyoka akipata mshahara wake hapo debeers na analala long street au camps bay nje na gari yake ikaonekana ni hatari sana ubalozi ndio ulilazimisha yule jamaa arudi kwa kukata tiketi na kila kitu ingawaje alikuja kulipwa stahiki zake na debeers akiwa USA hapo ni Cape Stad tuu mkuu mimi nilibahatika kuanza mambo ya safari na kazi nje miaka ya nyuma nikiwa na umri mdogo nimeona wamerekani wakiwasaidia raia wao sio kwa kusikia ..
Mara nyingi inakuwa ni michongo ya jitihada binafsi za wafanyakazi wa ubalozi wanasaidia watu.

Hata Bongo Andy alivyokuwa anasafiri kabla hajatulia alikuwa anaharibu sana South hapo anakimbilia ubalozini, watu wanamfanyia heshima jina la baba wa Taifa wanampa nauli ya kurudi Bongo.Lakini si kitu kilichopo officially.

Baharia usawa huu kutegemea serikali michosho, serikali zenyewe bajeti ndogo, uende kusafirisha maiti ya mtu mmoja kutoka unyamwezini $15,000. Huo mshahara wa ofisa mkubwa sana wa serikali kwa mwaka mzima Tanzania.

Watu wanunue bima tu, serikali ya Tanzania mimi nailaumu kwa kufuga umasikini unaofanya watu waitegemee sana.

Serikali inatakiwa kuangalia mifumo, watu wapate ajira, wakipatwa na msiba kuchangishana hizi $100 mpaka $1,000 isiwe tabu sana.

Watu wangekuwa na uwezo huo hata usingesikia wanailaumu serikali kushindwa kurudisha maiti Bongo.

Lakini kwa sasa serikali imefanya umasikini kama jadi Tanzania, na imetengeneza wananchi tegemezi sana.

Kuna demu mmoja mnyamwezi alikuwa ananipa story alikuwa anatalii kuzunguka sehemu mbalimbali, akaishiwa hela Cairo.

Kitu cha kwanza alichofanya alimpigia simu Mama yake, kwao wako safi. Mama yake alikuwa New Jersey akamtumia hela.

Yani hakuwa hata na wazo la kwenda ubalozini, aliona mambo kama hayo unayamaliza kifamilia tu.

Lakini ndiyo hivyo, nchi yake ilishaweka uchumi mzuri, familia yake ilikuwa na kipato.

Alikuwa ana option ya kumaliza mambo kifamilia.

Sisi upande huo pangu pakavu tia mchuzi, serikali haijaweka mifumo mizuri, watu hawana ajira, lazima watu waililie serikali kuanzia mambo ya serikali kweli mpaka mtu akishindwa kupenga makamasi atailaumu serikali.
 
Sawa Mkuu ila rate ya vifo hivyo 100 vinatisha mkuu yaani hapo ina maana kila baada ya siku nne Mtz m1 anafariki USA....Kama ndio hivyo basi panatisha....Kwenye community kupoteza mtu m1 kila baada ya siku 4 ni hatari.

Ni sawa na vyuoni mkianza mwaka wa kwanza hadi mnamaliza wanaweza wakafariki watu wawili au watatu ndani ya miaka hiyo minne au mitano ya kozi hadi mnamaliza.
Mkuu sijui katuonaje yaani kila baada ya siku tano msiba wa Mtanzania USA? daah kazi ipo kwa kweli wacha niishie hapa...
 
Huyu Mtanzania alikuwa safarini peke yake, Ethiopia haikuwa destination yake , alishushwa kwa dharura ya kuumwa ghafla na umauti ukamfika huko.Sisi hatuna familia wala jamaa kule.
Kama balozi yupo ,unadhani nanai awajibike kutowa msaada?
kama hawalipi gharama zote , hata kuchangia sehemu ya Gharama ubalozi hauwezi ?
Poleni kwa kufiwa lakini, utaratibu ni huo. Balozi hazina mafungu ya namna hii, na huwezi kusikia eti balozi wameandika matumizi kuchangia kusafirisha maiti ya mtanzania.
Kama balozi, hawajapewa hilo fungu watakupa hela wakiitoa wapi??
Watu wanaishi kigumu hata hizo nchi za watu, tena huko Ethiopia, hakuna hata ujasiliamali ni mishahara tu.

Everyday is Saturday..............................😎
 
Mwaka jana Nchiya Oman Illeta Ndege Kuchukua raia wake wote waliokwama kwa sababu ya Corona na kuwarudisha Oman Free of charge.
Hii ndio kujali kwa nchi na raia wake.
Je. Fedha za kugharamia ndege hiyo zillitolewa na ubalozi wa Oman hapa nchini?
===
Pole sana ndugu yangu kwa msiba wa mtanzania mwenzetu.
 
Sasa wewe ukitaka privilege hii kwa ndugu yako kwa nini wengine wote wasidai hivyo hivyo?

Wewe una u specil gani kuzidi wengine?
Hapa Tanzania matibabu ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 6 ni bure katika hospitali za serikali. Vivyo hivyo kwa matibabu ya wazee wa kuanzia umri wa miaka 60. Lakini sio wazazi wote wanaowapeleka watoto wao kupata matibabu ya bure hospitali za umma, huwapeleka hospitali za binafsi na kulipa gharama za matibabu kwa sababu wazijuazo wao, vivyo hivyo kwa matibabu ya wazee, sio wote hutumia hospitali za serikali.

Alichomaanisha Isanga family ni kuwa kuwepo na bajeti ya mambo kama haya kwa balozi zetu, uwepo wake haumaanishi kuwa wote wataokufa wataitumia. Ni kama ulivyosema wewe, wengine wataamua kuzikwa hukohuko na wengine watajisafirisha wenyewe nk ipo hivyo kiuhalisia, watu wote hatufanani maamuzi. Sasa bajeti iwepo halafu kutosha au kutotosha itakuwa jambo lingine baadae. Zamani kabla ya uwepo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Serikali ilikuwa inatoa fedha kusafirisha wagonjwa wa moyo India, ni mambo yanayowezekana kama nchi tukiamua kuyafanya.
 
Mara nyingi inakuwa ni michongo ya jitihada binafsi za wafanyakazi wa ubalozi wanasaidia watu.

Hata Bongo Andy alivyokuwa anasafiri kabla hajatulia alikuwa anaharibu sana South hapo anakimbilia ubalozini, watu wanamfanyia heshima jina la baba wa Taifa wanampa nauli ya kurudi Bongo.Lakini si kitu kilichopo officially.

Baharia usawa huu kutegemea serikali michosho, serikali zenyewe bajeti ndogo, uende kusafirisha maiti ya mtu mmoja kutoka unyamwezini $15,000. Huo mshahara wa ofisa mkubwa sana wa serikali kwa mwaka mzima Tanzania.

Watu wanunue bima tu, serikali ya Tanzania mimi nailaumu kwa kufuga umasikini unaofanya watu waitegemee sana.

Serikali inatakiwa kuangalia mifumo, watu wapate ajira, wakipatwa na msiba kuchangishana hizi $100 mpaka $1,000 isiwe tabu sana.

Watu wangekuwa na uwezo huo hata usingesikia wanailaumu serikali kushindwa kurudisha maiti Bongo.

Lakini kwa sasa serikali imefanya umasikini kama jadi Tanzania, na imetengeneza wananchi tegemezi sana.
Mtaji wa serikali hii ya CCM kuendelea kubakia madarakani ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa maskini, hawana nia ya dhati ya kuufuta umaskini.
Ni kupiga politiki na kuja na makaratasi yenye maneno mengi, mipango mingi lengo ni kula fedha za wahisani kwenye posho za vikao na kujilipa outrageously huko bungeni.

Huu umaskini hawana nia ya kuufuta, wanajua

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mkuu sijui katuonaje yaani kila baada ya siku tano msiba wa Mtanzania USA? daah kazi ipo kwa kweli wacha niishie hapa...
Mimi kwenye kundi moja tu napata msiba takribani mmoja kila mwezi, na mimi sijuani na Watanzania wote.

Nimeendeleza mjadala kwa kusema kuwa hiyo namba hata ukiigawanya mara nne useme anafariki mtu mmoja kila baada ya wiki mbili bado gharama zitakuwa kubwa mno kwa ubalozi.

Na hiyo nchi moja tu.

Umeona nilipoandika hivyo?
 
Wengi watashangazwa na na mada ya hapo juu.

Taratibu fuatilia

Tare 21/04/2021 siku ya juma tano, Dada yangu Fatma Said alifariki dunia Nchini Ethiopia akitokea Dubai kuja Zanzibar (Tanzania).
Akiwa ndani ya ndege 'Fly Dubai' aliumwa ghafla na kuilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura nchini Ethiopia ikiwa nio kiwanja cha karibu kwa walipokuwa.

Tukio hili la kumshusha pale ni sehemu ya taibu za ndege inapotiokea dharura. Mgonwa alipelekwa Hospitali na Kufarikiduni muda mchache baada ya kufika hospitali.

Yamkini serikali ya Ethiopia iliarifu ofisi ya Kibalozi ya TANZANIA kwa hatua stahiki.

Wana familia nao tulipopata habari tuliwasiliana na Balozi ili kujua hatua gani zifanywe ili Mwili wa marehemu urejeshwe Nyumbani kwa mazishi. Balozi wa Tanzania alianza kutudanganya na kutupiga danadana eti akidai kuwa hana FUND za kugharamia matukio ya aina hii.

Hatimae ilitubidi wanafamilia tulipishwe Gharama za Hospitali, Kusafirisha mwili na kila kilichohusu kusafirishwa kwa mwili husika.

Mwili ulifika jana tarehe 27/04/2021 kwa ndege ya Cargo ya Ethiopia Air Line.

Nilianza kujiuliza NINI FAIDA YA KUWA NA BALOZI NCHINI ETHIOPIA? Lakini mara nikakumbuka kuwa kama Zanzibar ingelikuwa na Ubalozi wake kule tungelipata matokeo tofauti?

Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Nimeyasema haya nikiwa na Uchungu mkubwa wa kuona kuwa MUUNGANO WETU umekuwa kikwazo kwa raia wa Zanzibar .HILI NALO NI MOJA YA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO kwenye mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. We are not treted equaly.

Namuoba Waziri wa mambo ya nje Ahusike na tukio hili la Ethiopia kwani Ubalozi wa TZ haukusaidia lolote kifedha katika jambo hi la Marehemu.

Isije ikatumwa Invoice ya kuonesha kuwa Ubalozi ulitumia fedha,itakuwa ni Upigaji wa fedha za serikali.

Nawakilisha.
Nakushauri mwandikie waziri wa mambo ya nje barua rasmi kuhusu jambo hili
 
Back
Top Bottom