Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ni wa kwenu. Atoe amri tu majeshi unayoyasema yataondoka kwenu. Rais wenu alikuwa waziri wa ulinzi miaka mingi tu kwa hiyo bila shaka anajua kila kitu kuhusu majeshi. Ashirikiane tu na Rais wa JMT kuondoa hayo majeshi.
Vizuri zaidi, waanzishe mchakato wa kujitoa katika Muungano. Wafanye referendum ya hatma ya Muungano pande zote mbili za Muungano halafu uone nani atasema uvunjwe. Machogo hatuna habari na Zanziba na Muungano ukivunjika hautaleta tofauti yeyote katika maisha yetu. Nyinyi ambao mnaishi kwetu bila shida yeyote, makuja mtakavyo, ndugu zenu wamejaa Sharif Shamba, mnatumia hospitali zetu, mnatumia shule zetu mpaka vyuo vikuu, mnamiliki mashamba, mnaajiriwa sehemu yeyote mnayotaka, mnagombea uchaguzi ngazi yeyote mnayotaka, mnalindwa na wanajeshi wetu, mnapata umeme wa dezo, mnaolewa, tunawalisha, hizo balozi mnazopigia makelele ni sisi tunaozilipia n.k.
Vunjeni Muungano mtuache tupumue maana mmemukuwa kama viroboto. Nafasi ndio hii. Nendeni muone kama tutalia. Kwa taarifa yako machogo wengi hawajui hata Unguja iko wapi! Msitusumbue. Hamlipi kitu lakini mnataka mpendelewe kila mahali. Watu kama nyinyi ndio mnao waharibia wenzenu tunaoishi nao vizuri tu Kigamboni.
Huyo unaemuita Baba yetu ndie aliyempa hifadhi Sultani wenu wakati mnataka kumchinja. Ndie aliyewahifadhi wakina Babu wakati mnataka kuwanyonga. Alifanya hivyo baada ya kuona mlivyowafanya wakina Mdungi. Ndie aliyekataa kugeuza nchi yenu kuwa mkoa. Lakini sishangai maana watu kama nyie hampendeki. Kama wenyewe kwa wenyewe hampendani, itakuwa sisi machogo!
Amandla...