Tukio la Mtoto kufungwa na mnyororo darasani, Polisi yawashikilia Mwalimu Mkuu na Mlinzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
​

Baada ya kusambaa kwa video ikumuonesha Mwanafunzi amefungwa mnyororo darasani, kama hukuiona ipo hapa ~ Mwalimu Mkuu amfungia mwanafunzi darasani kwa Mnyororo, Jeshi la Polisi limechukua hatua.

MWALIMU MKUU, MLINZI WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA UKATILI
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu wawili ambao ni Mussa Luambano (50) mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ngarenaro Jijini Arusha na Olais Mollel (33) mlinzi wa Shule hiyo kwa tuhuma za ukatili dhidi ya mtoto (13) mwanafunzi wa darasa la saba (jina limehifadhiwa).

Watuhumiwa hao kwa kutumia mnyororo, tarehe 01.09.2025 waliufunga mguu wa mwanafunzi huyo kwenye dawati na kisha kumfungia ndani ya chumba cha darasa kwa madai ya kuwa ni mtoro.

Aidha, tunaendelea kukamilisha upelelezi wa utakapokamilika taratibu nyingine za kisheria zitafuata. tukio hili, pindi Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linatoa wito kwa wananchi kuendelea kufichua matukio ya uhalifu katika jamii ili tuendelee kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria dhidi ya wote watakaobainika.

IMETOLEWA NA:-
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA ARUSHA.
 
Wameanza kazi ya Magereza!
 
Sasa huyo mlinzi aliyetoa taarifa akitoka kwenye hiyo kesi ajira hana, pia huyo mwalimu huenda akatenguliwa nafasi yake na kubaki mwalimu wa notisi.
Kabakiza Miaka 5astaafu,anafanya ujinga!
 
Reactions: K11
Picha mjongeo ya raia inashughulikiwa haraka,ila picha mjongeo ZaO,tunaambiwa labda za kutengeneza.Which is which?
 
Kabakiza Miaka 5astaafu,anafanya ujinga!
Matukio hayo ni madogo, hawezi fungwa wala kufukuzwa kazi.
Alichoshindwa ni kutoa adhabu ambayo iko kinyume na miongozo ya adhabu Kwa wanafunzi.

Kisheria mwalimu mkuu anaruhusiwa kutoa adhabu sitahiki iwe ya viboko, shamba, usafi et al inayozingatia kanuni na taratibu.

Tunaendelea kuwaasa walimu wajiepushe na matatizo ya kujitakia.
Haiwezekani mwalimu awe na uchungu kuliko mzazi/mlezi wa mtoto husika.

Kwa kizazi cha sasa ninawashauri walimu waachane na malezi ya watoto watukutu Kwa kusimamia nidhamu bali wajikite kufundisha watoto wenye utayari wa kusoma pekee.

Suala la viboko sijui adhabu flani achaneni navyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…