Tukio linalotegemewa tega masikio sasa

Tukio linalotegemewa tega masikio sasa

Ni mbabe sana,dharau,mtu wa visasi,hapendi kuwa chini ya mtu,fitina,wivu,mchonganishi na kibaya elimu yake ya masters degree haimsaidii.Sakata lake wakati akiwa DC Singida na aliyekuwa mkuu wa polisi RPC S.Dau linathibitisha hilo.Ikumbukwe kuwa baada ya Singida aliamishiwa Tabora kuwa RC na baada ya muda mfupi kamanda Dau nae akaamishiwa Tabora kama RPC so akamkuta kandoro akiwa ndo bosi wa Tabora.Ilimchukua Dau miezi michache tu kuhamishiwa Reli kama kamanda wa Reli baada ya Kandoro kumkataa Tabora kutokana na visa vyao vya Singida.Alimwandikia mahita kuwa hamtaki Dau kwenye mkoa wake.

Majita umetoa insight nzuri sana .Huyu jamaa yaani kandoro ana Masters ya kitu gani ? Mbona mie namuona mtupu sana ? Kiburi yeah anacho he can tell huhitaji kuuliza .Now kwa maana nyingine Pinda ameshapata msaada kama anautaka wa kumuondoa ama umwacha Kandoro.Lakini kwa kuwa Msemaji wa mwisho ni mzee wa Pwani mwenziwe nadhani kandoro kama Makamba ana mambo ya ajabu lakini naweza nasema linabaki kuwa chaguo la Mkwere !!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lunyungu,

Tumefahamiana kwa siku nyingi mkuu katika masuala ya maisha kama haya tuweke tofauti pembeni pls kama una access huko penyeza jina langu I would prefer U-RC lakini kwa kuanzia hata U-DC sio mbaya

Kindly do the needful nakuamini

Kwi kwi kwi

Masatu you aim high...........

All the best mkuu

Ukifanikiwa (Jamaa akikuunganishia), tukumbuke katika ufalme wako.
 
Lizy nimepata tetesi kwamba JK na mshikaji wake Upinde wana nia ya kuongoza wanawake kwua wakuu wa Mikoa so kaa mkao wa kuitwa kwenye ufalme
 
Mwakajana kagame alipunguza wakuu wa mikoa kutoka 9 hadi 4. Tujiulize mwingereza alikuwa na ma-PC 8 tena wakisafiri kwa 109 na simu za kukoroga na ufanisi wao ulikuwa mkubwa.

leo hii tuna emails, online conference, gps na ma-vx tunahaja yakuwa na wakuu wa mikoa 21? kwani wakiwa 8 tija haitapatikana? kwani tunazo brigade ngapi za jeshi na ufanisi wake uko palepale! ndo maana akina ditto walitoroka kazini na kupata mabalaa.

Sidhani kama Pinda nimtu makini tangu awe waziri mkuu anazurura tu mara msasani kwa mama nyerere, sumbawanga wikinzima akitoka huko ataenda butiama. Hivi kweli kasi ya ujenzi wa shule aliyokuwa nayo Lowasa Pinda ataiweza?
 
Wishimiwa, tumesikia data za Mh Kandoro, hebu tushuke pale Mwanza kwa Dr. James Msekela mnasemaje utendaji wake wa kazi kama mkuu wa mkoa kwa miaka miwili?
 
siasa sio hisabati, msekela hana jipya! hata kuhamasisha ujenzi wa shule hadi masha atoke bungeni! Pinda atutendee haki aturudishie Daniel Ole Njolay au mzee mashishanga. Ati anasingizia anaona majoka usiku! hii yote gear ya kutaka kukimbia tu output yake ziro, viwanja vya magufuri vimeisha hata kuwahimiza jiji wapime vingine kashindwa.
 
Chonde chonde mzee uwe makini kuwateua hawa akina mama, tuliona majibu utumbo ya megji na kule kenya wanahangaika na martha karua, hata EU wameona hazimtoshi!
 
Eddy,

Kauli nzito hii, yaani unamaanisha wazee wa kisukuma wana mtesa msomi wetu kwa kumletea mijoka usiku? au nimekuelewa vibaya?
Ingawaje nimewahi kusikia kwa watu wengi wanalalamika kuwa utendaji wake wa kazi ni zero, mpaka kuna mkuu wailaya aliwahi kumpa live kuwa yeye ndo mkwamishaji wa mipango yote ya maendeleo ufuatiliaji ni zero.
 
Mwenye data za Msekela James amwage hapa ndiyo kazi kubwa ili kumsaidia Pind kujua apinde ama abaki wima.
 
Wishimiwa, tumesikia data za Mh Kandoro, hebu tushuke pale Mwanza kwa Dr. James Msekela mnasemaje utendaji wake wa kazi kama mkuu wa mkoa kwa miaka miwili?
Huyo jamaa ni ziro kabisa,ofisi yake sasa hivi imekuwa centre ya kukutana na wapigakura toka Tabora ambao wanasafiri kila siku kuja kupiga soga nae na kumletea umbea wa huko.
Njoolay alianzisha gardens za watu kupumzika lakini sasa hata haziendelezwi. Sio hilo tuu,yapo mengi ila muhimu ni kuwa Mwanza kama jiji imemshinda.
 
James nani kamweka pale kama hana afanyalo ? Kuna faida gani kwa aliye mweka pale ?
 
Lizy nimepata tetesi kwamba JK na mshikaji wake Upinde wana nia ya kuongoza wanawake kwua wakuu wa Mikoa so kaa mkao wa kuitwa kwenye ufalme

Wow,

Sounds promising (!!!!!!!!!?????)

Wana JF Please, pendekezeni jina langu. Nina sifa zote mpaka napitiliza (no doubt).
 
Dr. Msekela, Mwana Tanzanet mwingine ambaye alipokuwa Sweden, tulikuwa tunapata cheche zake. Sasa mwambie aje hata kwenye mitandao, hawezi kukubali kwasababu amepewa nafasi na ameshindwa kudeliver yale ambayo tulikuwa tunajadiliana naye kila siku.

Ubunge wenyewe kabebwa mara zote. safari zote alishindwa ila NEC wakambeba kwa kuwaondoa washindi na kumweka yeye. Kuna safari alikuwa mtu wa tatu lakini bado wawili wa mwanzo wakaondolewa na kupewa yeye.

Ukianza kuona mtu anaanza kukimbia washikaji wa mwanzo, jua hapo kuna mambo
hayako sawa.

Nafikiri Waafrika tuna kaugonjwa kabaya sana kama anavyosemaga ndugu yangu Mkamap.

Tatizo la JF hatujuani kwa majina, maana mimi naandaa dossier ili mtu akipata ulaji, nimwambie ulisema hili na hili mbona hutimizi?

Niliokutana nao kule Tanzanet hao wote kila mtu nina file lake (kwi kwi kwi!!)
 
Mtanzania,

Haya makubwa kwi kwi kwi, vipi yule jamaa yako msaidizi wa BWM?
 
Mtanzania,

Haya makubwa kwi kwi kwi, vipi yule jamaa yako msaidizi wa BWM?

Yombayomba,

Kwi kwi kwi!!!!! yaani nimecheka kweli kweli. Yule alikuwa mwana Tanzanet kweli kweli, lakini sasa baada ya ufisadi wa mzee, naona kijiwe kimeota miiba. Ukimwona mwambie aje JF, huwa hatutumii majina hapa.
 
Majita umetoa insight nzuri sana .Huyu jamaa yaani kandoro ana Masters ya kitu gani ? Mbona mie namuona mtupu sana ? Kiburi yeah anacho he can tell huhitaji kuuliza .Now kwa maana nyingine Pinda ameshapata msaada kama anautaka wa kumuondoa ama umwacha Kandoro.Lakini kwa kuwa Msemaji wa mwisho ni mzee wa Pwani mwenziwe nadhani kandoro kama Makamba ana mambo ya ajabu lakini naweza nasema linabaki kuwa chaguo la Mkwere !!!!!!!!!!!!!!!!!

MTAALAM KANDORO NI MNYAMWEZI KWA BABA NA MAMA MNYALUKOLO MZALIWA WA MAZALIWA WA KIJIJI CHA MASUMBO -KIBAONI IFUNDA IRINGA,ELIMU YA MSINGI MASUMBO P/SCHOOL, AMEFANYA MENGI NDANI YA DAR. UJIVUNI NI WASIFU WA ZIADA WA KILA BINADAMU
 
Lunyungu Kama Kuna Hilo Basi Vema Meja Jenerali Kalembo Arudishwe Lindi Kwao Morogoro Ameiangamiza Kabisa Maana Alianza Mashishanga Kaleta Wasukuma Wanakata Misitu Yetu ,ng'ombe Wakausha Vyanzo Vya Asili Vya Maji Yetu- Above All Ukiachilia U Jenerali Wake Ni Wazi Kachoka Na Hatufai Morogoro.

Nisiseme Mengi Miye,na Watafiti Wamtembelee Huyu Mzee Waone Kama Ana Dalili Za Uchanya Kwa Morogoro
 
Dr. Msekela, Mwana Tanzanet mwingine ambaye alipokuwa Sweden, tulikuwa tunapata cheche zake. Sasa mwambie aje hata kwenye mitandao, hawezi kukubali kwasababu amepewa nafasi na ameshindwa kudeliver yale ambayo tulikuwa tunajadiliana naye kila siku.

Ubunge wenyewe kabebwa mara zote. safari zote alishindwa ila NEC wakambeba kwa kuwaondoa washindi na kumweka yeye. Kuna safari alikuwa mtu wa tatu lakini bado wawili wa mwanzo wakaondolewa na kupewa yeye.

Ukianza kuona mtu anaanza kukimbia washikaji wa mwanzo, jua hapo kuna mambo
hayako sawa.

Nafikiri Waafrika tuna kaugonjwa kabaya sana kama anavyosemaga ndugu yangu Mkamap.

Tatizo la JF hatujuani kwa majina, maana mimi naandaa dossier ili mtu akipata ulaji, nimwambie ulisema hili na hili mbona hutimizi?

Niliokutana nao kule Tanzanet hao wote kila mtu nina file lake (kwi kwi kwi!!)

Wamchongea RC kwa JK

na Edward Ibabila, Mwanza

WAKAZI kadhaa wa mkoani hapa, wamemchongea Mkuu wa Mkoa (RC) wao , Dk. James Msekela, kwa Rais Jakaya Kikwete, wakimtaka amwondoe mkoani humu kutokana na kutowatumikia vema.

Wakazi hao wamemwomba Rais Kikwete kumwondoa Dk. Msekela, kwa sababu hawaridhishwi na utumishi wake, kutokana na kile walichodai kuwa kushindwa kwake kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi mahususi kero zinazowakabili.

Wakizungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliyopita nje ya ofisi ya mkuu huyo wa mkoa, baadhi ya wakazi hao walisema tangu Dk. Msekela alipoteuliwa katika wadhifa huo takriban miaka miwili iliyopita, kero nyingi za wananchi hazisikilizwi na kupatiwa ufumbuzi ipasavyo.

Walisema hilo linatokana na Dk. Msekela kutumia muda mwingi akiwa jimboni kwake, hasa mwishoni mwa vikao vya Bunge. Pamoja na cheo cha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Msekela pia ni Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM).

Walisema muda mfupi anaokuwa ofisini huutumia kuzungumza na watu anaowataka yeye, hususan wafanyabiashara na watumishi wa serikali, huku wananchi wenye kero wakipewa majibu ya njoo kesho na katibu wa mkuu huyo wa mkoa.

Walidai kuwa wengi wao walikuwa wameandika barua nyingi za malalamiko mbalimbali yanayotakiwa kushughulikiwa na mkuu huyo wa mkoa, lakini wanapofuatilia huambiwa na karani wake kuwa barua walizoandika hazionekani, na kutakiwa kuandika barua nyingine, jambo ambalo walisema ni usumbufu mkubwa.

“Unavyoniona na hali yangu hii, leo ni mwezi wa tatu nafuatilia majibu ya barua yangu niliyomwandikia mkuu wa mkoa kumuomba anisaidie kupata kiwanja changu ambacho nilidhulumiwa. Lakini sijapata majibu hadi leo. Kila unapokuja unaambiwa rudi kesho, mwisho nimechoka kabisa,” alisema mwanamke mmoja mlemavu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.

Naye katibu tawala mstaafu ambaye kabla ya kustaafu alifanya kazi katika moja ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambaye alikuwa miongoni mwa wananchi hao, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alieleza kusikitishwa kwa vitendo vinavyofanywa na mkuu huyo wa mkoa na kuongeza kuwa iwapo Rais Kikwete hatamuondoa mapema, wananchi mkoani hapa watazidi kuichukia serikali yake.

“Kwa kweli mambo anayofanya RC wetu yanakatisha tamaa. Mtu unaweza kufika ofisini kwake saa 2 asubuhi, ukatoka saa 8 mchana, bila kumuona au kutatuliwa kero yako. Utaona wanaosikilizwa ni wafanyabiashara na watumishi wa serikali. Hizi ni kasoro kubwa kwa kiongozi wa serikali. Iwapo rais hatachukua hatua ya kumuondoa haraka, serikali yake itaendelea kubebeshwa lawama,” alisema.

Aidha, wakazi hao walilalamika waziwazi juu ya hatua ya Rais Kikwete kuteua wakuu wa mikoa na wilaya ambao pia ni wabunge, na kuongeza kuwa ni vigumu kwao kutekeleza majukumu ya kazi hizo mbili kwa wakati mmoja, hali inayosababisha kuwapo kwa udhaifu wa kiutendaji, hususan katika nafasi za uongozi wa kuteuliwa.

Baadhi ya wakazi hao, walidai kuwa walifikisha kero zao kwa mkuu huyo wa mkoa zaidi ya miezi tisa iliyopita, lakini hawajasikilizwa hadi sasa.

Alipoulizwa juu ya malalamiko dhidi yake na ofisi yake kwa ujumla, Dk. Msekela alikiri kutumia sehemu ya ratiba yake kutembelea wananchi wa jimbo lake.

Hata hivyo, alisema hiyo haiwezi kuwa sababu ya kushindwa kutekelezwa kwa majukumu yaliyo chini ya ofisi yake, kwa sababu kila anapoondoka hukabidhi ofisi kwa mtu anayekaimu.

Kuhusu kupotea kwa barua za malalamiko ya wananchi, mkuu huyo wa mkoa alisema binafsi hajawahi kupokea malalamiko ya aina hiyo.

“Sijawahi kupokea malalamiko ya aina hiyo. Hata hivyo, kama yapo, wananchi watumie namba yangu ya simu ya mkononi kunijulisha, nami nitachukua hatua,” alisema.

Source: Tanzania Daima
 
Back
Top Bottom