Leo naomba niseme tu ya moyoni bila kuweka siasa.
Jamii zetu sisi kama Watanzania kwa kuishi kwangu nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Lakini nimekaa na jamii tofauti, nimetembea nchi tofauti na kuona jamii zao lakini vilevile nimeishi na watu wa jamii karibia za aina zote hapa Duniani. Watanzania tuna upendo sana lakini tuna mapunguvu makubwa ambayo ndiyo yanaturudisha nyuma na hili ni kwenye jamii na tamaduni zetu. Ushauri wangu kwasababu Watanzania bado ni jamii ya vijana wengi 75% chini ya miaka 35 basi ni vizuri wakubwa kwenye jamii kuonyesha mifano mizuri .
1. Udanganyifu ni tatizo sana kwenye jamii yetu. Nilishatoa ushuhuda hapa kwamba nilimweka mzee mmoja kwenye shamba langu bagamoyo nikamjengea nyumba na kumpa pikipiki lakini aliishia kuweka pikipiki rehani na kuanza kuuza mabati ya nyumba ambayo anakaa mwenyew ili tu aseme ni wezi halafu nimtumie pesa. Lakini kibaya zaidi yeye kutokuwa mwaminifu imenifanya nisiwekeze zaidi kwake kitu ambacho kingesaidia kaya yake na yamii kwa ujumla. Tatizo la uaminifu ni kubwa sana. Lakini nilivyokuwa Dar miezi michache tu imepita nikashauriwa ninunue vifaa vya ujenzi kwa wapemba tu nilipouliza sababu wakasema wapemba ni waaminifu. Hivyo kumbe uaminifu unaweza kabisa kukusaidia kuendelea na wizi na udanganyifu ndiyo utakandamiza kabisa maendeleo yako
2. Kujua na kujiaminisha uongo. Tumekuwa na utamaduni kama jamii kujiaminisha uongo hata kama ukweli upo wazi. Hii tumeona hata kwenye siasa kuanzia kujiaminisha Corona haipo kwetu, miti shamba, manabii fake, uchawi fake, ........ yaani tuna utamaduni wa kuamini uongo hata kama ukweli upo wazi. Hili linaturudisha nyuma sana kimaendelo. Hata sasa mfano wabunge nimesikia wanaongelea bei kama vile hawajui sababu ya bei kuwa juu kwasababu tu tuna utamaduni wa kupenda kulalama na kujidanganya hata kama ukweli upo wazi.
3. Kupendana. Watanzania tunapendana pale tu tunapopata matatizo. Watanzania tutazikana sehemu yeyote na kusaidia kwenye shida laikini hatuna upendo wa kimaendeleo. Mfano Wa Ethiphia na Wakenya wana ukabila sana lakini Mkenya au waethiphia wakifungua biahara wanasaidiana na kuwa wateja bila kujali makabila. Sisi mfano tunachangia sana kwenye misiba lakini hatuwezi hata hapa US kusikia Watanzania wamechanga kila mwaka na kununua hisa za bond za serikali ili kusaidia nchi na kuwekeza nchini kama jamii. Huwezi kusikia tumefungua shule na kitu cha pamoja cha kimaendeleo kwasababu huyo mwenyekiti wa hiyo jumuia kuna watu watamuonea wivu na kumsema na kumtukana kiasi kwamba watanzania wengi wanaogopa kuwa viongozi kwenye jumuia zetu za ndani na nje kwasababu ya majungu na hii ni hata pale wakifanya kazi kwa kujitolea. Lakini tunasema tuna upendo lakini mpaka leo hakuna mtu anajua ni kwanini Watanzania wenye upendo wanawaogopa na kuwachukia ndugu zao wa diaspora kuliko Kenya na Ethiphia wakati hatuna ukabila? Watanzania sisi tuna utamaduni wa kujilinganisha na kama tunafuikiria kwa namna yeyote kuna mtu amekuzidi kitu basi badala ya kutafuta njia tuna utamaduni wa kuwachukia na kuhakikisha wapo wote tupo chini. Angalieni sababu za serikali kutokutangaza matokeo na wananchi wanaona sawa tu wakati mitihani haina siasa lakini kuna watanzania wanaumia tu pale wanapozidiwa badala ya kutafuta mbinu. Sasa tutakuwa na shule ambazo zinafelisha lakini kwasababu kuna utamaduni wa kujiaminisha uongo wanataka wananchi wajiaminishe kwamba shule za kata ni bora sana au sawa na shule ambazo kiukweli zinafaulisha.
4. Kulalamika sana. Tuna utamaduni wa kulalamika sana na hili linaturudisha nyuma kama jamii
Haya ni mambo nayofikiri yanaturudisha nyuma.
Pascal Mayalla bro upo?