Natty Bongoman
JF-Expert Member
- Oct 10, 2008
- 648
- 384
Tusisahau historia yetu, na tuwafundishe watoto na vijana ili wasije ingia mkenge tena
TUSISAHAU HISTORIA YETU, NA TUWAFUNDISHE WATOTO NA VIJANA ILI WASIJE INGIA MKENGE TENA
View: https://youtu.be/iGPUtwa9LkQ?si=ks4MVUocwBUSyS2G
aisee watamka ukweli, mambo ya laghai za divide snd conquer hadi baadhi yetu wameingia mkenge ... wale wasio wazalendo ama wamesahau mila zetu za kuwa ndugu wa kusaidianaSisi wenyewe hatutakiani mema pia angalia tunayotendana.
TUSISAHAU HISTORIA YETU, NA TUWAFUNDISHE WATOTO NA VIJANA ILI WASIJE INGIA MKENGE TENA
View: https://youtu.be/iGPUtwa9LkQ?si=ks4MVUocwBUSyS2G
Pointi nzuri sana nzalendoTATIZO LETU WAAFRIKA TUMETAPELIWA NA KUACHA ASILI YETU (TORATI YA IBRAHIMU...ISAKA...NA YAKOBO)....HAKIKA SISI NI WALE TULIOANDIKWA KWENYE BIBLIA.....NDIO MAANA LAANA ZINATUCHAPA MPAKA TUTAKAPOJITAMBUA......WAZUNGU WANAJUA HILI NA WANAOGOPA SANA......
Sina uhakika ila kwa vile hatuwaletea fujo za ukombozi, labda ndo maana hatuna hiyo historia kama Maumau waKenya walivouawa na hao hao waingereza...lakini Waingereza wakati wa utawala wao hawakuuwa watu kama walivyofanya CCM.
Sina uhakika ila kwa vile hatuwaletea fujo za ukombozi, labda ndo maana hatuna hiyo historia kama Maumau waKenya walivouawa na hao hao waingereza.
Sisi tuliuawa sana na mjerumani wakati wa tawala yake - Kina Chifu Mkwawa, Songea, na viongozi wetu wengineo wengi pamoja na wapambanaji wa vita yetu kuu ya majimaji. Historia imetunyima kutuelezea vile wahenga wetu walivopambana kikali hata kumshinda mjerumani hapa na pale hadi wao kuongeza nguvu...
Asante mkuu kwa hili somo la historia yetu...miaka ya 1940 wakati wa Utawala wa Waingereza kulifanyika maandamano na mgomo wa watu zaidi ya 10,000 ambao walipiga kambi ktk ofisi za Mkuu wa wilaya ya Pare [Same] kwa miezi miwili mfululizo wakipinga kutozwa kodi.
..Waingereza hawakutumia mabavu wala kuwauwa waandamanaji hao. Sasa piga picha maandamano hayo yangefanyika ktk utawala huu tulionao sasa hivi watu wangapi wangeuwawa.
Asante mkuu kwa hili somo la historia yetu.
Same walikuwa na umuhimu gani kiuchumi kwa waingereza?
Pointi.
Pointi nzuri sana nzalendo
Walio wengi, kutokana na elimu ya mzungu, hata ya kidini, bado hawajasanuka sisi ndo tuliendikwa bibliani.
- tunasoma na kusikia mchungaji kila anapozika tuliumbwa kwa udongo na Yesu akitambulishwa akiwa na nywele katani na miguu rangi ya shaba ilochomwa motoni, Lakini bado wengi wetu wanatundika picha ya Yesu mzungu wakiamini walichopotoshwa na mzungu... Jamani, wenzangu tafiti hio picha, google 'picha ya Borgia', mjomba wake Kadinali ndo aliebadili picha na kanisa katoliki kueneza. Cha kusikitisha huyo Borgia alikuwa mtenda madhambi noma.
- tunajua tawala Za kina Farao wa Misri walikuwa weusi ka sisi, kisha tunasoma Musa alikulia Misri akidhaniwa ni Mmisri, na Yesu alifichwa Misri ili asiuawe na Herode ...na bado tumemeza uongo.
- Ushahidi ni mwingi bibliani, ila mazoea yetu ya kumsikiliza na kumuamini mchungaji bila kuthibitisha bibliani imetuponza. Nahisi ni moja ya adhabu tulopewa, pamoja na adhabu nyinginezo nyingi kama Kumbukumbu la Torati 28 inavotuelezea wazi na kwa kirefu.
Big Ups kwako
Mkuu, yote hayo usemayo... je watuambia utawala wa muingereza ulitunufaisha?..wakoloni walianzisha mashamba ya mkonge, na walijaribisha kilimo cha pamba.
..ukiacha mgomo uliotokea Same kuna mgomo mwingine ulitokea kanda ya ziwa na wenyewe Waingereza hawakuuwa wananchi.
Ndo pointi yangu... dini tuloletewa ilishatekwa, kuchujwa na kupotosha ili kufanikisha utumwa na ukoloni..mbona Wachina na Wahindi hawakukubali Dini za kigeni na wanadunda mambo yao yako vizuri?
Mkuu, yote hayo usemayo... je watuambia utawala wa muingereza ulitunufaisha?
* Hayo mashamba pamoja na ya chai yalitunufaisha sisi ama yeye tena kwao?
nimekumbuka... ile biashara 'pembe tatu' ... mali ghafi tokea kwetu bei chee ama bure, utengenezaji ama uchujaji
(madini) kwao, kuuziwa bidhaa za mazao yetu bei ghali... kitu ambacho hata ukoloni mamboleo bado watumia
barani Afrika
* Muingereza kila alikotawala aliua utamaduni asili ama alijaribu mbaya mno... eti si ustaarabu ama ni upagani.
neno 'ustaarabu' laonyesha muarabu naye yumo...
* Tanzania ya muingereza - yeye kiongozi, muhindi karani, sisi mazezeta ndo wachafua mikono isipokuwa wale
wachache walochaguliwa mashuleni mwao ama na mapadre wao... wale ambao brainwashing imekubali.
Kwa maoni yangu, kwa muingereza Tanzania ilikuwa shamba lake na almuradi kilimo kinaendelea hakujali maandamano unayotupa elimu