Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Kupigana na maradhi mengine
Ikiwa katika mji magonjwa yalizidi kwa watu mkubwa wa mji hupigisha ramli kusudi apate njia ya kuzuia magonjwa hayo yasizidi, pia apate kufahamu ni mambo gani yaletayo magonjwa mjini mwake.
Mara nyingi waganga walikuwa wakiwaambia kuwa moto unaotumika mjini mwao ulikwisha haribika yaani ulichukuliwa na wachawi. Basi, njia iliyokuwa bora ni kupata moto mpya na ule wa kwanza uzimwe, yaani upatikane moto wa kupekecha, na vile vile wapate dawa za zindiko la mji kuzuia wachawi kuuchukua moto na kuuchafua (eti moto ukichukuliwa na wachawi, unapowashwa, yule unayemfukia moshi huweza kudhurika, sababu moto wa kawaida ulifichwa, na ule ulikuwa wa kichawi), pia wachawi wasipate nafasi kuingia mjini kuleta maradhi mbalimbalii.
Walikuwa wakimwalika mganga yule aliyeweza kuwaambia haya kuja kuzima moto ule. Kila nyumba ilikuwa lazima kuuzima moto, na baada ya kuuzima vijinga vyote vya kuni pamoja na makaa na majivu yote hukusanywa yakarundikwa nje penye njia panda.
Katika chungu hiyo mganga hutia zindiko lake, kisha huwashwa moto mpya wa kupekecha. Pengine badala ya kuuzima moto wa mji mzima hutolewa dawa za kuwaosha watu wote, kisha huchanjwa chale za kago.
Mganga huyo baada ya kuitwa kwa kazi ya kuusafisha mji, alikuwa hawezi kukubali kutengeneza dawa kabla ya kupewa kwanza Shs. 10/- mbali ya ujira wake, na vile vile huhitaji Shs. 2/- kwa kila mtumishi wake ambao kwa kawaida huwa wawili.
Baada ya matengenezo ya dawa watu wote wa mji ule huchanga mtama wa pombe ya kuzima moto, yaani mganga apate kuuwekea moto ule mibaraka.
Siku ya kuiva pombe hiyo hupewa ujira wake Shs. 10/-.