DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Mimi ni mmoja wa watu wa mwanzo kupiga kelele kuhusu ukarabati wa uwanja wa Mkapa. Haya tunayoona sasa ya Simba kushindwa kutumia uwanja ni matokeo ya watu kutuona wengine tuna viherehere na kutotuunga mkono mapema wakati tunayapigia haya kelele.
Kuna fedha nyingi zimewekwa kwenye ujenzi wa uwanja wa Arusha. Kama sikosei wa Dodoma nao ujenzi umeanza. Hivi viwanja vipya vitabeba majina ya viongozi wa sasa wa kisiasa na ndiyo vinaonekana kuwepa kipaumbele.
Shida ya ukarabati wa uwanja wa Mkapa siyo meneja wa uwanja kama baadhi ya watu wanavyokurupuka au kutaka kupotosha. Ninavyoona mimi ni kuwa shida ni kuwa pesa iliyoelekezwa ipelekwe kule haijapelekwa huko kwa sababu hakuna credit sana za kisiasa kumpromoti Mkapa kwa sasa. Tungebadili jina la uwanja uone kama usingekuwa kama Santiago Bernabéu.
Niko tayari kubeti kuwa hata AFCON haitafanyika kabisa Dar es Salaam ili viwanja vyenye majina ya wanasiasa wa sasa vipewe promo zaidi na vipate fursa ya kutumika katika hatua za ufunguzi na/au fainali.