Tukiwa kwenye mwezi wa huduma kwa wateja, tuwapongeze watoa huduma na taasisi ambazo zinatoa huduma nzuri na kutekeleza hitaji la mteja

Tukiwa kwenye mwezi wa huduma kwa wateja, tuwapongeze watoa huduma na taasisi ambazo zinatoa huduma nzuri na kutekeleza hitaji la mteja

Half american

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
38,283
Reaction score
97,793
Mwezi huu oktoba ni mwezi wa huduma kwa wateja, ndani ya wiki hii zimeshuhudiwa taasisi nyingi zikiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.

Huduma kwa Wateja ni sherehe ya kimataifa ya umuhimu wa huduma kwa wateja na ya watu wanaohudumia na kusaidia wateja kila siku . Wiki ya Huduma kwa Wateja ilianza rasmi mnamo 1987.

Huduma kwa wateja inatoa usaidizi ambao shirika/taasisi/kampuni hutoa kwa wateja wake kabla au baada ya kununua au kutumia bidhaa au huduma . Huduma kwa wateja inajumuisha vitendo kama vile kutoa mapendekezo ya bidhaa, masuala ya utatuzi na malalamiko, au kujibu maswali kwa ujumla.

Tukiwa miongoni mwa wateja wa huduma kwenye taasisi, makampuni na mashirika mbalimbali tuwape maua yao wahudumu/wafanyakazi wanaotoa huduma nzuri zinazopelekea kutimiza hitaji la mteja.

Binafsi ninaanza na kuipongeza kampuni ya usafirishaji ya BM COACH, licha ya ubize wa kazi kitengo cha mizigo ila nilipata huduma nzuri sana ambayo sijawahi kuipata popote kutoka kwa dada anaetambulika kwa jina la ZUU(sikufanikiwa kuuliza zaidi kutokana na ubize wa kazi), yupo ofisi za BM COACH MOSHI MJINI.

Dr. Zainab Tindi, huyu ni specialist wa maswala ya tiba na lishe MOI, Nilipendezwa sana na huduma yake. Kwa wale mnaojali maswala ya afya na lishe hutochoka kumsikiliza na kujifunza kwa huyu mtaalam wa mambo hayo.

Nitaendelea kuwataja wengineo kwenye komenti, taja mtoa huduma yeyote kama uliridhishwa na huduma yake nzuri, hata kama ni duka la mangi taja weka na location hakuna asiependa huduma nzuri.

Nawasilisha.

download (4).jpeg
 
Customer Care wangu ni mie mwenyewe!!

NAJIPA MAUA MWENYEWE

Wateja wangu wanaenjoy sio kidogo
Customer Care wangu ni mie mwenyewe!!

NAJIPA MAUA MWENYEWE

Wateja wangu wanaenjoy sio kidogo
Weka na postikodi ya ofisi/upatikanapo ili tuwaagize cheergirls/gigolo wakuletee zawadi zako.
 
Yule mama wa mihogo aliyenizoea mpaka ananipa offer kibao siku nyingine nakula bure naweza muandika hapa?
Muandike mkuu hata wale wauza dagaa za kurumangia wataje na ile pilipili ya mbilimbi warushe na mitaa yao siku ya siku tukibahatika kupita mitaa yao tuwaungishe.
 
Una bidhaa gani upate wateja wapya hapa? Itangaze biashara yako.

Asante ndugu mtangazaji kunipa nafasi hii kutangaza biashara yangu.

JAMANI MIE NAIUZA HII KWA BEI NZURI KULINGANA NA MAHITAJI YA MTEJA.

NAWAKARIBISHA NYOTE MJE KUINUNUA KWANI INA KILA KINACHOHITAJIKA NDANI YAKE

KARIBUNI SANA.

Asante
 
Kuna mama mmoja pale CRDB Bank tawi la Mbezi Luis kule chini kwenye stendi ya bajaji. Nilimkuta kwenye dirisha lililoandikwa Bulk. Japo niliagizwa kwenda huko kimakosa maana sikuwa hata na mia mbovu mfukoni, lakini alinihudumia vizuri sana mpaka nikashangaa. Na nilielewa maana katika dirisha lake kulikuwa na ngao kadhaa kuashiria kuwa alishashinda tuzo za "best customer care" mara kadhaa huko nyuma.

Mungu Ambariki sana 🙏🏿
 
Naipongeza taasisi ya mikopo ya SELF kwa huduma nzuri mkopo wanatoa mpaka bilioni 10 ndani ya siku kumi na saba au pungufu. Asante sana SELF.
 
Naipongeza taasisi ya mikopo ya SELF kwa huduma nzuri mkopo wanatoa mpaka bilioni 10 ndani ya siku kumi na saba au pungufu. Asante sana SELF.
Ipo wapi hiyo mkuu, pongezi nyingi kwao
 
Kuna mama mmoja pale CRDB Bank tawi la Mbezi Luis kule chini kwenye stendi ya bajaji. Nilimkuta kwenye dirisha lililoandikwa Bulk. Japo niliagizwa kwenda huko kimakosa maana sikuwa hata na mia mbovu mfukoni, lakini alinihudumia vizuri sana mpaka nikashangaa. Na nilielewa maana katika dirisha lake kulikuwa na ngao kadhaa kuashiria kuwa alishashinda tuzo za "best customer care" mara kadhaa huko nyuma.

Mungu Ambariki sana 🙏🏿
Hongera kwake na azidi kubarikiwa, ni miongoni mwa wachache wanaojua wanachokifanya. Vijana hasa wa crdb wanalalamikiwa sana kwa huduma mbovu, wana la kujifunza kwa utendaji wa mtu kama huyo.
 
Back
Top Bottom