Tukiwa na kadi ya kuingia harusi ausherehe yeyote kama ya mwendokasi ni biashara?

mbere

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
6,967
Reaction score
6,465
Wakuu,

Baada ya kuhudhuria harusi kadhaa kuna wazo nimepata kutokana na changamoto ya uingiaji unayofanana kwingi Tanzania.

1. Kutafuta kadi kama za mwendo kasi au ATM, NMB wana uwakala nazo, unakuwa pia na Mashine ya kuscan hizo kadi kadri ya utakavyopewa majina na kamati ya harusi husika.

2. Kwenda kwenye kamati mbalimbali na kutafuta tenda za kadi hizo za kisasa kwa ajili ya sherehe mbalimbali. ( kwamba MTU hataweza kuingia bila kuwa scanned ) So utakuwa umeondoa udanganyifu.

Hivyo utaokolea kamati usumbufu wa kusimama mlangoni
Na utaondoa cheating kabisa.

Naomba kuwasilisha wazo la kibiashara toa maoni na changamoto zake.

N.B: Unaweza pia kuwa na sever kwa utendaji mzuri zaidi na pia uweze kumudu harusi nyingi kwa wakati mmoja n.k.
 
Hilo wazo nimelikubali kwan capital yake yaweza kuwa sh.ngap?
Mtaji hapo ni mashine ya kuscan kadi ambazo utanunua kadhaa ambazo zujajua garama yake bado naa kadi za kutosha buti ambazo hazizidi 2000 kwa mmoja
Ina maana kila kadi utauza kati ya 4000 _ 5000
So naona kuna kajifaida nakaona

Kuna changamoto kila biashara ina changamoto wadau wanisaidie
 
Na kadi zenyewe zitakuwa za kurudisha
Kuna changamoto ya kutorudi kwa kadi kadhaa kwasababu sii wote watahudhuria harusini na nyingine kupotea, ila sii hasara kubwa maana siyo nyingi
 
Agreed. Ila kumbuka kuna TRA watataka chao
 
Hongera mkuu, kweli umewaza nje ya box
 
Kuondoa wasimamizi mlangoni utahitaji mageti yenye scanner kila ukumbi kama yale ya uwanja wa Taifa. Ni big investment
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…