Tukiwa Tunaelekea Uchaguzi Mkuu: Ni Yapi Majukumu ya Mbunge?

Tukiwa Tunaelekea Uchaguzi Mkuu: Ni Yapi Majukumu ya Mbunge?

Pantosha

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
640
Reaction score
958
October mwaka huu watanzania watawachagua viongozi watakao pewa dhamana ya kuongoza nchi hii kwa miaka mitano (2025 - 2030).

Wale wataochaguliwa watakuwa wataunda mihimili ya serikali na bunge na wana influence kubwa pia kwenye mahakama.

Kuyafahamu majukumu ya Mbunge huenda itasaidia vyama vya siasa kupendekeza aina ya watu wanaoweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo na pia wananchi watakuwa na choice zinazotakiwa badala ya watu wa kujaza namba tu kupiga makofi/meza.

Majukumu ya msingi ya Mbunge yanaendana na majukumu ya bunge ambayo ni pamoja na:
1. Kutunga/kuboresha/kubatilisha/kupitisha sheria
2. Kuishauri na kuisimamia serikali
3. Kupitisha budget ya serikali
4. Kuwakilisha wananchi, nk.

Sasa kutokana na majukumu hayo, unaona kabisa mbunge wa jimboni kwako atakuwa msaada kwa taifa?

Je, kuna haja ya kuwa na Mbunge aliyeshiba kielimu, mwenye uzoefu, anayependa kusoma vitabu, nk?

Ni sifa zipi za Mbunge twende nazo 2025?
 
Kujua kusoma na kuandika


"Je ni lini serikali italeta mkandarasi wa finance and building?" - Hamis Taletale mbunge wa morogoro kwa tiketi ya CCM
 
Kujua kusoma na kuandika
Sifa zilizopo kwenye katiba ya sasa:

Mbunge ana sifa hizi hapa:
1. Kujua kusoma na kuandika Kiswahili au kiingereza.
2. Awe mwanachama wa chama cha siasa.

Nonsense kabisa.
 
Sifa zilizopo kwenye katiba ya sasa:

Mbunge ana sifa hizi hapa:
1. Kujua kusoma na kuandika Kiswahili au kiingereza.
2. Awe mwanachama wa chama cha siasa.

Nonsense kabisa.
Endeleeni kuhisi CCM ina lolote jipya la kuwasaidia
 
Endeleeni kuhisi CCM ina lolote jipya la kuwasaidia
Acha kuwa na allergy na CCM.

Kwa taarifa yako waanzilishi wengi wa vyama vya Upinzani walikuwa CCM, wakatoka sio kwa ajili ya ukombozi wa wananchi bali kwa ajili yao.
Hapa issue ni Mbunge awe na sifa zipi?
 
Nipigien kula mm mbunge wa ubungo najua kusoma na kuandika ntaweka morogoro road subway wananchi sitawaangusha

😹😹😹🙌🏾
 
Acha kuwa na allergy na CCM.

Kwa taarifa yako waanzilishi wengi wa vyama vya Upinzani walikuwa CCM, wakatoka sio kwa ajili ya ukombozi wa wananchi bali kwa ajili yao.
Hapa issue ni Mbunge awe na sifa zipi?
Kwani hata akiwa na sifa usemazo anachaguliwa na wananchi ama na dola? Kama anachaguliwa na dola ni wazi atapangiwa cha kufanya akiwa bungeni.
 
John Heche ameelezea kwa uzuri zaidi wajibu na majukumu ya mbunge.
 
Majukumu ya wabunge ni kila jambo ndio bungeni hata wakiambiwa wote ni wajinga watapiga makofi bungeni
 
Mbunge kazi yake ni kula posho na Mshahara wake no more to it. Mengine yote mnajidanganya tu.
 
Back
Top Bottom