Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Nimesikia vizuri mchango wa Prof. Muhongo bungeni na kutafakari kwa makini. Nilichosikia ni takwimu na maelezo yaliyoshiba ukweli na uhalisia wa hali ya sasa ya dunia. Amechambua namna gani rasilimali tulizonazo zinaweza kuinua uchumi wetu kama tutazitumia vizuri na kwa wakati. Muhongo ametoa takwimu na si maneno matupu ya kupamba mtu.
Aidha nimesikia michango ya Kibajaji na Msukuma. Michango yao imejaa kejeli na vitisho kwa Muhongo na wote wenye mawazo mapya na tofauti na Magufuli. Muda wote wamakuwa wakisifia na kumuenzi Magufuli. Hawana takwimu zo zote za ku-support hoja zao. Wamesahau kuwa sasa ni muda wa kijadili mpango wa maendeleo na bajeti.
Nimeona baadhi ya watu wakiwapongeza Kibajaji na Msukuma huku wakimrushia matusi Prof. Muhongo. Nadhani huu ni muelekeo potofu na kama hautarekebishwa tutajikuta Taifa halina dira na linaangamia. Tanzania kama Taifa lazima tutafute mwelekeo sahihi kwa pamoja kwa kutumia rasilimali watu na vitu tulivyonavyo.