Tukubali au tukatae kwenye hii sayari ya Dunia katika nyanja ya Soka hakuna kama Pele wa Brazil



Una miaka mingapi? maana mawazo ya mtu wa miaka 75 kipindi hiki ni ngumu kuyaelewa, tusije kukuonea kumbe umakaribia kumaliza utumishi wako
 
Hivi wakati akiiwezesha Brazil kubeba world cup mara tatu hao mabeki wako mahiri wa ulaya hawakuwepo? Maradona alikuwa hodari lakini alivuma kwa muda mfupi sana(kama Gaucho).
Maradona ana takwimu chache zinazidiwa hata Cr7, hata hilo taji la world cup ni msaada tu wa goli la mkono
 
Una miaka mingapi? maana mawazo ya mtu wa miaka 75 kipindi hiki ni ngumu kuyaelewa, tusije kukuonea kumbe umakaribia kumaliza utumishi wako
Huyo Pele, ni wa miaka ileee! Kwa kizazi cha sasa, aje Pele yule yule, hataweza kutamba kama vile.
Ile, kupiga chenga kutoka katikati ya uwanja mpaka goli la mpinzani unaangaliwa tu, kwa sasa ni nadra sana!
Ila ki-burudani, sijamuona kama GAUCHO na ZIZOU!
 
Soka zamani ilikuwa brazil argentina, italy, germany na zote hizi pele kacheza nazo na wenyewe wanakiri zaidi ya wengine kuwa alikuwa kiumbe wa ajabu katika soka
 
mm tomaso, huyo pele sijawahi kumuona naishia kusoma hadithi zake tu, mm binafsi namkubali mtu mmoja tu aliyebadili fikra za ulimwengu kuupenda mpira wa miguu. Anaitwa GAUCHO kwelj nimeamin one man can change the world by big sean
 
Mi naamini zamani kulikuwa na mabeki kuliko hivi sasa
Kwangu mimi sioni beki ninaeweza nikasema anajua kukaba
Rio ndio kabisaa hamna kitu
 
We team inafungwa goli 5 sasa hivi utaniambia kuna mabeki
Zamani hiyo kitu haikwepo sana
Timu ipi imefungwa tano na imefungwa na nani?? Mbona rekodi inaonyesha Czechslovakia na Hungary zilikuwaga zinawapa watu visago vya saba bila enzi hizo?? Mabeki hao walikiwa wapi??
 
Mpira ulikuwa wa kibabe wachezaji mashahuri walikuwa hawalindwi kama sasa hivi ilikuwa mbadembade. Tunavyo mzungumzia Pele ni ngumu kutuelewa namna mpira ulivyokuwa na umepita katika vipindi gani. Leo ukitaja enzi za miaka ya sitini utaambiwa ilikuwa enzi ya Pele japo palikuwa na wachezaji wengine mahiri kama Eusebio (mkuu )kina jack na bobby Charlton huku Hungary wakiwa na ferenc puskas lakini bado nyota ya Pele iling'aa achilia mbali hapo hapo brazil walikuwapo wakali kama garrincha tostao akina revelino Didi Carlos Alberto na wengineo. Kikaja kizazi cha sabini hiki kilihusisha johan cruffy nae alikuwa na waqt wake ingawa nyota wengine kama gurd muller akina sapp meir na wengine wengi. Kisha zikaja zama za 80 hizi zilikuwa za Diego ingawa kulikuwa na manguli wengi kina Karl heinze rumminiga na kina claudio canigia lakini nyota ya Diego iling'ara .
 
Watu hamko makini pele angeenda ulaya kipindi kile kutafuta nini alikuwa analipwa pesa nyingi akiwa kwao, kuna kipindi alikuwa ni athlete anaelipwa zaidi duniani, ilikuwa rahisi zaidi pele kubaki kwao kipindi hiko ulaya si lolote, can you imagine kama uefa champions tu ilianzishwa kwa kugeza idea ya copa sudamericano campeonese de campion, sasa ulitaka pele aende ulaya akafanye nini, kina neymar ndio kizaz cha kukimbilia ulaya wamenyanyasika na kina barcelona, wamekuta ligi haina lolote, hakuna mtu anaelipwa zaid japo ni ligi ya 4 ama ya 5 kwa ugumu duniani, pele katika international cup aliwagaragaza vibaya miamba ya ulaya benfica, ac milan sijui takataka gani alikuwa akikutana nazo anafunga alichukua internationa cup mara kadhaa, leo nani brazil au timu nje ya ulaya inawin kombe la dunia kwa vilabu..

Pili pele katika mwaka 58/59 bunge la brazil lilimpitisha na raisi kutia saini wakimchukulia pele as a national treasure kumlinda asisafirishwe nje ya taifa, labda kama pele humjui vizur mkuu.

Unazungumzia mabeki wagumu, [emoji23] [emoji23] [emoji23] unanichekesha mkuu kuna mabeki wabishi kama kipindi hicho, refer kile walichomtendea pele 1966 pale uingereza mpaka akaapa kutokuja kucheza kombe la dunia kiasi cha kubembelezwa mwaka 70 fainali za mexico ndio wakaintroduce kadi nyekundu na njano, labda humjui pele vizur..


 
Acha masihara mkuu nadhani pele hujamfatilia vizur mie nimepoteza muda wangu kumtizama pele baada ya kuwa nimemshuhudia messi, niliamin messi ni namba moja, ila baada ya kumfatilia pele, messi na maradona nikaona pele hana mpinzani hata kidogo..

1.Pele
2.Messi
3.Maradona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…