Nonsense! Pele mwenyewe hajawahi kucheza soka ulaya. Kwa ubora wake alitakiwa angalao avae hata jezi za sporting lisbon au hata porto achilia mbali Barcelona na Real Madrid. Hajakutana na mabeki wenye roho mbaya kama Nigel de Jong au Frank Lebouf. Yeye alikuwa anapiga watu chenga wanamwachia tu.
Btw kwa mujibu wa matokeo ya kumtafuta mchezaji bora wa karne aliyeibuka mshindi sio pele. Hapa aliibuka Diego Armando Maradona. Fifa kwa fitna zao wakasema tuzo wapewe wote Maradona na Pele. Kwa madai kwamba Maradona ndani ya uwanja kwwli alikuwa nyoko ila nje ya uwanja alikuwa ni mtovu wa nidhamu mla madawa nk
Wakati wakikabidhiwa tuzo Maradona alisema NIPO HAPA KUPOKEA TUZO HII NILIOPEWA NA WAPENDA SOKA KOTE ULIMWENGUNI, NA SIPO TAYARI KUSHEA NA MTU MWINGINE. HII NI YANGU PELE MTAFUTIENI YA KWAKE.