MFAHAMU GWIJI LA MCHEZO WA MPIRA DUNIANI
Edson Arantes do Nascimento( PELE)
Alizaliwa tarehe 23 oktoba 1940, anatajwa kama mchezaji wa bora wa vipindi vyote katika historia ya mchezo wa soka.
Mwaka 1999, alipigiwa kura na kuwa “mchezaji bora wa karne” na Shirika la International Federation of Football History and Statistics (IFFHS), mwaka huo huo pele alichaguliwa kuwa mwanamchezo bora wa karne na International Olympic Committee.
Kwa Mujibu wa taarifa za IFFHS , pele ni mchezaji aliyefanikiwa sana kuliko mchezaji yoyote duniani toka mchezo wa mpira uanze, alicheza michezo 1363 na kufunga magoli yapatayo 1281, ambayo huusisha michezo ya kirafiki na mashindano.
Kipindi anacheza mpira ,ndiye mchezaji aliyekuwa analipwa pesa nyingi kuliko mchezaji yeyote duniani.
Pele kaanza kucheza soka, katika klabu ya santos nchini brazil akiwa na umri wa miaka 15 tu na kuanza kucheza timu ya taifa la brazil akiwa na umri wa miaka 16 tu.
Katika mashindano ya kombe la dunia , ameshinda Vikombe vitatu katika miaka ya 1958,1962 na 1970 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee duniani kufanya hivyo.
Pele ni mchezaji pekee wa brazil aliyefunga magoli mengi katika timu ya taifa ,kwa kufunga magoli 77 katika michezo 92.
Pele anafahamika kwa kuwa mchezaji mwenye uwezo wa kuchezea mpira,kufunga magoli na kuleta burudani ya soka awapo uwanjani, kwa brazil anafahamika kama shujaa wa taifa.
Mwaka 1957 ,alipoanza kuchezea klabu ya santos ,alimaliza msimu akiwa mfungaji bora akiwa na miaka 16 tu.
Baada ya kipaji chake kuwa tishio duniani katika soka , vilabu vikubwa vya ulaya kama Real Madrid,juventus,ac Milan ,Manchester united walianza kumsaka ili wamsajili.
1962 , ,bunge la brazil lilitunga sheria ya kumtambua kama “ National treasure” (hazina ya taifa), chini ya rais wa brazil enzi hizo aliyeitwa janio Quadros na hatimaye ilitangazwa rasmi na hivyo kumzuia kusajiliwa na timu za ulaya.
Mwaka 1962, baada ya timu ya benfica kucheza na santos na kufungwa katika mchezo huo na pele , kipa wa timu ya benfica aitwaye Costa Pereira alisema maneno
haya “ Nilipofika nilikuwa na matumaini ya kumzuia mchezaji mkubwa duniani , lakini wakati wa mchezo na mchezo kuishi niligundua kuwa nilijidanganya kufikiri hivyo,kwani niligundua pele hajazaliwa katika sayari ya dunia kama sisi”
Mwaka 1969,pele alifunga goli lake la 1000 katika mashindano yote, goli hili lilifungwa katika mchezo wa klabu yake santos dhidi ya klabu ya vasco da gama, katika uwanja wa maracana.
Mwaka 1967,pele alicheza nchini Nigeria kama mechi ya kusitisha mapigano ya vita ya kikabila nchini Nigeria.
Mwaka 1974, pele alistaafu soka katika klabu za brazil, japo aliendelea kualikwa kucheza mechimuhimu tu, miaka miwili baadaye , alisaini na timu ya nje na brazil ambayo ni new york cosmos ya marekani, alikwenda kucheza marekani kwa lengo la kuhamasisha mchezo wa mpira nchini marekani.
Mwaka 1977,Oktoba Mosi, pele alistaafu kucheza mpira kwa kucheza mchezo kati ya timu yake mpya ya new york cosmos na santos ,mchezo ambao ulishuhudiwa na mwana masumbwi mkubwa duniani ,muhamad ali , bobby moore pamoja na baba na mke wake.
Mwaka 1958, katika kombe la dunia lilichezwa nchini Sweden, alikuwa ni mchezaji mdogo katika historia ya kombe la dunia, katika mashindano hayo aliweka rekodi ya kufunga hat-trick akiwa na umri mdogo katika historia ya kombe la dunia, siku ya fainal na Sweden ,pele alifunga magoli mawili kati ya matano yaliyofungwa, goli lake la kwanza katika fainali hizo liliwekwa katika kumbukumbu ya FIFA ya kuwa goli bora katika historia ya kombe la dunia hadi leo. Pia mwaka 1958 ndio mwaka pele alianza kuvaa jezi namba 10, namba yenye heshima hadi leo, Mwaka 1958 ndio mwaka brazil inachukua taji lake la kwanza la kombe la dunia chini ya kipaji cha pele.
Mwaka 1959, katika mashindano ya SOUTH AMERICA CHAMPIONSHIP, pele alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.
Mwaka 1962,pele anaiwezesha brazil kuchukua kombe la dunia kwa mara ya pili, mashindano yalifanyika nchini chile.
Mwaka 1966, mashindano ya kombe la dunia yalifanyika nchini uingereza, na brazil ilikuwa na kikosi hatari chenye wachezaji Nguli kama , golikipa Gilmar, wachezaji kama garrincha,djalma santos,jairzinho,tostao na gerson. Katika mashindano haya brazil ilitolewa raundi ya kwanza kwa kucheza mechi tatu tu ,baada ya pele kuchezewa faulo mbaya ,katika mchezo wa brazil dhidi ya Bulgaria ,japo alichezewa faulo aliwezesha brazil Kushinda mchezo huo, lakini ilipeleke , kukosa mchezo wa pili dhidi ya hungary ambao brazil ilipoteza, mchezo wa tatu dhidi ya ureno alicheza hivyohivyo kuokoa jahazi japo alikuwa bado majeruhi, lakini pia alipigwa faulo mbaya na beki wa ureno aitwaye joao morais , pele alilia sana japo huyo beki hakutolewa nje na refarii aitwaye George McCabe, kwa Mujibu wa sheria za kipindi hicho ilibidi asalie uwanjani akiwa dhaifu bila kucheza hadi mchezo ulipoisha, kwani mabadiliko(subsititute) yalikuwa hayaruhusiwi, baada ya mchezo huu pele aliapa kwa kusema
“ hatocheza tena kombe la dunia” lakini baadaye alibadili maamuzi baada ya kushauriwa sana na akarudi mashindano ya 1970.
Mwaka 1970, pele alishiriki mashindano ya kombe la dunia yaliyofanyika nchini mexico , na ndio yalikuwa mashindano ya Mwisho ya pele kucheza kombe la dunia , na kikosi cha brazil cha mwaka 1970 ,katika FIFA ndio kinahesabiwa kuwa kikosi bora zaidi duniani kuwahi kutokea, kikosi hiki kilikuwa na wachezaji kama pele,rivelino,jairzinho,gerson,carlos alberto torres,tostao na clodoaldo.
Brazil ilicheza fainali na Italy katika uwanja wa Azteca katika jiji la mexico, brazil ilishinda 4-0 na kufikia rekodi ya kuchukua kombe la dunia kwa usaidizi wa pele na katika mashindano hayo hayo pele alinyakua kiatu cha dhahabu.
Mashindano ya 1970 yanakamilisha historia ya pele kombe la dunia , amecheza misimu minne na kuchukua misimu Mitatu , msimu mmoja wa 1966 hakuiwezesha brazil kuchukua sababu ya kuwa majeruhi.
Burgnich , mchezaji wa Italy baada ya fainali alisema maneno haya
“nilijisemea mwenyewe kabla ya mchezo kuwa,ameumbwa kwa ngozi na mifupa kama sisi, lakini baada ya mechi alisema sikuwa sahihi maana pele ni kiumbe wa sayari nyingine sio kama sisi”
Mechi ya Mwisho ya kimataifa pele akiwa na timu ya brazil alicheza mwaka 1971, julai dhidi ya Yugoslavia huko rio di janeiro, katika historia ya soka duniani na brazil ,takwimu zinaonesha pele ameshinda michezo 67,droo mechi 14 na kupoteza mechi 11. Na villevile mechi zote alizocheza pele na garrincha kwa dakika 90 ,hakuna mechi yoyote waliyowahi kupoteza miamba hao wawili.
Pele anaingia katika rekodi za Nguli,gwiji la mpira toka mchezo huo uanze kwa kuwa na staili ya pekee katika uchezaji ,kwa kuwa na vitu vyote kama spidi,ubunifu,mbinu za mpira,nguvu,stamina ,kukimbia ,chenga ,kupiga vichwa , ku dribble n.k kitu ambacho hakuna na hajatokea mchezaji mwenye uwezo kama wake , kudhihirisha hilo FIFA wameanza kuachia video za mambo aliyofanya pele uwanjani toka mwaka 1958, ambayo ni marudio kwa wachezaji wa kizazi hiki kama kina zidane, gaucho ,Ronaldo de lima, christain Ronaldo,messi ,maradona n.k
Pele ni mchezaji anayetajwa sana na hakuna mfanowe katika historia ya mpira na mara kwa mara amekuwa kinara wa mchezo wa mpira duniani, akitajwa na Nguli mbalimbali wa mpira katika zama tofauti tofauti,
Mifano ya Nukuu za wachezaji Nguli mbalimbali waliocheza na pele au kumshuhudia ,
Johan cruyff, Nguli wa mpira kutoka uholanzi alisema
“ pele ni mchezaji pekee wa mpira aliyewashangaza wengi tofauti na walivyofikiri kabla ya kumuona akicheza”
Carlos arbeto torres ,nahodha wa brazil mwaka 1970 baada ya kombe la dunia alisema
”pele siri yake kubwa ilikuwa ubunifu, hivyo vitu vyote alivifanya kwa wakati mmoja na muda mfupi, hakika sio binadamu wa kawaida katika mpira”
Clodoaldo ,Nguli wa mpira brazil anasema
“nimecheza na pele timu moja na nimemshuhudia katika uwanja ana kipaji cha ajabu sana na kuna nchi wanatamani kumshika,wengine kumpinga busu na wengine kupiga busu alipokanyaga”
Ferenc Puskas , mchezaji wa Zamani wa klabu ya brazil na timu ya taifa ya hungary anasema
“mchezaji bora wa kihistoria alikuwa Di Stefano, lakini nakataa kusema pele alikuwa mchezaji , huyu alikuwa juu ya yote hivyo hana wa kufananishwa naye”
Just Fontaine,mshambuliaji wa ufaransa na mfungaji bora kombe la dunia 1958, anasema
“siku nilipomuona pele anacheza , ilinifanya nijihisi kutundiga daruga na kustaafu mpira kwani yule hakuwa binadamu wa kawaida”
Bobby Moore, kapteni wa uingereza kombe la dunia mwaka 1966 anasema
“pele alikuwa ni mchezaji aliyekamilika kila idara ambaye sijawahi kumuona katika maisha yangu ya kucheza mpira na baada ya kustaafu mpira” nakumbuka nilimuuridha kocha saldhana aliulizwa na waandishi habari wa brazil , Je ni nani kipa bora katika timu yake , kocha alijibu ni PELE.,
Bobby Chalton ,Nguli wa soka Manchester united na mmoja wa wachezaji waliochukua kombe la dunia 1966 wakiwa na timu ya uingereza anasema
“mara kadhaa nafikiri mchezo wa mpira ,ulivumbuliwa kwa ajili pele tu”
Mwaka 1970, kipindi cha kombe dunia, mtangazaji wa mpira katika luninga huko uingereza alimuuliza Bobby Charlton , je ni namna gani? Unatamka neon Pele , Majibu yalikuwa rahisi tu pele ni MUNGU wa mpira.
Frank beckenbaur ,kapteni wa ujerumani kombe la dunia mwaka 1974, alinukuliwa
akisema “pele ni mchezaji bora wa nyakati zote , ametawala soka kwa miaka 20 yote aliyocheza soka na kuwa juu ya wote kama Diego Maradona, Johan Cruyff, Michel Platini – hawa wote huwezi walinganisha na pele kawazidi mbali mno.
Andy Warhol
anasema “pele alikuwa ni baadhi ya watu wachache wanaonichanganya katika Nadharia zangu , badala ya kuwa na umaarufu wa dakika 15 , yeye hufanya kuwa wa karne 15.
" Jina langu ni Ronald Reagan , ni rais wa marekani ,lakini wewe huitaji kujitambulisha sababu kila mtu duniani anajua wewe ni nani pele, hii ilikuwa ni salam za kumkaribisha pele ikulu ya marekani.
Baadhi ya Makombe na mataji aliyotwaa pele
1. Kimataifa
.kombe la dunia vikombe 3
.roca cup vikombe 2
.Cruz cup vikombe 3
.bernardo O Higgins Cup kombe 1
.atalntic cup kombe 1
2. Klabu
.Santos –jumla ya Vikombe 24
·
Campeonato Paulista (10):
·
Torneio Rio-São Paulo (4):
·
Campeonato Brasileiro Série A (6):
·
Copa Libertadores (2):
·
Intercontinental Cup (2
New York Cosmos
Jumla ya Vikombe 2
·
North American Soccer League,
Soccer Bowl:
·
North American Soccer League, Atlantic Conference Championship:
Mataji ya ufungaji bora
·
Santos
·
Copa Libertadoreser:
1965
·
Campeonato Paulista (11): 1957, 1958, 1959, 1960, 1961, 1962, 1963, 1964, 1965, 1969, 1973
·
Torneio Rio-São Paulo : 1963
·
Bola de Prata: 1970
·
Brazil
· Mchezaji bora kijana kombe la dunia: 1958
· Mchezaji bora kombe la dunia (kiatu cha dhahabu): 1970
·
Copa America mchezaji bora:
1959
·
Copa América mfungaji bora:
1959
· Mataji mengine
·
FIFA Ballon d'Or Prix d'Honneur:
2013
·
Ballon d'Or (7): 1958, 1959, 1960, 1961, 1963, 1964, 1970 -
Le nouveau palmarès (the new winners)
· Mchezaji wa karne (FIFA): 2000
Mataji ni mengi ila nimeleta baadhi tu ili kumtambua huyu gwiji wa mpira ambaye , hajawahi tokea toka mchezo wa mpira uanze.
Huyu ndiye baba wa mpira duniani kwa kifupi au jina la utani tunamuita PELE.