Tukubali au tukatae kwenye hii sayari ya Dunia katika nyanja ya Soka hakuna kama Pele wa Brazil

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
Hat-trick 92 maisha yake yote
Mabao 4 mara 36 maisha yake yote
Mabao 5 mara 6 maisha yake yote
Mabao 8 mara 1 maisha yake yote

Miguu yake yote ilifunga magoli yasiyo na idadi
Kichwa chake kilifunga magoli yasiyo na idadi
Alikuwa na chenga ambazo aliemzidi ni garincha tu
Alikuwa na kasi ya sunami uwanjani
Ndiye mchezaji aliefunga bao bora kuwahi kitokea duniani santos vs juventus

Amecheza match 1385 katika maisha yake yote ya mpira kuliko mchezaji yeyote

Amefunga mabao 1280 katika maisha yake yote ya soka kuliko mchezaji yeyote

Bao lake la 1000 alifunga kwa penalty na mashabiki waliingia uwanjani kusherekea bao hilo kitu kilichopelekea mpira kusimama kwa nusu saa kuwaondoa watu uwanjani

Alianza soka la kulipwa akiwa na miaka 15 tu
Na hat-trick yake ya kwanza alifunga akiwa na miaka 15 mwaka 1956

Brazili haijawahi kupoteza match pele akiwa uwanjani

Takwimu ndio kila kitu zaidi ya hapo ni kudanganyana tu

Jamaa amechezea team 2 tu maisha yake yote huku akitumia muda wake mwingi santos

Fifa wanamtaja kama mchezaji bora kuwahi kuonekana duniani mpaka leo

Ni mchezaji pekee katika hii dunia alietwaa kombe la dunia mara tatu huku akiwa tegemeo kubwa kwa taifa lake la brazili
Mchezaji pekee aliekuwa akiumia mchezoni mashabiki wake wanamlilia mpaka arudi uwanjani

Na huyo ndiye mfalme wa kandanda duniani PELE
 
Hata kama hujamuona kumbukumbu zipo nyingi tu
Siku nyingine ukitaka kuandika kuhusu nguli huyu anza hivi "edson arantes do nascimento (Pele wa brazil )
Nb:mengine yote umekokotoa uzuri mtu huyu alie fanya watu waupende mpira mpaka ikafika mtu hata katika maisha ya kawaida ukifanya kitu kizuri basi unaambiwa "umecheza kama Pele "
 
Nonsense! Pele mwenyewe hajawahi kucheza soka ulaya. Kwa ubora wake alitakiwa angalao avae hata jezi za sporting lisbon au hata porto achilia mbali Barcelona na Real Madrid. Hajakutana na mabeki wenye roho mbaya kama Nigel de Jong au Frank Lebouf. Yeye alikuwa anapiga watu chenga wanamwachia tu.

Btw kwa mujibu wa matokeo ya kumtafuta mchezaji bora wa karne aliyeibuka mshindi sio pele. Hapa aliibuka Diego Armando Maradona. Fifa kwa fitna zao wakasema tuzo wapewe wote Maradona na Pele. Kwa madai kwamba Maradona ndani ya uwanja kwwli alikuwa nyoko ila nje ya uwanja alikuwa ni mtovu wa nidhamu mla madawa nk

Wakati wakikabidhiwa tuzo Maradona alisema NIPO HAPA KUPOKEA TUZO HII NILIOPEWA NA WAPENDA SOKA KOTE ULIMWENGUNI, NA SIPO TAYARI KUSHEA NA MTU MWINGINE. HII NI YANGU PELE MTAFUTIENI YA KWAKE.
 
Hat-trick 92 maisha yake yote
Mabao 4 mara 36 maisha yake yote
Mabao 5 mara 6 maisha yake yote
Mabao 8 mara 1 maisha yake yote

Miguu yake yote ilifunga magoli yasiyo na idadi
Kichwa chake kilifunga magoli yasiyo na idadi
Alikuwa na chenga ambazo aliemzidi ni garincha tu
Alikuwa na kasi ya sunami uwanjani
Ndiye mchezaji aliefunga bao bora kuwahi kitokea duniani santos vs juventus

Amecheza match 1385 katika maisha yake yote ya mpira kuliko mchezaji yeyote

Amefunga mabao 1280 katika maisha yake yote ya soka kuliko mchezaji yeyote

Bao lake la 1000 alifunga kwa penalty na mashabiki waliingia uwanjani kusherekea bao hilo kitu kilichopelekea mpira kusimama kwa nusu saa kuwaondoa watu uwanjani

Alianza soka la kulipwa akiwa na miaka 15 tu
Na hat-trick yake ya kwanza alifunga akiwa na miaka 15 mwaka 1956

Brazili haijawahi kupoteza match pele akiwa uwanjani

Takwimu ndio kila kitu zaidi ya hapo ni kudanganyana tu

Jamaa amechezea team 2 tu maisha yake yote huku akitumia muda wake mwingi santos

Fifa wanamtaja kama mchezaji bora kuwahi kuonekana duniani mpaka leo

Ni mchezaji pekee katika hii dunia alietwaa kombe la dunia mara tatu huku akiwa tegemeo kubwa kwa taifa lake la brazili
Mchezaji pekee aliekuwa akiumia mchezoni mashabiki wake wanamlilia mpaka arudi uwanjani

Na huyo ndiye mfalme wa kandanda duniani PELE
Rekodi yangu kuanzia chekechea mpaka la saba shule ya msingi ni zaidi ya hii ya Pele.
Jamaa alikuwa yeye kijana alafu anacheza na wazee.
 
Kwangu pele ni nambari 1, nimemfuatilia huyu mtu alikuwa hatari

1. Pele
2. Messi
3. Maradona
Messi ni zaidi ya Pele. Sidhani kama Pele angekatiza mbele ya Rio Ferdinand ktk ubora wake.
Pele hamna kitu, alicheza na MIZEE enzi hizo alafu mpira wake hata kwa kuuangalia haina mvuto wowote. Anabebwa sana huyu jamaa. Maradona pia kamuacha mbali sana Pele.
 
Ndiye mchezaji aliefunga bao bora kuwahi kitokea duniani santos vs juventus

Hapo red goal of century alifunga Diego Maradona. Nusu fainal kombe la dunia 1986 kule mexico dhidi ya chamdomo England. Alipiga chenga mabeki wa5 kabla ya kumrudia beki mwingine na kumfunga Peter Shilton

Fifa wanamtaja kama mchezaji bora kuwahi kuonekana duniani mpaka leo
Sio kweli. Tuzo ya mchezaji bora wa karne alipewa na wapenzi wa soka duniani na kukabidhiwa na fifa wakimshirikisha Pele ambaye alishindanishwa na kubwagwa na Maradona.
 
Nonsense! Pele mwenyewe hajawahi kucheza soka ulaya. Kwa ubora wake alitakiwa angalao avae hata jezi za sporting lisbon au hata porto achilia mbali Barcelona na Real Madrid. Hajakutana na mabeki wenye roho mbaya kama Nigel de Jong au Frank Lebouf. Yeye alikuwa anapiga watu chenga wanamwachia tu.

Btw kwa mujibu wa matokeo ya kumtafuta mchezaji bora wa karne aliyeibuka mshindi sio pele. Hapa aliibuka Diego Armando Maradona. Fifa kwa fitna zao wakasema tuzo wapewe wote Maradona na Pele. Kwa madai kwamba Maradona ndani ya uwanja kwwli alikuwa nyoko ila nje ya uwanja alikuwa ni mtovu wa nidhamu mla madawa nk

Wakati wakikabidhiwa tuzo Maradona alisema NIPO HAPA KUPOKEA TUZO HII NILIOPEWA NA WAPENDA SOKA KOTE ULIMWENGUNI, NA SIPO TAYARI KUSHEA NA MTU MWINGINE. HII NI YANGU PELE MTAFUTIENI YA KWAKE.
Kama alikuwa kilaza aliwezaje kutwaa kombe la dunia mara tatu? Hao kina messi walishatwaa mara ngapi ? Kwasababu wao wanacheza ulaya?
 
Naomba kujua kama tangu ujue soka hasa la majuu. Ulishawahi kusikia mchezaji yeyote nafananishwa na Pele?

Utasikia. New Maradona
New Christiano Ronaldo
New Gaucho nk

Huwezi kusikia new pele...
 
Back
Top Bottom