Tukubali tu: Sisi wajinga... (I know, it hurts)

Kwa level ya digrii ya kwanza na entry level position (yaani wote wametoka shuleni bila kuwa na uzoefu wa kazi). Kwa wastani Mhandisi wa Tanzania atakuwa amechimba sana kuliko yule wa Marekani. Sasa swali lako hapa ni lipi?

Sasa kama wasomi wetu "wamechimba" sana kuliko wa Ulaya na Marekani (ingawa ma theory na mavitabu wanayotumia mengi yametungwa na kuandikwa na wazungu) sasa kwa nini sisi hatuendelei?
 
Kwa level ya digrii ya kwanza na entry level position (yaani wote wametoka shuleni bila kuwa na uzoefu wa kazi). Kwa wastani Mhandisi wa Tanzania atakuwa amechimba sana kuliko yule wa Marekani. Sasa swali lako hapa ni lipi?

Mhn..Mkuu weka data!
 
Sasa kama wasomi wetu "wamechimba" sana kuliko wa Ulaya na Marekani (ingawa ma theory na mavitabu wanayotumia mengi yametungwa na kuandikwa na wazungu) sasa kwa nini sisi hatuendelei?

Huku Nyani huwa una data!

Ila kule wewe na Mc Cain mshanichosha!
 
Kwa level ya digrii ya kwanza na entry level position (yaani wote wametoka shuleni bila kuwa na uzoefu wa kazi). Kwa wastani Mhandisi wa Tanzania atakuwa amechimba sana kuliko yule wa Marekani. Sasa swali lako hapa ni lipi?

swali langu ni kuwa kama wote wamesoma sawa au zaidi (nikichukukulia maneno yako at face value) ni kitu gani kinaweza kuwafanya wanapokuja kwenye utendaji wa kwetu wanaonekana hawawezi kufanya jambo wao wenyewe kwa kina na manufaa ya nchi na tukimleta mhandisi kama wao kutoka nje akaonekana kufanya kazi zaidi? Na hapa najaribu kufikiria wale vijana wa Kijapa waliokuwa na Konoike wakati wa kutengeneza barabara ya Mbeya...
 
Sasa kama wasomi wetu "wamechimba" sana kuliko wa Ulaya na Marekani (ingawa ma theory na mavitabu wanayotumia mengi yametungwa na kuandikwa na wazungu) sasa kwa nini sisi hatuendelei?


Nilicho observe personally ni kuwa sisi "tunachimba" sana kwa kutumia msuli, tunapapasa mitabu mingi sana, hatuhurumiani, tunapigana ma disco sana, kiasi kwamba tunatengeneza ma academicians waliobobea katika nadharia.

Wenzetu wanaweza wasifanye kazi sana kama sisi bali wanafanya yaliyo muhimu.Kwa mafano, kipindi kirefu kidogo kilichopita nikiwa primary nilipata kukaa na mtoto wa IST nikataka kujua wanavyofundishwa.Tukaanza kuulizana, formulaes tukafikia formulae ya kupata eneo la duara, mwenzangu akanipa formulae na historia ya formulae ilivyopatikana na kwa nini pi ni 22/7, basi mimi nilibaki mdomo wazi kwamba siku zote nimekuwa nikitumia pi kama 22/7 kama a given constant, wala mwalimu hakuniambia hii pi imetoka wapi na kwa nini ikawa 22/7.

In other words, elimu "yetu" ni mechanical zaidi, iko based kwenye kurudia kitu kile kile bila kikichunguza zaidi na iko canonical zaidi.

Wenzetu wanaenda kwenye mizizi ya vitu na hata hivyo vitu "vidogo" au visivyo "vigumu" wanavyosoma mitaala yao inawataka wavisome deeply.

Ukiwa na elimu hii canonical, huwezi kuwa adaptive au innovative, utataka kila kitu kije kama textbook examples ulizozizoea, which is hardly the case.

Ukijifunza the underlying principles (kama vile kwa nini pi ikawa 22/7) sio tu unaweza kuwa adaptive, unaweza hata ku design vitu vya kuwezesha a breakthough in the next paradigm.
 

Tanzania na Afrika kwa ujumla practical ni lesser than nadharia and so tuna watu smart wa vitabu lakini translation together with implementation ime prove kuwa poor!

Watu huwa wana crame na hawajui ni kwa namna gani kisomo chao kiko applicable kwenye real life!

Na hii nafikiri ni kutokana na ukweli kuwa we are far behind kimaendeleo!
 

Kumbe na mimi nilikuwa na type the same thing!
Pundit we always share the same ideas...Tutafutane mkuu!
 

Nionavyo mimi ni kwamba tutaimba sana kuhusu hiyo competency lakini mwisho wa siku hakutokuwa na mabadiliko iwapo tu hawa local contractors, either hawapewi ushirikiano wa kutosha ama hawawezeshwi kwa njia moja au nyingine kuongeza ujuzi na pia kujenga uwezo wa kiushondani na makampuni ya ujenzi toka nnje.
Ukiangalia kwa mfano suala la mitaji, makampuni mengi ya wenzetu yana access na mikopo mikubwa ambayo huweza kuwajenga wao kiutaalam, ikiwa ni pamoja na kuwa na zana za kutosha katika kufanikisha kazi zao, kitu ambacho makampuni yetu mengi hayana. Kama tunatoa kandarasi hizi katika nia safi ya kuinua ushindani basi kwa nini tusiwawezeshe hawa makandarasi local wafikie uwezo huo wa kushindana ili hela angalau iweze kubakia nchini? Kama tunahisi kwamba uwezo wao ni duni kwa nini tusiweke masharti ya kuwabana makandarasi wa nnje ili wanapotafuta miradi basi lazima wawe na local partners ili kuhakikisha kwamba hawa local partners wanajifunza na kupata huo uwezo wakiushindani progressively. Ni kweli kwamba tunapong'ang'ania ushindani kwa kukumbatia makampuni ya nnje..mihela yote hiyoo inarudi ulaya mwishowe tunashindwa kukusanya mapato ya kutosha na kuishia kuomba tena misaada...kama mihela hii ingekuwa inalipwa kwa makandarasi wa ndani ..nadhani tungefaidika kwa mambo mengi sana, ikiwa ni pamoja na ongezeko la ajira na bajeti tegemezi..Kweli utaendelea kumuachia jirani akuvishie mkeo mpaka lini..mwishowe si ndo...ivo..?
 

Pundit,
Lakini elimu yetu si imeundwa kufanana na ile ya Uingereza? Au nimekosea hapa?
 


Mkuu MJJ hapa chini Mkuu Pundit naona ameto jibu lako....sisi twabukua na kucram(kasuku)



 
Pundit,
Lakini elimu yetu si imeundwa kufanana na ile ya Uingereza? Au nimekosea hapa?

Elimu iliyobadilishwa na kina Mungai na Mama Sita kama wanabadilisha viatu? Elimu inabadilishwa kuliko cabinet ya Kikwete, nayo elimu?

Sie katika pride ya nationhood tumetupa hata yale mazuri ya west.
 

Swali zuri sana:

Katika ufundi au uhandisi, taaluma moja ina matawi mengi. Kama ni Civil, kuna road construction, majumba, madaraja, reli, tunnels na mambo mengi ambayo kwa wasiosomea fani za uhandisi hawazioni.

Hivyo shule inajaribu kumpa mhandisi nadharia matawi yote lakini sio uzoefu wa kazi (experience). Hivyo kuwa na elimu nzito ya shule haikusaidii wewe kuwa mhandisi mzuri iwapo huna experience.

Kuna uwezekano mkubwa fundi wa Konoike ana uzoefu wa zaidi ya project tano kubwa za ujenzi wa barabara tofauti kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Kitu kingine ni kuwa, miaka mingi isiyopita graduates wa kitanzania walikuwa wanamaliza na kwenda kushika nafasi za uongozi. Kuwa afisa wa ujenzi wa wilaya au Mkoa. Na kwa mtaji huu ni wachache sana walioweza kufanya kazi za pamoja za kwenye projects ambazo ndizo zinazokupa uzoefu.

Vilevile Konoike ni kampuni la biashara (BIZNIS). Hivyo mafanikio ya Mhandisi wa Konoike sio yake. Mara nyingi ni mafanikio ya mfumo mzima wa Biashara wa kampuni ya Konoike. Hivyo wajapan wa Konoike waliweza kuacha kazi na kurudi kwao na wahandisi wengine kuchukua nafasi zao bila kuteteleka kitu.

Tanzania tulikuwa na Kampuni ya MECCO. Hii ilikuwa ni Kampuni ya biashara. Kampuni hii haikufanikiwa sio kwa matatizo ya wahandisi kutokuwa na taaluma bali ubaya wa BIZNIS model.

Ukiwa na BIZNIS model nzuri taaluma itashuka tu na tumeona mara nyingi makampuni ya kigeni yakichukua wahandisi wa kikwetu kufanya kazi nao na bila kulalamika.

Swali la kujiuliza kwanini Mhandisi wa kitanzania ana-fit katika BIZNIS model ya kampuni la kigeni na sio kampuni la kizawa?
 
Sasa kama wasomi wetu "wamechimba" sana kuliko wa Ulaya na Marekani (ingawa ma theory na mavitabu wanayotumia mengi yametungwa na kuandikwa na wazungu) sasa kwa nini sisi hatuendelei?

Ngabu nitakujibu nikifika nyumbani ngoja nimalizie mabox.
 
Mkuu Pundit,
Mungai na Mama Sitta si wamekuja juzi juzi tu hapa? Mwanakijiji ameongelea Konoike...na kama kumbukumbu zangu zinanitendea vyema hawa Konoike walikuja baada ya Kajima...nadhani mwaka '85. Kwa nini wahandisi wetu na makampuni yetu hayakujenga hiyo miundombinu hadi tukawaajiri hawa Wajapenga? Sidhani kama Mungai na Mama Sitta walikuwa mawaziri wa elimu kipindi hicho. Natambua kwamba elimu ya msingi ni muhimu lakini hapa si tunazungumzia elimu ya juu (chuo kikuu)?
 

Tanzania na Afrika kwa ujumla practical ni lesser than nadharia and so tuna watu smart wa vitabu lakini translation together with implementation ime prove kuwa poor!

Watu huwa wana crame na hawajui ni kwa namna gani kisomo chao kiko applicable kwenye real life!

Na hii nafikiri ni kutokana na ukweli kuwa we are far behind kimaendeleo!
 
KWANINI KABLA HATUJA CONCLUDE KUWA SISI NI WAJINGA TUSI ZINGATIE HAYA YA ALIYEWAHI KUWA MWANASHERIA MKUU..JAJI SINDE WARIOBA NA WENGINEO?
UJINGA UKO KWENYE UTAMBUZI WA VIONGOZI WAZALENDO?



ehe mambo magumu. kweli watanzania tu wajinga lakini nyie mnaosoma ulaya miaka nenda rudi bila kuhitimu ndio wajinga zaidi kwani hamna kitu mnachangia hapa zaidi ya kuleta usanii kwenye mambo mazito. Malizeni digirii zenu mrudi nyumbani kama kweli mnataka kuleta mabadiliko maana hii forum wengi wenu ni wazamiaji mko ulaya hata hamjui kinachoendelea bongo. Wengine mko miaka nane hata digrii ya kwanza hamjapata sijui mnategemeaje kuleta mabadiliko hapa bongo. Tunachoka na porojo zenu rudini nyumbani wana wapotevu nyie.
 
:
Swali la kujiuliza kwanini Mhandisi wa kitanzania ana-fit katika BIZNIS model ya kampuni la kigeni na sio kampuni la kizawa?

Kwanza kabisa Tanzania tunayo ile tabia kuwa kila mtanzania ni ndugu yako ndivyo hulka yetu tofauti na jiarani zetu wa Kenya Uganda Malawi n.k...ukiangalia utendaji na ufanisi wetu unakuwa mdogo sana tunapo fanya kazi katika kampuni zeu za wazawa kwa sababu at the end of day nobody will fire you.
 


Bin Maryam kaongea vizuri kuhusu mfumo wa elimu na mfumo wa kiuchumi kuenda bega kwa bega, utajifunza computer science all you want with your textbooks, lakini kama huna computer ya kufanyia projects/prcatice utatoka hapo mtupu hata ki script kiddie cha high school kitakutoa nishai.Mimi nataka kuongezea a cultural dimension hapa.

Sasa sisi tulikuwa tunafundishia mibuku mambo ya engineering kama ungwini vile, kisa hatuna mfumo wa uchumi unaoruhusu ma practical ya maproject makubwa ya kutosha kumfanya mhandisi akomae.Ndiyo maana huku west kila miezi fulani fulani ikifuika unakuta maofisini interns kibao wanajaa, tena hata hawalipwi hela nzuri, ni experience tu ya kufanya kazi.

Sasa nyumbani tunakosa uchumi na culture inayoweza ku absorb interns.Hili hata Nyerere alishalisema, kwamba how can a poor afford not to make use of its student while the richest nations are doing that? Jibu ni kwamba basically hatumthamini mtoto/mwanafunzi, tunaona hajui na atatuharibia kazi tu. Yeye mwenyewe (Nyerere) alikuwa ndiyo architect wa hiyo system halafu akajifanya kushangaa alivyong'atuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…