Nilicho observe personally ni kuwa sisi "tunachimba" sana kwa kutumia msuli, tunapapasa mitabu mingi sana, hatuhurumiani, tunapigana ma disco sana, kiasi kwamba tunatengeneza ma academicians waliobobea katika nadharia.
Wenzetu wanaweza wasifanye kazi sana kama sisi bali wanafanya yaliyo muhimu.Kwa mafano, kipindi kirefu kidogo kilichopita nikiwa primary nilipata kukaa na mtoto wa IST nikataka kujua wanavyofundishwa.Tukaanza kuulizana, formulaes tukafikia formulae ya kupata eneo la duara, mwenzangu akanipa formulae na historia ya formulae ilivyopatikana na kwa nini pi ni 22/7, basi mimi nilibaki mdomo wazi kwamba siku zote nimekuwa nikitumia pi kama 22/7 kama a given constant, wala mwalimu hakuniambia hii pi imetoka wapi na kwa nini ikawa 22/7.
In other words, elimu "yetu" ni mechanical zaidi, iko based kwenye kurudia kitu kile kile bila kikichunguza zaidi na iko canonical zaidi.
Wenzetu wanaenda kwenye mizizi ya vitu na hata hivyo vitu "vidogo" au visivyo "vigumu" wanavyosoma mitaala yao inawataka wavisome deeply.
Ukiwa na elimu hii canonical, huwezi kuwa adaptive au innovative, utataka kila kitu kije kama textbook examples ulizozizoea, which is hardly the case.
Ukijifunza the underlying principles (kama vile kwa nini pi ikawa 22/7) sio tu unaweza kuwa adaptive, unaweza hata ku design vitu vya kuwezesha a breakthough in the next paradigm.