Tukubali tu: Sisi wajinga... (I know, it hurts)

Tukubali tu: Sisi wajinga... (I know, it hurts)

Swali hapa sasa ni nani mjinga?
1)Serkali
2)wananchi
3)Wote wananchi na serikali?
Whats the solution then?
Kwasababu kuimba tu kuwa sisi ni wajinga bila ku propose solution then ni kama GLORIFICATION YA UJINGA!
Ni maoni yangu tuu!
 
Sasa ujinga huondoka; hivyo tusijisikie vibaya kwani katika kutambua ujinga wetu ndivyo tunavyotambua ni jinsi gani tunahitaji kujua zaidi (yaani kuondoa ujinga).

Nakumbuka vijitabu vya mfululizo wa "Ujinga wa Mwafrika", vilikuwa vinatumiwa sana na kina David Wakati na Khalid Ponera katika mazungumzo baada ya habari; lakini baadaye vilipigwa marufuku.

Nadhani wakati umefika wa kuvirudisha au nitaanzisha makala ya "ujinga wa Mtanzania"..
Kamanda MKJJ:
Vitabu vile na yale Mazungumzo baada ya habari yangekuwa yanatiliwa mkazo na hao walioshika dhamana za nchi hii, hapana shaka hiyo 70% isingekuwa inaenda nje ya nchi.
Tatizo ni ulofa mkubwa kwa wenye dhamana na watanzania kwa ujumla. Ulofa huu ndio umezaa ufisadi na kila mtz ambae ana ndoto ya kufanya kazi serikalini ana ndoto ya kuwa fisadi huu ndio ukweli...
 
Akili zetu zimedumazwana sera za ukiritimba,tukaingia katika soko huria kama wajinga na tunaendelea kuwa wajinga hadi siku akili zitakapozinduka.Si katika siasa tu bali hata katika uchumi wetu.

Ksumaba ile ileee....haimaliziki hadi generation hii iondoke au atokezee Mkombozi atakayefanya kama Jerry Rawlings kule Ghana.Halafu kipite kipindi cha miaka kama kumi tukiwa chini ya mtu kama Jerry....na ten tuanze kuingia katika enzi za Kufour.hapo tutaweza kuwa Watanzania wenye akili hasa baada ya kupiga deki hizi akili zetu na kusafisha kabisa uoza uliomo ndani yake.

Nilidhani ndugu yangu JK angeweza kuwa smart na kuleta kitu kipya lakini mpaka sasa naona hana will ya kufanya hivyo.
Hali inakuwa ngumu kila kukicha na ahadi za Mheshimiwa hazionekani kutekelezeka.
Kwa nini Kikwete asiwe kama Jerry? Kwa nini Kikwete asiwe kama Nelson Mandela?

Ni kwa sababu ya kasumba ya tangu awali kabisa ambayo inashindikana kuondoka kichwani mwake?Mbona ni mtu ambaye ametembea nchi nyingi tu duniani?
 
- Unapotunga sheria ya Usalama wa Taifa inayokataza watu wa usalama wa taifa kusimamia usalama huo ni ujinga!

- Unapotunga sheria ya maadili ya viongozi ambayo inaruhusu watu kukagua mali za viongozi lakini inakataza kumwambia mtu mwingine huo ni ujinga

- Unapokuwa na viongozi wawili wanaozungumzia jambo lile lile na wanapingana kama Ndulu na Mgonja au Mkulo na Ikulu huo ni ujinga

- Unapoacha mtuhumiwa anajiuzulu kwa kashfa halafu anaenda kupongezwa kwa ujasiri wa kujiuzulu huo ni ujinga

- Unapoacha kutafuta waliokwiba fedha unakamata watu wawili na wengine tisa kwa habari za kuchonga halafu unawaachilia kinyemela huo ni ujinga

Mjinga is what mjinga does!!
 
Mwanakijiji, rejea maneno ya FMES kuhusu viongozi wetu na sisi wananchi....
 
- Unapotunga sheria ya Usalama wa Taifa inayokataza watu wa usalama wa taifa kusimamia usalama huo ni ujinga!

- Unapotunga sheria ya maadili ya viongozi ambayo inaruhusu watu kukagua mali za viongozi lakini inakataza kumwambia mtu mwingine huo ni ujinga

- Unapokuwa na viongozi wawili wanaozungumzia jambo lile lile na wanapingana kama Ndulu na Mgonja au Mkulo na Ikulu huo ni ujinga

- Unapoacha mtuhumiwa anajiuzulu kwa kashfa halafu anaenda kupongezwa kwa ujasiri wa kujiuzulu huo ni ujinga

- Unapoacha kutafuta waliokwiba fedha unakamata watu wawili na wengine tisa kwa habari za kuchonga halafu unawaachilia kinyemela huo ni ujinga

Mjinga is what mjinga does!!

Kwa hiyo hii ishu goes beyond ile uliyoi'quote' kuhusu contractors kutoka nchi za nje? Katika hili la makandarasi, bado sijakupata Mkuu ni kitu gani kilichokufanya uone kuwa sisi ni wajinga!
 
Which ofcourse is UJINGA!
 
- Unapoacha mtuhumiwa anajiuzulu kwa kashfa halafu anaenda kupongezwa kwa ujasiri wa kujiuzulu huo ni ujinga

Mjinga is what mjinga does!!
Naam, hapa kamanda umenena, hii leo kuna mabandiko sio chini ya manne yenye kuzungumzia suala/tatizo/kero hii na katika ile hali yetu ya ulofa(ujinga) lawama zimekimbizwa kwa haraka kwa hao wapokeao watuhumiwa kwa vifijo na vigelegele huku wakisahau kuwa kuna bosi kubwa ambae alipaswa kumuwajibisha mtuhumiwa badala ya kumpa nafasi ya kujiuzuru ili apate nafasi ya kujinadi upya...

Simply ni Ujinga wa Mwafrika.. Maduka ya vitabu ya kanisa la katoriki(bookshop) walikuwa wasambazaji na wauzaji wazuri wa vitabu hivyo... Ukipata nafasi ya kuvipitia na kuweka online pengine itaweza kusaidia kuondoa upofu, zaidi tuna ujinga wa kutokusoma nakala na kubaki kushabikia udaku.... Labda vikiwa online itasaidia.

Au uwe unavirusha hewani kupitia KHL, kama macho ni mavivu kusoma sidhani kama masikio yatakuwa mavivu kusikiliza
 
Sisi Wajinga, unaongelea wanasiasa na walarushwa au Watanzania wanaofanya kazi kwa bidii kusaidia familia zao. Who is sisi?
 
Kama aliyosema Prof. Ndulu ndio ukweli wenyewe, nini basi kifanyike?
1. Kampuni yoyote ya Kigeni inayofanya kazi Tanzania lazima isajiliwe kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
2. Kampuni yoyote ya Kigeni inayosjiliwa kufanya fanya kazi Tanzania lazima iwe na account ya benki katika benki za Tanzania na
malipo yote kwa kampuni hiyo yafanywe kupitia accounti ya Tanzania.
3. Ikisha sajiliwa na kuwa na account ya Tanzania ni lazima ijisajili kama mlipa kodi TRA.
4. Itakuwa ni jukumu la TRA kufatilia makampuni yote yaliyosajiliwa kuhakikisha yanalipa kodi kulingana na mapato wayapatayo (Faida), kwa kazi za ujenzi wazifanyazo nchini kwetu.

Tatizo la mikataba mingi ya kimataifa kuna kipengele huwa kinawekwa kwamba kodi zote zitalipwa na client na siyo consultant. Matokeo yake mwenye kazi anamlipia kodi consultant/contractor. Kwa nini, sheria zetu za kodi zimekaaje?
 
Kwa hiyo hii ishu goes beyond ile uliyoi'quote' kuhusu contractors kutoka nchi za nje? Katika hili la makandarasi, bado sijakupata Mkuu ni kitu gani kilichokufanya uone kuwa sisi ni wajinga!

kwamba kuna sheria inayoweza kumfanya mwekezaji aondoke na fedha zote alizochuma Tanzania na inaruhusu remittance iende huko ng'ambo.

kama asilimia 70 ya wakandarasi ni wageni... kuna ugumu gani wa kuhakikisha kuwa mapato wanayopata kiasi kikubwa nacho kinabakia Tanzania? Kwa mfano, tumepewa hizi bilioni 700 na US, sisi tukashangilia; na zimetolewa kwa ajili ya miundo mbinu nk sasa tutakapotaka kuleta mkandarasi na wamarekani wakatuambia tutafute mkandarasi wakwao ina maana when it is all said and done, kiasi kikubwa "tulichopewa" kinarudi Marekani!!

huu ni ujinga.
 
Hatuwezi kuupona ujinga....bila ya kuona kuwa ndio uleeeee.

Kuuona ujinga completely objectively na kwa uhalisi wake wote.... Huko ni kuonyesha dalili za awali za kupona. Kitendo hicho sio cha kijinga kabisa.

Ni kitendo cha kuerevuka.

Tuonyeshe kuuerevuka na kukomaa kwetu..kwa Kukubali sisi ni wajinga wa kiwango kizuri tu, kwani kukubali hivyo hakutufanyi wajinga!
 
- Unapotunga sheria ya Usalama wa Taifa inayokataza watu wa usalama wa taifa kusimamia usalama huo ni ujinga!

- Unapotunga sheria ya maadili ya viongozi ambayo inaruhusu watu kukagua mali za viongozi lakini inakataza kumwambia mtu mwingine huo ni ujinga

- Unapokuwa na viongozi wawili wanaozungumzia jambo lile lile na wanapingana kama Ndulu na Mgonja au Mkulo na Ikulu huo ni ujinga

- Unapoacha mtuhumiwa anajiuzulu kwa kashfa halafu anaenda kupongezwa kwa ujasiri wa kujiuzulu huo ni ujinga

- Unapoacha kutafuta waliokwiba fedha unakamata watu wawili na wengine tisa kwa habari za kuchonga halafu unawaachilia kinyemela huo ni ujinga

Mjinga is what mjinga does!!

Haya ndiyo mapungufu yaliyoko kwenye msingi mzima wa sheria zetu.

Mzee Mwkjj, watanzania siyo wajinga, ni maskini na wasiojiamini! Lakini viongozi wetu ni wajinga wakubwa!
 
Ukiwa na watu masikini na wasiojiamini halafu wakachagua watu wajinga, combination hiyo inatisha wangu!
 
Back
Top Bottom