Tukubali utawala wetu umeshindwa, umetuangusha, umejiangusha na kutia aibu

Tukubali utawala wetu umeshindwa, umetuangusha, umejiangusha na kutia aibu

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,709
Kwa yaliyotokea Tanzania mwaka jana ambapo, kwa mara ya pilli, watawala wetu wachovu na hovyo waliua watu wetu tokana na maandamano ya Oktaba 29 na kinachoendelea kwa sasa, ni dhahiri utawala wetu umechoka, umeshindwa, na hata kufulia. Umejaribu kutulisha udini uchwara na kushindwa. Umejaribu kutengeneza maadui feki, umeshinda. Umejitahidi kutaka kuficha ukweli umeshindwa.

Unajitahidi kuonyesha unafaa wakati haufai kabisa, nako umeshindwa. Bado tutaendelea kudai haki japo tunahimizwa tulinde amani ambayo watawala kidhabi wameivuruga. Wanajitahidi kujionyesha kuwa wa misuli ya kutawala lakini wameshindwa vibaya.

Wanahaha na kutapatapa wakitafuta suluhu bila kukubali kuwa wao ndiyo kiini cha tatizo wanalikwepa, nayo wameshindwa. Wameshindwa kulhali na katika kila jitihada. Wanasingizia hili na kuzua lile ili wakubaliki lakina wameshindwa vibaya.

Tungekuwa na mfumo mzuri wa utawala, hawa mabazazi wangekuwa korokoroni wakingoja kukatiwa vifungo kwa madhambi na makosa waliyotutendea kama watu na taifa.

KWA UFUPI, NI KAMA HATUNA SERIKALI, NA KAMA IPO INAPWAYA NA IMESHINDWA VIBAYA SANA. SAMUYA MUST GO. Tulianzishe tena.
 
Nchi ilishajifiaga mda saiz inaendaenda ilimradi tu.
 
Ogopa kufanya jambo kwa kulazimisha halaf unyimwe ushirikiano, hata kama jambo lenyew ni jepes, utakua mzigo mzito sana
 
Back
Top Bottom