MsaniiMkubwa
Member
- Sep 2, 2026
- 31
- 60
Siku za karibuni nilipata fursa yakutembelea makaburi walipolazwa baadhi ya Wapendwa wangu pale jijini Arusha.Miongoni mwa mabadiliko niliyokutana nayo ni pamoja na ongezeko kubwa la Makaburi na wengine ni Watu niliowahi kuwafahamu ila sikujua kama wameshatangulia mbele ya haki.
Katika pitapita zangu nilishangazawa na moja ya kaburi ambalo lilikuwa na mvuto wa kipekee.Sina tatizo na urembo wa kaburi lile hata kama wangelipamba kwa Tanzanite na dhahabu kote.Kilichonitamahusha ni nafasi waliyoichukuwa huku wakijua fika lile ni eneo la uma (public).
Sijui kwa nini Mamlaka ikawaruhusu kufanya vile.Pamoja na umaarufu wa aliyezikwa pale nilijiuliza kama kweli yeye angeshirikishwa kabla juu ya jambo lile kama angeridhia.
Ndugu na Jamaa zako watafanya wanavyofanya kukuheshimisha kutokana na nafasi uliyokuwa nayo lakini kumbuka jina linalobaki pale ni la kwako.Na wengi wakiwemo Wajukuu wako na Vilembwe watatafsiri hali ile kama ulikuwa Mtu Mbinafsi Duniani na hukutosheka mpaka Kaburini umetamani nafasi ya Wenzako Watatu ukae wewe mnwenyewe.
Tuache usia wa maelekezo ili tusibaki wachoyo mpaka Kaburini. Tena ukizingatia wengine tulikuwa Watumishi wa uma, jina lenyewe umejenga kwa kuwapunja wenzako vipi tena iwe hivyo mpaka kaburini?.