Fuvu:
huyu alikuwa discipline master. noma. mwembambaaaa kama snoop dogg.
Kisu:
Bonge la headmaster niliyewahi kumuona. Aligeuza shule iliyokuwa ya wahuni kuwa shule yenye heshima inayofaulisha kwa kiwango cha juu bila mitihani kuvuja. Huyu jina yake kamili ni Kisusange. Kuna wakati alihamaki, akauliza wanafunzi: "naskia kuna wanafunzi wananiita Kisu, hivi wewe baba yako unaweza kumuita ba?"
Nakumbuka baadhi ya majina ya walimu waliyopewa na wanafunzi kama ifuatavyo:
1. Solar system - mwalimu wa geograph form 1 au 2 alifundisha solar system akapatiwa jina hapohapo
2. Bambabay - mwalimu wa commerce form 3 alikua akielezea transport system,akaitaja bambabay ndio ikawa jina lake.
3.magazijuto - mwalimu wa hisabati darasa la saba alifundisha magazijuto na yeye ndio ikawa jina lake la utani au aka
4. Chonya of chilimwa - mwalimu wa kiswahili secondary alisoma habari za chonya of chilomwa akawa ndio jina lake
tupeni majina zaidi
Mmenikumbusha mbali na hayo majina.
Nilikua Kwiro secondari, headmaster wetu aliitwa Antony Magambo, sie tulimwita Mbwiko, mpaka leo sijui maana yake! Alikua mkali kama pilipili, hakua na kosa dogo , ni bakora kwakwenda mbele. Alitunyosha hakika. . . . Mungu ampe maisha marefu popote alipo.