Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Hahaaaaa bila shaka huyo atakuwa ni mwalimu Hesero ..Azimio Primary school (musoma)Kwa walisoma bwiru boys kuna mwalimu mmoja alikuwa anaitwa muganyizi au bega jina la utani,huyu bwana alikuwa balaa alifundisha engneering science,electronics,electrical engineering na electrical installation kwa wakati mmoja masomo yote na kufanya boys kushika nafasi za juu kitaifa enzi zetu..Minority-mwalimu wa radio and tv servicingmchizi-huyu ticha alikuwa ana mikwara sana na alikuwa na macho mekunduu all the timemwl mazuki-alisifika kwa kigari chake aina ya volkswagen(mwendo wa kobe)mmmh kweli tumetoka mbali
 
aha haaa,umenikumbusha mbali,cjui yupo wapi huyu mzee cku hizi,aliwahi kunityt,kisa nimeingia dini darasa la wahindi,palikuwa hapatoshi,alichukua madaftari yangu akakaa nayo karibu siku nzima!daaah

Yule take ur home and go books.alivuma sana.Alishafariki kitambo.
 
umenikumbusha mbali sana huyu ticha alishanipiga fimbo mpaka nkajikuta nauliza hiki nini, kunamwingine anaitwa kagashe naye ni noma.

Kagashe yupo,Jesus alishatangulia mbele za haki. 2 Jump (Turuka) vipi?
 
sukuma nidandi- teacher wa hisabati std 6
kipilipili - mwl wa hisabati std 7.alikua ananata huyu balaa. mkali kama pilipili kichaa
totozi - mwl wa fizikia form 1, alikua anapenda kuzengea sana njuka
IPP - mwl wa Gs form v na vi yani huyu akiingi class hadi atoke ni pumba tu.( International pumba producer) nasikia siku hizi kawa headmaster huko mpwpwa. lol siwapatii picha wanaoongozwa nae.
 
piano-wa english darasa la sita.
sikuelewi-alikua hasikilizi sababu yoyote ya kosa, so alikua anapenda kutumia neno "sikuelewi"
ngwema-alikua ka jenerali ngwema
kishati kimoja-alikua na koti lake alilipenda sana
dikodiko-hyu aliuamnoko kweli kuadadake
tozi-brazamenbrazamen
 
mi namkumbuka mmoja tu kipindi nasoma rubya seminary mwalimu wa hesabu alikuwa akiitwa CHARCOAL


 
mi namkumbuka mmoja tu kipindi nasoma rubya seminary mwalimu wa hesabu alikuwa akiitwa CHARCOAL



Mkuu umenikumbusha Rubya Seminary!
Miaka ya nyuma alikuwepo Bursar mmoja akiitwa Fr. Pius Rutechura - tulikuwa tukimuita jina la utani Bingwa.
 
Mwalimu Domain, alikuwa anafundisha hesabu na alophamia shuleni kwetu topic aliyoanza nayo ni ya mambo ya domain na range. Kwa hiyo kila dakika utamsikia akiuliza what is the domain?

Mmh! Mwl Domain! Kama alikuwa na upara na mwanya basi nami kanifundisha namba (Maths). Tulikuwa tukimuita hivyo hivyo 'Mwl Domain'!
 
mazengo complex tulikvwa na mwamfupe(unyamaunyama)yunus(popobawa)komba(kipatiko)sichone(njenje)
 
Muzungu alikuwa ticha wa namba halafu hajui ki2 mazengo complex
 
Pande za Mbeya secondary kuna ticha tulikuwa tunamwita "Tod" kwan alikuwa na macho makubwa.

Near by Ileje Mbeya.
 
Haha umenikumbusha huyu Mwalimu vile viatu vyake na vimiguu vyake na Moustach... hata sisi tulimuacha akiwa na hicho kitabia...1995 Pamoja na Kijo
Kuna Ticha jina nimelisahau Tulikuwa tunamuita Baiskeli akitembea kama ananyonga Baiskeli sababu ya ulemavu wa Mguu wake..

Kuna Teacher alikuwa anakaa Usa river akapewa jina la mama wa USA
GM Mlimkuta?

Kuna Teacher mmoja alikuwa anatumia english ya kwenye Dictionary kwa sana yaani akiongea ni vituko tu na alikuwa ni Mshamba mshamba hivi hata uvaaji wake na viatu lol jina nimemsahahu siku alikuta Wanafunzi kwenye Mikahawa wamedoja akawaandika majina wote na kila mwanafunzi alikuwa akimtajia majina ya wachezaji wa Yanga kuanzia Steven Nemes karibu list nzima... kwenye parade si ilikuwa wiki ya zamu yake akaanza kuita yale majina wajitokeze mbele si kicheko hicho kwa wanafunzi mstalini alipoona ujinga akawa anawadakua mmoja mmoja kwa sura huku akiwaita kwa yale majina wewe Minziro si nakuita huitiki jeuri sio....
 
NKUU Prmary school,hii iko machame tulukua na mwalimu mmoja tulimwita KINNCHI,hii ilikua ni mwaka 1990alikua anapenda sana kutongoza wanafunzi.
 
Fiudo-mwalimu anyefundisha Civics, pat ya modes of production (Feudalism)
Exotic-Mwalimu aliyepewa jina baada ya kufundisha exotic breeds of livestock

huyo fyudo ni wa Tosamaganga?
 
Jamani Mwl Magambo yupo? Alikuwa second master Nganza miaka ya late 1980s!

Nsumba pale
soujer: mwl kaboja manual work
Bwana pepsi: H/m mbaga
Dj manta: alikua anachapa vichache ila vichungu
Makemiko: chemistr practical
Mb dog: ana mwembe kichwan
Jamshid: kuna mwanafunz wa jina hilo alimsumbua sana dspln master likawa jna
Mwananch: alipenda kuita wanafnz hvyo mwl lumwecha
Tha tha tha: mwalim magambo alikua na kigugumizi
chief nanga: alifundsha litureture msemakwel
A mean: alifundisha jiog mwl lenin
now now: mwalim wa kemia kila dk lzma aseme now mwk kagua
 
FUVU Mwembamba ana kichwa kikubwa chembamba hakina nyama sana ticha wa hisabati azabway.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…