Haha umenikumbusha huyu Mwalimu vile viatu vyake na vimiguu vyake na Moustach... hata sisi tulimuacha akiwa na hicho kitabia...1995 Pamoja na Kijo
Kuna Ticha jina nimelisahau Tulikuwa tunamuita Baiskeli akitembea kama ananyonga Baiskeli sababu ya ulemavu wa Mguu wake..
Kuna Teacher alikuwa anakaa Usa river akapewa jina la mama wa USA
GM Mlimkuta?
Kuna Teacher mmoja alikuwa anatumia english ya kwenye Dictionary kwa sana yaani akiongea ni vituko tu na alikuwa ni Mshamba mshamba hivi hata uvaaji wake na viatu lol jina nimemsahahu siku alikuta Wanafunzi kwenye Mikahawa wamedoja akawaandika majina wote na kila mwanafunzi alikuwa akimtajia majina ya wachezaji wa Yanga kuanzia Steven Nemes karibu list nzima... kwenye parade si ilikuwa wiki ya zamu yake akaanza kuita yale majina wajitokeze mbele si kicheko hicho kwa wanafunzi mstalini alipoona ujinga akawa anawadakua mmoja mmoja kwa sura huku akiwaita kwa yale majina wewe Minziro si nakuita huitiki jeuri sio....