Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Tukumbuke majina ya utani kwa walimu shule tulikotoka

Mwagaloni"-Ikungi sec singida,

Alikuwa anatembea na kigaloni amejaza pombe humo ndani hivyo hata kiwa ofc anazimua kidogo,
 
Kilamba sugar! Mwl Geseco alikuwa anabinua midomo yake kama analamba sukari
 
Na je kwa wale tuliobahatika kuwa Walimu mnajua majina mnayoitwa??
Mimi naitwa Mwehu aka stone Age sijui kwa nn
 
Dudu, asili ya jina silijua, he was really dudu.

Contra (kifupi cha contradictions) alikuwa 2nd Master wa ukweli, ukipitia mikononi mwake utamwona mchungu lakini ukiishamaliza shule, thamani yake ni kubwa mno.

DH Huyu alikuwa Mwalimu wa Kiswahili O-level, anaanza na jina la D, akawa anavaa raba za Double Hapiness (DH), aka Dingi Hajiwezi shuleni, kilabuni hadi kanisani. Hakuwa mnoko, alikuwa kimbilio la wanafunzi wakiwa na issues nzito. Nampenda sana, kwasababu ya busara zake tatizo ni kuwa alipata mshahara mdogo na akawa na dependants wengi.
.Haha tosamawe hiii
 
Patriot....aah mwl. wangu Civics alituambia saana kuhusu uzalendo basi jina akapewa
Africanus...mwl wangu History alinifanya niipende History...Maruku S.S Bukoba

Mkuu mwaka gani huo?Mimi nimehitimu 2000 na history tulikuwa na ticha Felix Nyamwihula a.k.a Zinjanthropus
 
MANURE: adhabu yake kubwa ilikuwa kuleta samadi. Ikabidi aitwe manure. Mwingine tulimuita MR. SOOO. Alipenda kuongea sana hili neno. Mwalimu wa english F3 ilibidi tumuite SUFIX kwa sababu alianza kufundisha sufix na prefex.

Mr SOO, Manure na Suffix nawafahamu pia
 
Nyamayao: mwalimu wa book-keeping st. anthony's mbagala huyu alikuwa anafanana na Nyamayao yule mwigizaji wa kaole enzi zile

Pipiro: Mwl. wa hesabu st. anthony alikuwa mfupi na mkorofi sana afu mbishi.

Desert Boy: mwl. wa history alijiita mwenyewe hilo jina akimaanisha yeye ni mgumu eti.
 
Haha umenikumbusha huyu Mwalimu vile viatu vyake na vimiguu vyake na Moustach... hata sisi tulimuacha akiwa na hicho kitabia...1995 Pamoja na Kijo
Kuna Ticha jina nimelisahau Tulikuwa tunamuita Baiskeli akitembea kama ananyonga Baiskeli sababu ya ulemavu wa Mguu wake..

Kuna Teacher alikuwa anakaa Usa river akapewa jina la mama wa USA
GM Mlimkuta?

Kuna Teacher mmoja alikuwa anatumia english ya kwenye Dictionary kwa sana yaani akiongea ni vituko tu na alikuwa ni Mshamba mshamba hivi hata uvaaji wake na viatu lol jina nimemsahahu siku alikuta Wanafunzi kwenye Mikahawa wamedoja akawaandika majina wote na kila mwanafunzi alikuwa akimtajia majina ya wachezaji wa Yanga kuanzia Steven Nemes karibu list nzima... kwenye parade si ilikuwa wiki ya zamu yake akaanza kuita yale majina wajitokeze mbele si kicheko hicho kwa wanafunzi mstalini alipoona ujinga akawa anawadakua mmoja mmoja kwa sura huku akiwaita kwa yale majina wewe Minziro si nakuita huitiki jeuri sio....

Kijo bado yupo mpaka sasa pusi na mzee mungure washatngulia mbele ya haki hao wengine siwafaham nadhani walishaondoka
 
Kijo bado yupo mpaka sasa pusi na mzee mungure washatngulia mbele ya haki hao wengine siwafaham nadhani walishaondoka

Mwenyezi Mungu azilaze Roho za Marehemu pahali panapostahili Amina...

Pusi alikuwa ana mikwara sana...

Bashahija vipi Yupo bado? Thobis nilisikia yupo Tengeru kama sikosei Teacher alikuwa cha Pombe sana na Fegi kwa sana... Kuna Wanafunzi wenzetu nao nimesikia wametangulia kama Goodson Magesa,Golden Elasto,Elisante Pallangyo... Mungu azilaze Roho za Marehemu pahali panapostahili

Mkuu bado waishi maeneo hayo? Dah Long time sana nikikumbuka
 
Mwenyezi Mungu azilaze Roho za Marehemu pahali panapostahili Amina...

Pusi alikuwa ana mikwara sana...

Bashahija vipi Yupo bado? Thobis nilisikia yupo Tengeru kama sikosei Teacher alikuwa cha Pombe sana na Fegi kwa sana... Kuna Wanafunzi wenzetu nao nimesikia wametangulia kama Goodson Magesa,Golden Elasto,Elisante Pallangyo... Mungu azilaze Roho za Marehemu pahali panapostahili

Mkuu bado waishi maeneo hayo? Dah Long time sana nikikumbuka

Mimi nliondoka mwaka 2008 taarifa nazipata kwenye mitandao tu halafu naona ni wakitambo kweli 1995
 
Mkuu mwaka gani huo?Mimi nimehitimu 2000 na history tulikuwa na ticha Felix Nyamwihula a.k.a Zinjanthropus

2002 Nyamwihula amefariki 2002 unamkumbuka shafi; magayane..kiswazi na civics daah kitambo..géo akiwa ngirwa
 
Scarcity - mwalimu wa economics A level (alikuwa akiisema "scarcity" hadi anasinzia)
Torrential - mwalimu wa geography A level (alikuwa akisema "torrential rainfall" kama umekaa mbele unapewa mvua ya mate ya kutosha)
Lubumbashi - mwalimu wa Geography O level....ile topic ya Congo
 
hedaru sec 2003-2006 kulikua na ticha jina halisi mr kisese aka mbogo
alikua mbogo kweli kweli.akikushika na kosa hana msamaha,huwa anauliza kwani ukikanyaga moto unaungua hapo hapo au baadae?
afu anakupa option ya kuchagua idadi ya fimbo kati ya 2 au 6, ole wako uchague 2 hutokaa chini wiki nzima
 
Back
Top Bottom